Siku za mikutano iwe likizo - barabarani hatupiti...

mbongopopo

JF-Expert Member
Jan 24, 2008
1,611
759
Tuchukueni likizo na watoto tusiwapeleke shule

Labda serikali itafungua macho na kufanya kitu maana hii ni kali hapo watakapoona wanafungia barabara gari moja au mbili

Na inazidi kuwa mbaya zaidi watu walale masaa mawili waamke tena kwenda kuangaika sababu ya nini wasichoweza tufurahisha pia?
 
Hoja ya kuwa likizo inatia mashaka saana. Halafu uchumi wa nchi inakuwaje? Kimsingi kuweka mkutano pale Mlimani City ni poor planning. Miundo mbinu mibovu, hivi kwanini wasiweke Kilimanjaro pale na wageni wa nje watafutiwe hoteli maeneo yale? Ili watu wa barabara za nje ya jiji wasalimike na adha ya foleni?
 
Ukiangalia hili jambo kuna makampuni yanawapa wafanyakazi wao ruhusa kufanya masaa machache hiyo tayari inaaribu etc

Na hii inasumbua maeneo ya Dar kwa hiyo ndio hivyo uchumi utakuwaje kama siku ya kawaida kwa mafoleni haya???

Ni bora watu kukaa home nakufanya mengineyo as wengine wanafanya hivyo kuliko kushinda barabarabi siku nzima uchumi unapatikana hapo?

Ndio maana nimesema watafunguka macho kama ndio kilimanjaro etc watatumia
 
kwa maoni yangu mkutano huu ulifaa ufanyike Arusha kwani Arusha ndio makao makuu ya EAC. Why this meeting was not held there and held in Dar instead is a million dollar question!!!
 
Hoja ya kuwa likizo inatia mashaka saana. Halafu uchumi wa nchi inakuwaje? Kimsingi kuweka mkutano pale Mlimani City ni poor planning. Miundo mbinu mibovu, hivi kwanini wasiweke Kilimanjaro pale na wageni wa nje watafutiwe hoteli maeneo yale? Ili watu wa barabara za nje ya jiji wasalimike na adha ya foleni?

na uchumi wetu sisi wananchi unakuwaje tunapokaa foleni zaidi ya masaa mawili? Kabla ya kupanga mkutano pale Mlimani City wanapaswa kuangalia mambo yote kwa upana zaidi. Wanaweza kwa mfano ku-upgrade barabara nyingine zinazopita mitaani ili kupunguza msongamano kwenye barabara kuu. Kuna barabara kadhaa kutoka Mwananyamala mpaka Mwenge lakini zina hali mbaya sana. Hizi wanapaswa kuzinjenga kwa kiwango cha lami
 
Back
Top Bottom