Siku ya Mtoto Njiti Duniani

Wild Flower

JF-Expert Member
Jul 20, 2023
338
704
Kila Novemba 17, Siku ya Mtoto Njiti huadhimishwa Duniani ili kuongeza uelewa na kupaza sauti kuhusu changamoto zinazohusiana na suala hilo

Mtoto njiti huzaliwa kabla ya wiki 37 za Ujauzito kukamilika

Mtoto mmoja kati ya kila Watoto 10 huzaliwa Njiti na kila mtoto anayezaliwa chini ya uzito wa kilo 2.5 huwekwa kwenye kundi la Mtoto Njiti

Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti Duniani Novemba 16, 2024 Daktari bingwa wa watoto Dkt. Albert Chotta amesema licha ya Serikali kuweka jitihada katika kuboresha miundombinu ya utoaji wa huduma kwa watoto njiti ni wakati serikali ijitahidi kuweka muuguzi mmoja kwa ajili ya kumhudumia mtoto njiti mmoja

Pia, taasisi ya Doris Mollel Foundation iliyoa semina na mafunzo kwa baadhi ya Waandishi wa Habari kwa lengo la kutoa mafunzo ya uandishi wa habari za watoto njiti kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mtoto njiti duniani

Aidha taasisi ilizindua mtandao wa kidigitali kwa wazazi wa watoto njiti kwa lengo la kutoa mafunzo ya jinsi ya kulea mtoto njiti ili kukabiliana na vifo vya watoto njiti nchini
 
Back
Top Bottom