Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,997
- 20,329
Mwaka 1961-1964 tangu taifa la Tanganyika litoke kupata uhuru lilikuwa na watu milioni 10+, na 88% walikuwa ni wajinga sana, 10% walikuwa ni wajinga wastani wakati 1% walikuwa ni werevu, na 1% walikuwa ni werevu sana!
Kutoka 1965-1985 sasa tukiitwa Tanzania, taifa lilikuwa linakadiriwa kuwa na watu milioni 30+, na watu 78% walikuwa ni wajinga sana, 12% walikuwa ni wajinga wastani, wakati 7% walikuwa ni werevu, na 3% walikuwa ni werevu sana!
Mwaka 1985-2000 taifa likikadiriwa kuwa na watu milioni 40+, watu 68% walikuwa ni wajinga sana, 22% walikuwa ni wajinga wastani, wakati 8% walikuwa ni werevu, na 2% walikuwa ni werevu sana!
Mwaka 2000-2013 taifa likikadiriwa kuwa na watu milioni 44+ watu 76% walikuwa ni wajinga sana, 20% walikuwa ni wajinga wastani, wakati 3% walikuwa ni werevu, na 1% walikuwa ni werevu sana!
Sababu za kushuka kwa ongezeko la werevu na kupanda kwa ongezeko la wajinga miaka ya hivi karibuni kunatajwa kuwa kumechochewa na mfumo mbovu wa elimu nchini.
Sasa kwa wafanya siasa hii ni rahisi sana kwao kwakuwa haiwalazimu kutumia sheria ya MIMMK ambazo humuongoza mwanasiasa kuendesha siasa zake, wale wenzangu tuliobahatika kusoma elimu ya juu ya mikakati ya kisiasa mtakuwa mmenielewa.
utamaduni wa Wajinga:
Aghalabu Wajinga huishi kwa mifano. Yaani huwa hajui na kubadilika kwake hadi tukio limtokee. Kwa mfano, wakati Mkapa anapitisha utandawazi na ubinafsishaji, marehemu profesa Chachage L. Chachage aliandika paper na kuziwakilisha sehemu mbalimbali ikiwemo katika mkutano wa AU, Ethiopia mwaka 2000. Akawaambia watanzania jamani huo utandawazi haupo hivyo kama unavyohubiriwa na wanasiasa wa CCM na WASOMI wasaliti waliolipwa fedha ili waupambe mfumo huo mchafu.
Watanzania hawahawa walimjia juu Chachage na kumwita kuwa ana njaa. Na isitoshe mstaafu Mkapa akamkejeli kuwa wasomi wanapenda sana kulalamika lakini hawaji na suluhisho. Miaka michache baadaye watanzania wameona matokeo ya utandawazi kwa mifano. Sasa lililobaya ni kuwa serikali ya CCM au watanzania wenyewe hawajawahi kujiuliza tangu mfumo wa utandawazi uingie nchini umeleta faida gani.
Aidha Wajinga huwa ni watu wa kukaririshwa. Kwa mfano watanzania wakaririshwa kuwa tatizo yaliyosababishwa na serikali wayaite changamoto, na ugumu uliotokana na serikali kutengeneza mazingira wezeshi wamekaririshwa wayaite fursa. Nako utakuta mtanzania anatamka kama mwehu, "watanzania fursa zipo nyingi na nyingine zinaonekana kwa jicho la tatu" sasa ukimuuliza hizo fursa zikowapi, hakuambia bali atakubabaisha wewe zitafute tu utazipata.
Na lingine Wajinga huishi kwa mazoea, yaani kwa mfano, unga umepanda bei hapigi hata kelele atalalamikia ndani ya nafsi yake, mwishowe anazoea ile hali. Yaan kwa kifupi mjinga hajui haki yake, hajui wajibu wake ni upi, na hajui wajibu wa serikali kwake.
Sasa, Wajinga muelewe kuwa ujinga ni talanta, na talanta zenu zinaendelezwa kwa mukusudi ili wengine wanufaike.
Kazi za serikali ni 2: kuendeleza watu na kuwalinda watu. Ajira na kazi ni sehemu ya serikali ya kuwaendeleza watu. Serikali Ina kazi ya kuwafanya watu wake wawe matajiri, waheshimike kiutajiri na kimaarifa. Na ni wajibu wa serikali kuvilinda vyote. Sasa mjinga anaamini ataheshimiwa kwa umasikini na unyonge wake.
Kipimo rahisi cha kujua ujinga wa watanzania hasa hawa wanaoitwa wa kizazi kipya angalia maoni yao juu mada hii hapa hapa.
Taifa la wajinga hushangilia uovu na kuuchukia ukweli...