Siku ya ukimwi duniani

Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
10,270
8,031
SALA YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

Mungu Baba Yetu

Katika siku hii ya UKIMWI Duniani tunakuja kwako na kila kitu kinacho tuponda ponda na kutusukuma

Tunakuomba:
Uwe pamoja na wanao na binti wote wanaoishi na VVU na UKIMWI.
Watoto wamekuwa yatima, wanawake wamekuwa wajane.
Vizazi vinatoweka. Mungu, utupe nguvu ya kukabili wimbi la UKIMWI katika
upana na ukubwa wake.

Tuinue juu ili tuweze kwenda ulimwenguni na kupambana dhidi ya UKIMWI
na ubaguzi na unyanyapaa wenye jeuri kubwa kwa wale walioathirika.

Tusaidie kukabiliana na kujitangazia haki kwetu binafsi na mawazo yetu yasiyo sahihi kuhusu VVU na wale walioambukizwa.

Fungua mioyo yetu kwa ajili ya mabadiliko na upatanisho. Katika wema wako Mungu wape mapumziko wale waliofariki kutokana na Ukimwi, na wale wanaoishi na na VVU.

Amina.
 
Ewe Mwenyezi Mungu, wape ujasiri wanasayansi waweze kugundua kinga thabiti ya gonjwa hili, tulitokomeze kabisa duniani. Uwalaze pahala pema peponi wote waliotangulia mbele ya haki.

AMIN
 
Eee Mungu muumba mbingu na nchi, nisaidie mimi na rafiki zangu tuzishinde nafsi zetu, tuchukie VVU na UKIMWI lakini tuwapende ndugu zetu wanaoishi na VVU/UKIMWI,tuwaheshimu watu wanaojitngaza waziwazi kuwa wanaishi na VVU kwani kwa kufanya hivyo wanasaidia kupunguza maambukizi mapya. Yasaidie macho yangu yanayowatazama wadada warembo na kusababisha niwatamani isvyo pasa, nisaidie nikupende wewe zaidi kuliko kuipenda dunia na mabo yaliyo katika dunia.Nisaidie kumfanya mke wangu kuwa rafiki yangu wa karibu na nione fahari ya kuwa naye pekee yake katika maisha yangu.Zaidi sana nifanye fahari yangu iwe katika kukupenda wewe kuliko kuona fahari juu ya idadi ya wanawake niliowamega. Mafanikio yangu yasiwe katika elimu na mali pekee yake, bali yawe katika kujenga familia yenye furaha na umoja.

Ninamuombea mdogo wangu nayeishi na VVU na anawaambukiza wasichana wadogo hasa wa vyuo vikuu kwa vipesa vyake vidogo aache kujichukia na kuchukia watu wengine, atambue upendo wako Mungu naye awapende watu wengine na asiendelee kuwaambukiza kwa kusudi.

Naomba haya kwa imani kupitia jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, Amen.
 
AAmin mungu asikie sala zenu...
Tusiwanyanyapae eee
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom