Siku si nyingi serikali ya CCM itarudisha utaratibu wa shughuli za Bunge kuonyeshwa moja kwa moja

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,694
149,920
Ninaamini mpaka sasa serikali hii ya CCM imegundua kuwa imefanya kosa kubwa kusitisha urushwaji wa shughuli za vikao vya Bunge moja kwa moja japo hawawezi ku-admit kosa hilo hadharani na badala yake watatumia mbinu yoyote kurudisha matangazo hayo ya moja kwa moja.

Katika kujirudi,watakuja na kauli za ajabu ajabu za kujikosha ambazo zitawashangaza na kuwaacha wengi midomo wazi ili mradi tu wajirejekebishe.

Ndugu zangu hayo yakitokea kama ninavyotabiri hapa,ndio wengine tutajikuta tunakumbuka soma la historia kuhusu kile kinachoitwa "human evolution" na hapa zaidi ni kuhusu "brain evolution".Sitafafanua zaidi mwenye kuelewa ataelewa.

Hivyo basi,msije kushangaa hawa hawa wanaotoa matamko na kuwaponda UKAWA mitandaoni na katika vyombo mbalimbali vya habari,wakawa wa kwanza kusifia uamuzi huo na bila aibu watasema sasa UKAWA watakosa hoja!

Tusubiri.
 
hawawwzi kuonesha hawa maccm kwasababu kama unakumbuka swala la ESCROW lilivyojadiliwa laivu na raia waliona na kupata mwanga jinsi mambo yanavyoendelea serikalini. Baada ya siku chache tu ulikuja uchaguzi wa serikali za mitaa hapo bdipo ccm ilichapika.raia wanaingia kwenye uchaguzi bado wana hasira za escrow...wamejifunza.hawataonesha laivu tena.
 
Endelea kuota maana, sisi wengine hatuna haja ya kuona sarakasi huko bungeni, tunahitaji bunge lenye tija sio bunge la vioja...
 
Tumewatuma tungependa tujue wanatusemea nini? Na wanajibiwa nini? Kama watawasema wezi kwanini iwe sirini si walituibia sisi. Hivi unaweza ukaibiwa na usiambiwe mwizi wako ni nani?
 
Narudia tena, sh. b'400 zinapotea kwenye foleni Dar + sh. b'4 za bunge live + thamani ya masaa kazi yanapotea nchi nzima kwa kuangalia bunge live. Jambo hili halikubaliki kwa nchi changa kama Tz. Naunga mkono hatua za serikali kuondoa hasara hii.
 
Wananchi hawahitaji kusikia vimbwanga vya kina kubenea vya kuongelea shanga....Kuna Mengi ya kufanya zaidi ya hili
Muovu akisha fanya uovu wake hubaki na kazi moja tu ya kuficha uovu wake-sujui nyinyi mko wapi hapo.
 
Movu akisha fanya uovu wake hubaki na kazi moja tu ya kuficha uovu wake-sujui nyinyi mko wapi hapo.
Tunajua nia ya mafisadi kujikosha kupitia matamko na kelele bungeni badala ya kujadili maendeleo ya wananchi
 
Halafu ni kitu rahisi sana, ni mh. Mzee wa kuchapa watu bakora aaguze kimya kimya kamera ziingie na kurusha live hata bila kutoa taarifa yeyote. Maisha yanasonga.
 
Kupata habari ni haki ya Msingi na ipo kwenye katibap. Ipo siku mhe. Magufuli atasema yatosha na wale wasiojua haki zao watashangaa kama walivyoshangaa alipozuia Safari za nje wakampongeza kwa aibu.
 
Ndugu yangu, Mwana Fasihi Emmanuel Mbogo katika moja ya Kazi zake anasimuli:
".....alikuwa kavaa gunia refu,pana la mama yake, nywele zake timtim, miguu anapekua. Alibweka: Wuu! Wuuu! Wuuu!....alizoa mchanga akajimwagia kichwani...sura yake ilibadilika. Ikawa INATISHA. Inachekesha. Hadira yake ikaangua vicheko."heeee! heee! Hoooo! Leoooo mambooo leoooo!
Zita akapiga magoti.Akaanza kutembea kwa miguu minnne kama mbwa. "Wuuuu.Wuuuu. Mnajua? Mimi Bobi. Ntawala. Aliwatisha watu kama vile anataka kuwang'wenya..."
My take: Haya ndo naona CCCCCm inafanya......
 
nadhani ni vizuri wabunge wetu wanapochangia hoja kujua kuwa audience yao ni kuanzia asie na elimu hadi professor wa chuo kikuu, nafikiri kama ni kweli waheshimiwa waliyasema yale niliyosoma kwa magazeti ya leo, basi kwa mtazamo wangu hawastahili kuwa wabunge! na nchi yetu itabaki mkiani milele!
Ndugu, wengine hatukusoma gazeti unalolisoma. Lina ujumbe gani HASA kuhusu hawa Wabunge?
 
Endelea kuota maana, sisi wengine hatuna haja ya kuona sarakasi huko bungeni, tunahitaji bunge lenye tija sio bunge la vioja...

Nani atakuwa anaruka sarakasi usizotaka kuziona ndugu Stroke?

PM Majaliwa? mawaziri wakiwasilisha bajeti zao? Spika Job Ndugai au Bi Kidude, Tulia Ackson?

Nani? Kina nani mkubwa? Kina nani hao waruka sarakasi?.....Hebu waorodheshe hapa bwana alaaah....!!??
 
Inawezekana makarudisha kweli kwa maana hata huyo mzee wa Kuwait mwenyewe ukimwuliza sababu za kuzuia bunge kuoneshwa live, hazijui. MaCCM yamekabidhi akili kwa wale fisi waliokuwa wanatembea nao na wametokomea nazo mbugani.
 
Back
Top Bottom