Siku ya Vijana wa Afrika-nini utume wetu?

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
713
1,241
Ujumbe wangu wa mshikamano nimeuambatanisha hapa chini. Frantz Fanon aliwahi kusema "Kila kizazi, lazima nje ya uvungu uvungu(obscurity) kiutambue utume wake, ama kiutimize au kiusaliti". Nini utume wa kizazi chetu? Nawatakia maadhimisho mema ya siku ya vijana Afrika.

JJ
 
Attachments

  • Solidarity Message-African Youth Day.pdf
    111.9 KB · Views: 116
Huko nyuma Mike aliwahi kuandika waraka humu http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=4334

Ambao nauweka hapa chini ujadiliwe sambamba na tafakari kuhusu utume wa Vijana:

"Waraka Kwa Wizara ya Vijana:Baraza au Balaa kwa vijana?! [1]

Nakumbuka methali ya Kiswahili isemayo “ukiona mwanaume anapiga kelele ujue ameshikwa pabaya!”Methali hii iliwahi hata kutumiwa na Mhe.Mudhihir Mudhihir ndani ya vikao vya bunge pale alipokuwa anatetea hoja za jimbo lake.

Nimelazimika kuanza na methali hii kutokana na mjadala unaoendelea hivi sasa miongoni mwa vijana mahiri na machachari wanaharakati na wenye mapenzi mema na Taifa letu hili la Tanzania.

Hii ni kutokana na ukimya wa muda mrefu na kufatiwa na tukio lililotokea mnamo tarehe 23 Julai hadi 25 Julai, 2007 huko Jumba la Bandari,Tanga kwa kuitishwa mkutano wa vijana pasi usawa wa uwakilishi hasa kwenye asasi makini zilizokuwa mstari wa mbele katika kushughulikia suala la uharakishwaji wa uundwaji wa Baraza la Vijana na Sera mpya ya vijana ya mwaka 2007.

Kwa baadhi swala la uundwaji wa Baraza la vijana wanaweza kuligeuza na kuliita sasa “sakata la uundwaji wa baraza la vijana” na wapo waliodiriki kufikia kuliita “balaa”.Hii ni kutokana mchakato kuchukua muda mrefu sana na uendeshwaji kwa usiri mkubwa sana pasi walengwa hasa vijana wote wa kitanzania kujua kiunaga ubaga.

Kama wahenga wanenavyo kuwa “aliyeng’atwa na nyoka haishi kushtuka pindi aguswapo na unyasi”, ndivyo hali halisi iliyopo kwa vijana wetu hivi sasa.

Kwani wizara imekuwa ikiitisha mikutano kama hiyo ambayo nashawishika kuiita batili mara kwa mara.Ikumbukwe hata mwaka 1994 na mwaka 2000 iliitisha na kuendelea kuwatenga baadhi ya vijana makini wakiwa katika miamvuli ya asasi za vijana.Kwanini lakini?

Licha ya vijana wa asasi, pia hakukua na uwakilishi toka vyama vya siasa wala taasisi za kidini.Je mfumo gani ulitumika kuwapata wawakilishi? Je wawakilishi walikuwa na ufahamu wa kutosha juu ya mambo waliyokuwa wanaenda kuyajadili? Je wawakilishi walikusanya maoni toka kwa vijana wengine?

Kwani ni miaka takribani 11 sasa tangu vuguvugu la kuomba uanzishwaji wa baraza la vijana lilipoanza yaani mnamo mwaka 1996.Toka kipindi hicho zao lililovunwa licha ya kuwa na ubora wa kiwango cha chini sana lakini angalau likatokea ni Sera ya vijana ya mwaka 1996.

Katika sera hiyo wanaharakati hawakuisusia bali walijitahidi kutoa maono yao juu ya nini kiongezwe kuboresha mambo.Mengi yalipokelewa lakini nashawishika kusema nina mashaka katika utekelezaji wake kwani hakuna madadiliko yoyote yaliyochukuliwa wala kutolewa kwa sera mpya.

Tumeona mabadiliko mengi ya uongozi na ya majina katika wizara husika ya vijana bila mabadiliko kiutendaji.Nakumbuka enzi za Kapuya ambaye pia alitoa ahadi nyingi juu ya uundwaji wa baraza la vijana na sera bora ya vijana ambavyo vyote hakuvitekeleza, akamaliza muda wake sasa amekabidhiwa wizara nyingine nashindwa kuamini kama hata katika wizara nyingine aliyopo atashindwa kuendeleza katabia haka.Astakafilu...lahhi masafa ya Mtume yarabi!

