Mdakuzi mkuu
JF-Expert Member
- Dec 27, 2016
- 212
- 720
Hatari sana.
Mwaka 2008 nikiwa nasoma Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) kampasi ya Mazimbu,na wakati huo nilikuwa nakaa chumba Na. 04 Hostel 5 kitanda cha chini.
Siku moja kipindi cha mvua nikiwa nimelala na umeme ukawa unasumbua sana (unakatika mpk siku 3 hadi 4), usingizi ukakatika usiku wa manane nikasema nijigeuze kitandani (nilikuwa nimelala chali).
Ghafla nikaona mkono wangu wa kulia umekuwa mzito, mkono ambao ndo nilitaka kuvuta blanketi nijifunike vzr. Nilipoushika kwa kutumia mkono wangu wa kushoto, nikahisi kitu laini kipo juu ya mkono wangu.
Akili ya haraka ikaja, nikalabua chini hicho kitu kilichokuwa kimenilalia mkononi.La hasha!!! Alikuwa nyoka (wa wastani),ambaye alijibanza kupata joto kipindi hicho cha baridi.
Nilipomrusha tu,nikasikia kishindo "puu..".Dah.
Nikawaamsha wenzangu.Shida ikawa kushuka kitandani na kunyata mpk switch ilipo, na wakati huohuo nyoka akawa amepaniki,anatoa sauti km ya mawimbi baharini.
Rafk yangu aliyekuwa juu akafanikiwa kuiwasha taa aisee!!!bonge ya joka jeusi.
Tukamsurubu,Mungu mkubwa.
SUA-Mazimbu na majoka meusi,akuu!