Siku ya mashujaa tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku ya mashujaa tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kajukeg, Jul 26, 2010.

 1. kajukeg

  kajukeg Member

  #1
  Jul 26, 2010
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapendwa wana jamvi jana ilikuwa ni siku ya mashujaa wa tanzania,kila mtanzania mwenye damu ya kitanzania alikuwa na fursa ya kukumbuka watu muhimu waliolipigania taifa letu kiasi cha hata kupoteza maisha yao.
  nilikuwa nasikiliza hotuba ya mkuu wa inchi wa wakati ule hayati baba wa taifa mwl nyerere alioitowa wakati akilihutubia taifa kwenye uwanja wa taifa dar ktk siku ya mashujaa mwaka 1979.
  moja kati nukuu zake muhimu ambazo zimepelekea mimi kuguswa na kuandika ujumbe huu ni hii; nanukuu,
  "Katika vita hii kuna wengine wamerudi wengine hawakurudi,wengine wamerudi na majerha makubwa ambayo wengi wao wametibiwa na wamepona na wamerudi majumbani mwao lakini wengine wamepata vilema vya maisha hawatapona kabisa,hivyo jukumu la maisha yao ya baadaye ni jukumu letu.na wale ambao hawakurudi kabisa mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu mahali pema,tunatoa pole kwa ndugu wa marehemu mana huzuni yao ni yetu pia na msiba wao ni wetu pia na jukumu la maisha yao ya baadae ni jukumu letu" mwisho wa kunukuu.
  swali langu linakuja hapo ni kweli kwamba waathirika hawa waliopata vilema vya maisha pamoja na ndugu wa waliopoteza maisha ktk vita hivyo bado wanahudumiwa ipasavyo mpaka leo na serikali yetu,ama kauli ile ya mwl iliishia siku ilelile pale uwanja wa taifa? ama wahusika wote hawapo tena duniani,ama ndo ukweli wa usemi usemao ' waache wafu wawazike wafu wenzao ndo unaendelea'

  Tujadili ndugu zangu.
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,062
  Likes Received: 24,061
  Trophy Points: 280
  Hivi ilikuwa jana? Ingekuwa leo ingekuwa raha.......mambo ya long weekend! BTW siku ya mashujaa ni mapumziko? Sikumbuki vema!
   
 3. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 522
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Tanzania ya Nyerere siyo Tanzania ya Kikwete, waulize wale wazee waliokuwa East African Communite watakuambia, haki ya hao wahanga ilikwenda na Mwalimu siku anazikwa,
   
Loading...