Ikumbukwe katika harakati hizi za uundwaji wa baraza la vijana jambo ambalo si la kuliletea mzaha hata kidogo kwani tumekubali hata kimataifa kwa Tanzania kutia saini katika mkataba wa vijana [African Youth Charter] ikiwa na kipengele cha uundwaji wa baraza la vijana.

Lakini wapo ambao wanaweza kuhoji kwanini hasa kuundwa kwa baraza la vijana, kwani kuna shida gani? Hiyo ni vema kabisa.Historia inatufundisha palikuwapo na Tanzania yenye serikali ya kufuata mfumo wa chama kimoja.TANU na baadae CCM ilikuwa ndiyo chama pekee.Kwa kutambua umuhimu wa chombo kinachowaunganisha vijana kiuhalali ndipo Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi [UVCCM] ukaanzishwa.

Hata baada ya mfumo wa vyama vingi kuruhusiwa mnamo mwaka 1992 bado hakukuundwa chombo kitakacho wakusanya hawa vijana wenye itikadi, falsafa na mitazamo tofauti kufuatana na vyama, dini na taasisi, mbalimbali.

Katika kipindi cha mpito kuelekea 1992 kulikuwa najuhudi za baadhi ya viongozi kuanzisha mashirika yasiyo ya kiserikali ya vijana kupitia makada wa UVCCM ambayo yangechukua majukumu ya UVCCM, juhudi hizi ziliandikwa sana kwenye magazeti wakati huo kwa mfano ulianzishwa Muungano wa Vijana Tanzania [MUVITA] amabao ulisajiliwa na viongozi wake wote walikuwa makada wa UVCCM hata hivyo walishindwa kupata nguvu kwa sababu hawakuweza kupata uwezesho wa kifedha kutoka serikali au kwenye chama kama walivyokuwa wamezoea kwenye UVCCM

Natambua uwepo wa asasi mbalimbali katika nagzi ya mikoa na hata kitaifa zinazowakusanya vijana na kujadili, kutoa uwakilishi lakini bado hazina uhalali kisheria [legitimacy], hivyo kupelekea uwepo wa haja kubwa ya kuundwa na kuhalalishwa kwa baraza huru la vijana ambalo litakuwa chombo na sauti ya vijana wote.

Nakumbuka hoja hii ilishikiwa kidete sana na asasi iliyofutwa ya National Youth Forum [NYF].Lakini kunani hasa kupambana na ukweli? Nasema hivi kwani HakiElimu nayo ilitaka kufanywa NYF.Tumeona TYVA na YUNA iliyoona ni jambo la busara sana uwepo wa baraza la vijana kuichukua na kuendelea kuisambaza kila kona.

Ikumbukwe mnamo tarehe 23 Julai, 2007 TYVA iliitisha mjadala juu ya Uundwaji baraza la vijana na kuhudhuriwa na vijana toka kada mbalimbali, mwakilishi wa wizara akiwemo[jina tunalihifadhi] ambaye alituahidi ushurikiano wakutosha na kushirikishwa katika mchakato mzima wa uzinduzi wa sera ya vijana na uundwaji wa baraza la vijana.Je huu ndiyo ushirikiano hasa wizara uliotoa?

Hapa naukumbuka ujumbe mfupi wa barua pepe ambayo niliupokea na kunipa hamasa kuuweka katika makala hii.Kamaradi mwenzangu alinitumia juu ya sakata hili la baraza la vijana akisema;

“Baraza nilijualo mimi linakuja kuwaweka vijana wote nchini, bila kujali itakadi zao, pamoja katika masuala ya msingi ya kitaifa na maslahi kwa vijana wote. Huu ndio uhuru wetu wa kweli! Baraza linakuwa chombo cha kusimamia matakwa ya vijana na kuwasemea wote. Unatoka wapi ugomvi huu wa kijinga? Hizi ni fikra duni za watu wasio na mapenzi na nchi yao na wenye hila na matakwa binafsi. Hawa ni wachoyo. Kijana wa kweli mwenye mapenzi na nchi yetu hawezi hata siku moja kutamani baraza bovu eti tu ili kukilinda chama chake! Kwani chama hicho ni maslahi ya watu gani?

