Jorge WIP
JF-Expert Member
- Jul 12, 2018
- 3,567
- 5,289
Dakika chache zilizopita ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa ila nina utaratibu wa kuacha tu siku ipite bila kufanya taratibu yoyote.
Lakini marafiki zangu leo wamenishangaza baada ya usiku kunitegea na kunifanyia sherehe, waliniita kama kuna dharura nikaenda kukuta wamepanga kila kitu aisee sikutegemea kabisa!
Nikauliza kwanini wameingia gharama, wakasema haijalishi upendo wao kwangu hauna lebo ya bei, tukio dogo la leo limenirudishia imani kidogo katika ubinadamu, nilijua tumebaki magaidi tu, kumbe kuna watu wazuri bado wapo ndani ya dunia hii na wanajali.
Nawasihi msikate tamaa mlioumizwa kwenye mahusiano, yawe ya mapenzi au kindugu, jua ipo siku utakutana na watu wanaokujali na kuona thamani yako.