Siku ya kwanza kufika Sinza nilitokwa na machozi sana

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Ilikuwa miaka ya nyuma hivi Mzazi katwambia tuje kutembea afrika hasa hasa TZ. Tukaja.tukafikia nyumba yake mojawapo katika zile tatu za Oysterbay. Maana tuliona kwenda kukaa moja kwa moja Upanga tutakosa uhuru.labda tukae ile ya upanga east.maana zile nyumba nazo tukiwa kule tunabanwa sana tumezungukwa na wazungu tu.

Ikawa sometime tunalala obay au tunenda Upanga.maana sisi tulikuwa tunapenda sana ya Obay sababu ilikuwa ni Ufukweni kabisa. Tulikuja na rafiki zetu watoto wa kizungu hawa tulizunguka sana wao walitupeleka canada,sweden,uk,usa na russia.

Sisi tukawaleta egypt,south africa,botswana na tanzania.wakataka tukanunue vinyago pale mwenge.basi mzee akasema zitumike gari mbili benzi nyeusi na nyingine ya kijivu.miaka hiyo ndo zimetoka toka tu.

Basi hao mpaka mwenge.tukawa tunashangaa yale maisha ya wale jamaa.ndo dereva akasema twendeni mpaka sinza mpafahamu.

Daah...siku hiyo nlishangaa kumbe kuna watanzania maskini sana.nikawa nawaza hawa jamaa wanaishije?nyumba zimebanan ile mbaya.hata wanaweza kupumua kweli.nlitokwa na machozi ya huruma sinza yote imejaa watu maskini.

Dereva aliona tulivyoshangaa naye akawa anashangaa maana alisema kule ndo wanaishi watu wenye kipato cha juu.hapo tukajua dereva anatuona sisi wakuja sana.anatuona sisi mafala.sinza imechoka yeye anasema ndo watu mambo safi.

Sasa jana kuna jamaa yangu ofisini akanambia anataka kuoa nikamuuliza sasa utaenda ishi wapi maana kwa sasa anaishi Mbezi beach.akanambia eti amepata nyumba ya kupanga Sinza.nlishtuka sana.kumuuliza tsh ngapi anasema 900,000. Kwa mwezi.

Unajua nlimuuliza mara mbili..what?unawezaje kwenda ushi sinza na mtoto mzuri kama unayetaka mwoa?sinza eneo la watu waliochoka.hiyo nyumba ya laki tisa kwa mwezi ni nyumba au banda la kufugia kuku?

Jamaa ndo akasema basi ngoja nitafute mikocheni.nmemshauri asioe kwenda mtesa mtoto wa watu.akatafute apartment hata za bei rahisi oysterbay atapata kwa Mil 3 - 5 kwa mwezi.kuliko kwenda ishi na mke uswahilini kama sinza.

Nikawaza jamaa ndo katoka kununua kigari chake prado mayai ya mwaka 2017 baada ya mimi kumponda kuwa anawezaje endesha harrier ya mwaka 2014 si itakuwa imesha expire.ndo kununua hiyo prado na nikamwambia angalau basi hata anunue na gari za ukweli toka Ulaya au Marekani.

Vijana huwa nawashauri usioe kama hujajipanga.maana namuuliza jamaa yangu. Ok unaoa una tsh ngap bank kama akiba... Huwezi amini ananambia mil 27.5 guys why mnakosa umakini?mil 27.5 unataka kuoa?ili iweje?umtese mtoto wa watu? Maana hamna kitu hapo.

Mimi nasema mpaka nikishe angalau Bil 1+ ndo sasa nione huku issues zangu zikiwa zimesimama. Mtu analipwa salary mil 6.7 take home anataka aoe.ili iweje?ni kuchuma dhambi tu.bint hatoweza pata mahitaji yake.

Mimi nlianza kazi nalipwa pesa kidogo sana mil 27 baada ya makato.nikasema huu ujinga nlifanya miezi mitano nikaacha. Nikaja kuajiriwa nalipa mil 43.nkasema hapa niangalie angalie pakoje. Sasa hivi si mbaya sana.nanunua gari zinasoma 0km au less than 10,000 kms.

Mimi sinunui gari ime expire.yaani gari imetoka miaka 5 ago? Hiyo expired mimi nachukua kitu mwaka huo huo au si zaidi ya 2years.

Hivi jamaa yangu mmoja ananishauri sababu napenda magari basi kwenye store yangu ninunue na Land Cruiser V8 Kilimo kwanza. Nawaza hizi gari si zipo nyingi sana? Mnaweza hata jikuta mnachukuliana magari.nimeulizia Nissain V8 mpya wanasema mil 400. Nikasema hii ndo machine sasa.

Anyway maisha yanabadilika sana ila tujipange pesa zipo acheni kulalamika tu watanzania...mimi mshahara sigusi kabisa...ila si haba kudondosha dondosha tu lakh kadhaa kwa siku hainipi shida.

Nliuliza kama kuna mtu mtaalamu wa kuchoma nyama.... Ntampa lakh 450,000 kwa siku. Kama atakuwa tayari aseme nitume mtu wa kuja mchukua. Maana kuna gari moja VW hii ndo sasa naona iwe ya kubebea watu kama taxi.

Najua kuna watu mtakasirika.mi huwa nashangaa.nikisema jamani sijala au nina maisha màgumu mnaamini kirahisi sana.ila sisi ambao tulivuka poverty line toka hatujazaliwa mnaona kama tunajidai.huo ni unyanyasaji.maskini anaruhusiwa kujisifia umaskini wake. Akiongea mtu mwenye vijicent kidogo inakuwa issue na kujenga chuki.
 
Back
Top Bottom