Hivi leo yafaa nini kuwa na CCM imara yenye kuchukua majimbo yote ya uchaguzi nchini lakini vijana wanalala njaa, hawana ajira, wanakufa kwa UKIMWI na hawawezi kwenda shule? Ni upuuzi. Ina maana gani kuwa na CHADEMA imara yenye nguvu sana lakini maslahi ya vijana hayajashughulikiwa ipasavyo? Ama CUF ama chama kingine chochote. Kwa kweli hakuna maana yoyote. Shabaha yetu ni maslahi ya vijana yazingatiwe na maisha yetu yaboreke. Tamaa yetu ni kuona vijana wanapewa haki zao na wanawezeshwa kuchukua fursa zao za kiuchumi ili wajiendeleze. Tamaa yetu ni kuwaona vijana wanashiriki kikamilifu katika vyombo vya kutoa maamuzi. Mwisho wa siku sisi tunawatazama vijana. Mbona tunasahau na kuangalia mambo madogo?”

Lakini ndugu yangu huyu bado akaendelea kujadili juu ya sakata hili la baraza la vijana kuwa;

“Kijana yeyote makini, bila kujali chama chake cha siasa hawezi kutamani baraza bovu la vijana. Siamini kama imani ya serikali ni kuwavunja vijana nguvu na kuwafukarisha. Hii ni hatari sana na sijui kama ndiyo imani yao . Ni aghali sana kuwafukarisha vijana. Ni bora mara mia kujaribu kudhibiti athari za kisiasa za kuwapa vijana nafasi yao ili tuapambane sawa sawa. Maana tukifukarishwa hatutakuwa na cha kupoteza, tutasema, liwalo na liwe sasa tunapambana kwa mbinu zote. Hii ndiyo hatari ya kukata tamaa na ninamini serikali inalijua hili. Pamoja na ufahamu huu bado wanataka kufanya wanachokifanya? Mama yetu Joyce (Mkurugenzi wa Idara ya Vijana), ana matatizo ya msingi. Nadhani amechoka na anahitaji kupumzika kidogo. Ipo haja ya kuwapa wengine kazi ya vijana. Yaonyesha ama ameshindwa kutuelewa na kuelewa matakwa ya dhati ya vijana ama ameamua kwa makusudi kutenda maovu makubwa yanayoweza kuhatarisha amani ya nchi yetu. Hili halivumiliki. Kama yeye ni timamu hata kama CCM ikimshinikiza kutengeneza baraza bovu hawezi yeye kutengeneza bovu kama hili. Ni upungufu mkubwa wa kiuwezo ama ni uzembe wa hali ya juu sana . Kwa vyovyote vile hakuna maelezo yatakayomtoa katika hili. Kwanini asiwajibike?”.

Nadhani katika makala hii ya kwanza sitamjadili Mama yetu Joyce, lakini naahidi kufanya katika sehemu ya pili ya makala hii.Hata vitabu vitakatifu vinasema “Divai mpya haikai katika kiriba kikuu kuu kwani itakipasua” Ni matumaini yangu Mhe.Nchimbi na Mhe.Chiligati ni divai mpya, je itakuwaje? Itapasuka?

Frantz Fanon aliwahi kusema kila kizazi nje ya uvugu uvugu “obscurity” lazima itambue utume wake na aidha iukubali na kuutekeleza au iusaliti-tafsiri ikiwa ya kwangu.[Every Generation must,out of realtive obscurity discover its mission and either fulfill it or betray it!"].Je vijana tupo tayari kuukataa kupigania uanzishwaji wa baraza huru la vijana ambalo litakuwa na nguvu ya kutoa sauti halisi ya vijana kwa maslahi ya Taifa zima?"
 
inalekea una njaa ya madaraka wewe Mnyika ! baraza la vijana wakati hilo tulilokuwa nalo mnasema ni kubwa, sasa hilo unalosemea wewe ni nini ?

mie napinga bana, tena sitaki kusikia ! Maana i dont see no possible way you can convince thoroughly and support your statement using your own THINKING to support your hoja ! Kutumia mifano ya nani sijui kasema nini that will ONLY mean you support their idea, lakini you didnt dig in deep kuona athari zake ! will you be responsible for the repercusions if any will arise ??

gharama zitaongezeka, na kwa nini kila mtu akimbilie kwenye siasa bana, kuna kazi kibao za akitekcha, konstraksheni, unaweza ukakimbilia huko na sio kwenye siasa mkuu, wanasiasa ni wengi mno na wanatuumiza vichwa sasa mkiongezeka si mtatuumiza hadi viwiliwili !

