Siku ya uzinduzi wa jiji la Arusha-Wakazi wa Arusha hawapendi Bongoflava wanapenda Hip hop | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku ya uzinduzi wa jiji la Arusha-Wakazi wa Arusha hawapendi Bongoflava wanapenda Hip hop

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by lengijave, Oct 31, 2012.

 1. l

  lengijave Senior Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna taarifa nimezipata kuwa kesho tarehe 01.11.2012 jiji la Arusha linazinduliwa rasmi na hivyo wameamua kuwaleta baadhi ya wasanii wa bongo flava kwa ajili ya kuburudisha wakazi wa Arusha,na kujaza uwanja ili Rais isiwe mpweke

  Kwanza kabisa ningependa kuwashauri wadau wote kuwa wakazi wa mji wa Arusha hawapendi mziki wa bongo flava ila wanapenda hip hop,kwa hiyo hata ukimleta Diamond kwa bure bado hawata mpenda na kwa sababu wameamua hivyo ni bora basi wamuekee diamond ulinzi mkali kama wa kiongozi sababu watu wanaweza kweli kwenda uwanjani lkn si kwa sababu ya kucheza muziki ila ni kwa ajili ya kumtukana

  Pili kwa msiofahamu Arusha kuna wasanii wa hip hop wenye uwezo mkubwa kati ya 100 - 1000,na studio mbalimbali ambazo kwa muda wa miaka 10-20 wanarekodi hip hop tu hawataki miziki ambayo haina hisia ya ukombozi

  Tatu mwaka 2012 fiesta ilishindwa kufanyika arusha,unaweza kujiuliza ni nini hasa iliwafanya watu wa fiesta waliokuwa wanagawa hata magari lkn walishindwa kufanya onyesho-kunaweza kuwa na sababu mbalimbali lkn aina ya wasanii ambao clouds wanapata maslahi hawakubaliki Arusha,unafikiri kama Diamond angevua nguo Arusha!!watu wangemuelewa kweli,

  Pamoja na maamuzi yote ya TZ goverment kuamua kufanya hivyo bado wananchi wa Arusha tutaendele kupenda hip hop,Kwa mnaofuatilia Hip hop naomba leo muangalie kazi nzuri mpya ya JOH MAKINI - SIJUTII video ambayo imeachiwa jana usiku kwenye you tube angalia pia ubora wa producer kutoka Arusha Nisher aliye andaa video
   
 2. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii ni kweli kiasi flani, ila vijana wa kiume zaidi ndo wanapenda hizo hip hop wasichana wanapenda hawa bana pua kama Diamond watu wazima wako neutral hawana time sana na muziki.
   
 3. Wimbo

  Wimbo JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 23, 2012
  Messages: 376
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kipindi cha sasa usipime na wakati wa Azimio la Arusha, Jakaya atakuwa na watumishi wake wa Manispaa wanaotamani kuwa Jiji, na wanafunzi watakaokwenda huko kwa tishio la rollcall, watu sasa hivi wanakimbizana na ugumu wa maisha wewe unaleta za ubongo wa freva! hata kama angekuwa Pepe kale aliyesahau Arusha mkanda wa kiuno wala wasingestuka.
   
Loading...