nkulikwa
JF-Expert Member
- Jul 21, 2015
- 721
- 813
Pamoja na kunyonywa kwa kodi nyingi sana kuanzia PAYE mpka VAT bila kusahau loans board ambayo wengine wanaona ni harali kulipa 15% ambayo makubaliano yalikuwa ni 8% bado siku ya mei Mosi watabeba mabango na kupigwa na mvua au jua kusilikiza hotuba za matumaini! Tumejifanya wanyonge, tumepuuzwa na vyama vyetu na kuwa shamba la mavuno. Hadi fedha unayokatwa umewekewa masharti na wenye nguvu utalipwa ukiwa mzee utadhani una ahadi na kifo. Hata utakapokuwa mzee akili hupungua na watoto wako ambayo wangesoma kwa fedha uliokatwa watakuwa wamechukua nafasi ya umaskini wako. Kizazi hadi kizazi maisha Yao ni mzungumko wa ufukara.