Kila kijana akikimbilia kwenye siasa, mashamba ya mpunga kule tunamuachia nani ? hatuhitaji viongozi wengi ku-overcome matatizo ya taifa letu FYI !!
 
inalekea una njaa ya madaraka wewe Mnyika ! baraza la vijana wakati hilo tulilokuwa nalo mnasema ni kubwa, sasa hilo unalosemea wewe ni nini ?

mie napinga bana, tena sitaki kusikia ! Maana i dont see no possible way you can convince thoroughly and support your statement using your own THINKING to support your hoja !

gharama zitaongezeka, na kwa nini kila mtu akimbilie kwenye siasa bana, kuna kazi kibao za akitekcha, konstraksheni, unaweza ukakimbilia huko na sio kwenye siasa mkuu, wanasiasa ni wengi mno na wanatuumiza vichwa sasa mkiongezeka si mtatuumiza hadi viwiliwili !

Soma kabla ya kujibu. Tanzania haina baraza la Vijana. Na baraza la vijana si chombo cha wanasiasa. Ni chombo cha kuwaunganisha vijana wote bila kujali itikadi ya vyama. Anyway, tuiache hiyo hoja ya baraza. Sijaandika mimi, ameandika Mike.

Mimi nimeandika kuhusu siku ya vijana Afrika- nataka tutafakari; utume wa kizazi kipya ni upi? Je, tunautimiza?

Mje, mkataba wa vijana Afrika unasemaje? Kwa nini mpaka sasa haujaridhiwa na Bunge letu tukufu ingawa Kikwete alishatia saini kule Banjul mwaka jana?

JJ
 
paragrafu ya mwisho sijakuelewa ulichosema ! baraza la vijana nasajesti liwe ONLINE kama JF tu !

Itakuwa vizuri kabisa kama tukiona vijana wetu wachapakazi, wakiongelea teknolojia mpya za kuvuna mpunga, viazi,mananasi yanayooza tanga, nyanya zinazooza iringa, !

Tunahitaji sana wakulima kuwa na maisha bora,
hatuhitaji sana wanasiasa kuwa na maisha bora !

Ushauri kwako Mnyika: Kama utaweza kulima gunia moja la mpunga, au viazi utakuwa umesaidia vijana wengi sana kwa kweli, sasa imagine kijana mchapakazai kama wewe unaweza kulima magunia mangapi ?
 
Kada:

Baraza la Vijana litajumuisha vijana wanaolima mpunga na hata hao wanaojadili teknolojia mpya!

Wanasiasa nao ni muhimu kwa kuwa wakulima wanalima sana lakini wanasiasa wameshindwa kuweka mazingira bora ya kisera na kifedha yenye kuwezesha barabara kujengwa mazao kusafirishwa masoko kupatikana ama walau viwanda vya usindikaji. Wanajenga Twin towers badala ya Viwanda. Wananunua Gulf Stream JET badala ya Matrekta, wanakwenda kuleta Mvua Thailand badala ya kuboresha kilimo cha umwagiliaji.

Nililima sana nilipokuwa Maua Seminary na kugundua adha ya kilimo cha Jembe la Mkono; kwa nnachofanya sasa nawasaidia wakulima wengi zaidi!

Tuendelee kujadili utume wa kizazi chetu; soma ujumbe wangu kwenye kiambatanisho 'Solidarity Message', utanielewa!

JJ
 
hicho unachoongelea wewe ni kitu ambacho kitaleta mifarakano mikubwa sana hapo mbeleni, yaani itakuwa kama "YOUTH AWAKENING" hapo ndipo wengi watamwaga damu ovyo sana, and we dont want that to happen, ! angalia sana unachozungumzia in deep Mnyika !

Ninaamini maendeleo yataletwa pale vijana wataamua kujishughulisha kivitendo na sio kupiga zogo kila saa, mtu kama Mwanakijiji naamini muda aliokuwa nao kwenye net, angeweza kila siku kuzalisha magunia hata 70 ya viazi mbatata, na wengine waliopo kwenye trupu lake hata magunia 50 wangezalisha each !

"YOUTH AWAKENING" will affect so much, and cause distraction and misplacement of important things in our young, growing nation !
tuanzeni kwanza kulima siasa baadae !
 
Hii ilikuwa Jamiiforums, vichwa vya kufa mtu!
 
Back
Top Bottom