Habari zenu za mchana wapendwa,
Natumai nyote hamjambo, kwa wale tunaowasiliana PM na nje ya JF nimekuwa hafifu kwenye mawasiliano kwa wiki mbili hizi kutokana na mambo kadha wa kadha hayo ni pamoja na majukumu yanayonikabili. Kama ulidhani nimechuna makusudi basi uelewe si hivyo.... ni ngija ngija za ndima.
Katikati ya majukumu nikapatwa na tafakuri, humu JF tumezoea kuona ID imepotea haichapishi tena wengine wakiwa wamejitoa mazima wengine wamefungua ID mpya wengine albadani wametutoka kwenye dunia hii.
Pia tumeshuhudia mara kadhaa watu wakileta mrejesho humu kuwa flani kafiwa na mtu wake wa karibu au mwana jamii mwenzetu amepata ajali au amelazwa anaumwa na saa nyingine kuwa mwanajamii mwenzetu ametutoka.
Tafakuri iliniuliza, hivi Kasie siku ukiaga dunia, kuna atakayejua humu JF? Kuna atayekuja kutoa taarifa au mrejesho kuwa kigagula Katie kavuta kamba....???!!
Je, wewe ulishajiuliza siku ukirudisha namba, kuna wanajamii humu wataojua na kuja kutoa taarifa? Taarifa tuu na si michango tafadhali. Je, wafikiri nani atayekuja kuleta taarifa zako humu?
Binafsi sina mahsusi wa kuleta mrejesho wangu humu, labda kama mpiga picha maarufu wa zamani aka
Tyta bado yupo ndo ataweza leta mrejesho wangu siku nikirudisha namba kwa muumba. Maana huyu ndo alijitolea kunishushushu bila kunitaarifu maji yalipomzidi kimo akakimbia kusikojulikana na hatukuwa tumemalizana ugomvi wetu just like
Watu8..... hehehehheee don't get suprised, kesi ya muuza matunda haijaisha.....
Asante Bw. Mtwango kwa kunitumia huu wimbo nikiwa napata mlo wa mchana.
Ni tafakuri tuu, as simple as that. Nothing complicated.
Kasie Mahaba Matata.