Siku yangu ya kuzaliwa marafiki wamenifanyia sherehe ya kushtukiza, upendo bado upo jamani katika dunia

Jorge WIP

JF-Expert Member
Jul 12, 2018
3,567
5,288
Dakika chache zilizopita ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa ila nina utaratibu wa kuacha tu siku ipite bila kufanya taratibu yoyote.

Lakini marafiki zangu leo wamenishangaza baada ya usiku kunitegea na kunifanyia sherehe, waliniita kama kuna dharura nikaenda kukuta wamepanga kila kitu aisee sikutegemea kabisa!

Nikauliza kwanini wameingia gharama, wakasema haijalishi upendo wao kwangu hauna lebo ya bei, tukio dogo la leo limenirudishia imani kidogo katika ubinadamu, nilijua tumebaki magaidi tu, kumbe kuna watu wazuri bado wapo ndani ya dunia hii na wanajali.

Nawasihi msikate tamaa mlioumizwa kwenye mahusiano, yawe ya mapenzi au kindugu, jua ipo siku utakutana na watu wanaokujali na kuona thamani yako.
 
Dakika chache zilizopita ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa ila nna utaratibu wa kuacha tu siku ipite bila kufanya taratibu yoyote.

Lakini marafiki zangu leo wamenishangaza baada ya usiku kunitegea na kunifanyia sherehe, waliniita kimtego kama kuna dharura nkaenda kukuta wamepanga kila kitu aisee sikutegemea kabisa!

Nikauliza kwanini wameingia gharama, wakasema haijalishi upendo wao kwangu hauna lebo ya bei, tukio dogo la leo limenirudishia imani kidogo katika hii ubinadamu nilijua tumebaki magaidi tu,kumbe kuna watu wazuri bado wapo ndani ya dunia hii na wanajali.

Nawasihi msikate tamaa mlioumizwa kwenye mahusiano, yawe ya mapenzi au kindugu, jua ipo siku utakutana na watu wanaokujali na kuona thamani yako.
Una umri gani? Umeshaanza kudaiwa kodi ya nyumba au school fees?
 
Ila JF members wanapenda nyuzi za masikitiko wakupe pole za kinafiki

Sasa kosa la mleta mada ni lipi?kushare furaha yake kwa kuoneshwa upendo na wanaomzunguka?

Alichofanyiwa inahusiana vipi na utoto/kutokuwa na majukumu?

Hongera bhana Jorge WIP
Hongera pia kwa kufikisha umri uliofikisha,Mungu akakujaalie kila lililo jema
Negative comments wala usizingatie
 
Ahsante sana Joanah...watu wengi wangekuwa na mtazamo kama wako basi tungebahatika

Mfano: Maada ingekuwa “majukumu yamenishinda sina pesa naumbuka” wangechangia hao au “gf wangu kachukuliwa na sponsor” ungeona response yake
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom