Siku yangu ya kuzaliwa marafiki wamenifanyia sherehe ya kushtukiza, upendo bado upo jamani katika dunia

Watu wanafikira potofu sana kila jambo hawakosi la kusema, ndio maana unatakiwa usiangalie watu wanasema nini, ili mradi huvunji sheria za nchi wala humnyimi uhuru mtu mwingine wewe fanya unaloona linakufaa, ukisikiliza hawa watu watakutumbukiza shimoni, watu wengine hawana ule wasaa wa kuweza kufurahia na marafiki, hivyo wanataka na kila anaewazunguka wawe hivyo. HAIWEZEKANI.
Umenena vyema ukipata nafasi ya kufurahia furahia maisha furahia tunaishi Mara moja tu hamna kipindi Cha pili
 
si kweli. ungekuwa adult jambo dogo kama hilo usingepoteza muda wako kuliandikia. wewe bado ni katoto
It goes the same way kwako kama na wewe ungekua mtu mzima usingepoteza mda kuleta negative energy humu
 
Wadau wa JF tupunguzeni Makasiriko, maisha ndio ni magumu ila negative energy imezid sana... huu ungekuwa uzi wa huzuni watu wangecheka kweli humu
 
Dakika chache zilizopita ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa ila nina utaratibu wa kuacha tu siku ipite bila kufanya taratibu yoyote.

Lakini marafiki zangu leo wamenishangaza baada ya usiku kunitegea na kunifanyia sherehe, waliniita kama kuna dharura nikaenda kukuta wamepanga kila kitu aisee sikutegemea kabisa!

Nikauliza kwanini wameingia gharama, wakasema haijalishi upendo wao kwangu hauna lebo ya bei, tukio dogo la leo limenirudishia imani kidogo katika ubinadamu, nilijua tumebaki magaidi tu, kumbe kuna watu wazuri bado wapo ndani ya dunia hii na wanajali.

Nawasihi msikate tamaa mlioumizwa kwenye mahusiano, yawe ya mapenzi au kindugu, jua ipo siku utakutana na watu wanaokujali na kuona thamani yako.
Hongera
 
Kikwete naye juzi alisherekea birthday
Rudi kasikilize interview yake kwasababu alifanya birthday juzi halafu urudi tena hapa familia yake ndo ilitaka vile ila yeye huwa hafanyagi upuuzi ule
 
Rudi kasikilize interview yake kwasababu alifanya birthday juzi halafu urudi tena hapa familia yake ndo ilitaka vile ila yeye huwa hafanyagi upuuzi ule
We ni mjinga sana naweza nikasema hivyo mleta uzi amesema yeye hakua na mpango wa kufanya birthday Ila marafiki zake ndo wamemfanyia na amewashukuru kwa upendo Mkubwa waliomuonyesha hio inatofauti Gani na kikwete ambayo familia yake ilimfanyia
 
Kummko
 
pwilo ustaarabu ni bure aisee haujaitwa ku comment kwanini unamtukana jamaa bila sababu, acha upuuzi hauko kijiweni na low lives wenzako hapa
 
Dakika chache zilizopita ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa ila nina utaratibu wa kuacha tu siku ipite bila kufanya taratibu yoyote.

Lakini marafiki zangu leo wamenishangaza baada ya usiku kunitegea na kunifanyia sherehe, waliniita kama kuna dharura nikaenda kukuta wamepanga kila kitu aisee sikutegemea kabisa!

Nikauliza kwanini wameingia gharama, wakasema haijalishi upendo wao kwangu hauna lebo ya bei, tukio dogo la leo limenirudishia imani kidogo katika ubinadamu, nilijua tumebaki magaidi tu, kumbe kuna watu wazuri bado wapo ndani ya dunia hii na wanajali.

Nawasihi msikate tamaa mlioumizwa kwenye mahusiano, yawe ya mapenzi au kindugu, jua ipo siku utakutana na watu wanaokujali na kuona thamani yako.
M ninachojua ilikua siku ya watu wenye matatizo ya afya ya Akili na waziri akasisitiza kuna watu wanatakiwa waende mirembe
 
M ninachojua ilikua siku ya watu wenye matatizo ya afya ya Akili na waziri akasisitiza kuna watu wanatakiwa waende mirembe
Kuna jamaa comments kadhaa za juu hapo anatakiwa aende 😅
 
Roho mbaya aijengi punguza stress kuna ubaya gani mtu kufurahia siku ya kuzaliwa kila mtu na life style yake me kwa upande wangu siwezi kabisa kusherekea siku ya kuzaliwa lakini na heshim wanao sherekea maisha ya hapa duniani ni mapito so fanya kinacho kupa amani na furaha
Jaribu kwanza kua na akili ya uelewa wa ulichokisoma kabla ya kukurupuka,kuna sehemu nimesema kua kuna ubaya wa mtu kufurahia siku yake ya kuzaliwa? wewe ndio una stress na sio mimi,

Soma tena comment yangu kwa kutulia,zingatia matumizi ya question mark kisha njoo tena hapa kwa heshima na nidhamu.
 
Hongera Kwa kuongeza umri Kuna watu Wana makasiriko wengi wapweke mno hawanaa hta watu wakifurahi nao kwenye vitu kama hivo
 
Back
Top Bottom