Sikubali dharau, hata kama leo sina kitu!

Sikubali dharau, hata kama leo sina kitu!

Kuna kitu kimoja nataka watu waelewe kuhusu mimi. Sipendi dharau, na sijawahi kuona umaskini wa mtu kuwa ruhusa ya kumdhalilisha.

Leo sina pesa, sawa. Leo nimelewa, sawa. Lakini msichanganye hali yangu ya leo na thamani yangu kama binadamu. Kukosa kitu mfukoni hakumaanishi umekosa akili, heshima wala utu.

Mimi naweza kukaa kimya nikadhaniwa sina uwezo, nikacheka nikadhaniwa sina mawazo, au nikapitia kipindi kigumu nikadhaniwa nimeisha. Lakini ukweli ni kwamba maisha yana misimu yake.

Sihitaji kujifanya tajiri ili niheshimiwe. Wala sihitaji kumdharau mtu ili nionekane nina thamani.

Ninaweza kukosa pesa, lakini sitaki kupoteza utu wangu kwa sababu ya pesa.

Na kama leo nimelewa, kesho ni siku nyingine. Maisha yanaendelea.

Kitu kimoja tu: usinipime kwa nilichonacho leo, maana hata wewe hujui kesho yako imebeba nini.

HESHIMA KWANZA. MENGINE NI MAJARIBU YA MAISHA.

— Mawazo ya mtu ambaye bado hajafika, lakini hajakubali kushindwa.
Huna kitu bado unalewa
Kwa nini sasa wasikudharau

Wanakuona hauna future shtuka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom