Siku mbili za Halima Mdee rumande Oysterbay

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
894
Reaction score
994
SIKU MBILI ZA HALIMA MDEE RUMANDE OYSTERBAY
Usiku wa kuamkia leo tarehe 6 Julai, 2017 ni usiku wa pili wa kulala korokoroni Mwenyekiti wa BAWACHA taifa, Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa Kawe CHADEMA Halima James Mdee.

Katika rumande ya Polisi Oysterbay wilayani Kinondoni, Mdee ameendelea kutumikia masaa 48 aliyopewa na Mkuu wa Awilaya ya Kinondoni Ally Hapi kwa kosa la kumdhihaki Mh. Rais Dr. John Magufuli na kutoa maneno machafu yanayoweza kuvunja amani.

MATAMSHI YA MDEE
Akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya CHADEMA Mdee ananukuliwa kudai kuwa Mh. Rais Magufuli amekua na "tabia ya hovyo...", "...ipo siku ataagiza watanzania (wake kwa waume) watembee vifua wazi...". Maneno mengine ni "...Rais lazima afungwe breki...",apewe semina elekezi n.k.

UCHOCHEZI
Halima Mdee anatajwa kutoa kauli za uchochezi kama vile "...woga wetu wananchi ndio unaotugharimu nchi hii..." "...watakaomfunga breki ni nyinyi wananchi...", maneno yanayotajwa kupandikiza na kuhamasisha chuki na vurugu kwa wananchi.

KUKAMATWA KWAKE
Baada ya amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mdee alianza harakati za kutoroka na kuruka mtego wa Polisi. Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni lilimkamata akiwa amejificha nyumbani kwa mama yake Kibamba wilayani Ubungo tayari kwa kutoroka.

RUMANDE
Halima Mdee anatajwa kuhifadhiwa katika rumande ya watuhumiwa wa uhalifu wa jinsia ya kike katika kituo cha Oysterbay Kinondoni.

BUNGE KUMUWAJIBISHA TENA
Akiwa bado anatumikia kifungo cha kutohudhuria Bunge hadi mwaka 2018, Halima Mdee ameingia tena matatani.

Kufuatia matamshi ya Mdee na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chadema, Spika wa Bunge Job Ndugai ameagiza kamati ya Kinga na Madaraka ya Bunge kukutana haraka kujadili kitendo cha Mbunge huyo kutoa matashi ya kulifedhehesha Bunge. Akikutwa na hatia huenda akaongezewa adhabu nyingine.
 
Halima Mdee lazima abadilike, watanzania sasa hivi hatutaki siasa za chuki. Hata kama Rais anakosea, kuna njia nzuri za kumpinga lakini sio kama wabunge wengi wa upinzani wanavyofanya.

Ila Mtukufu Rais na Spika wabaki hivyo hivyo?

Una uwezo wa kujibu kila hoja inayoelekezwa kwako? ila wenzio wakikujibu ni wachochezi?

Safari bado ni ndefu sana, ila tutafika
 
Why always you my young brother? Unafurahishwa na unachokifanya? I feel sorry for you
 
Kwenye hayo maneno ya Mdee ni wapi alipomdhihaki Rais?
tafsiri ya dhihaka, chuki, matusi, uchochezi na chochote kibaya ni kwa mujibu wa mkulu tu na kaumu yake. nadhani sasa hivi ni mwendo wa 'Uko na mimi ama dhidi ya mimi'. Usishangae ukasifia lakini kwa vile tu mwenye madaraka 'hakupendi' ukashtumiwa kwa dhihaka.
 
Halima Mdee lazima abadilike, watanzania sasa hivi hatutaki siasa za chuki. Hata kama Rais anakosea, kuna njia nzuri za kumpinga lakini sio kama wabunge wengi wa upinzani wanavyofanya.

Na ' Mwanamume ' anawanyoosha kweli.
 
SIKU MBILI ZA HALIMA MDEE RUMANDE OYSTERBAY
Usiku wa kuamkia leo tarehe 6 Julai, 2017 ni usiku wa pili wa kulala korokoroni Mwenyekiti wa BAWACHA taifa, Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa Kawe CHADEMA Halima James Mdee.

Katika rumande ya Polisi Oysterbay wilayani Kinondoni, Mdee ameendelea kutumikia masaa 48 aliyopewa na Mkuu wa Awilaya ya Kinondoni Ally Hapi kwa kosa la kumdhihaki Mh. Rais Dr. John Magufuli na kutoa maneno machafu yanayoweza kuvunja amani.

MATAMSHI YA MDEE
Akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya CHADEMA Mdee ananukuliwa kudai kuwa Mh. Rais Magufuli amekua na "tabia ya hovyo...", "...ipo siku ataagiza watanzania (wake kwa waume) watembee vifua wazi...". Maneno mengine ni "...Rais lazima afungwe breki...",apewe semina elekezi n.k.

UCHOCHEZI
Halima Mdee anatajwa kutoa kauli za uchochezi kama vile "...woga wetu wananchi ndio unaotugharimu nchi hii..." "...watakaomfunga breki ni nyinyi wananchi...", maneno yanayotajwa kupandikiza na kuhamasisha chuki na vurugu kwa wananchi.

KUKAMATWA KWAKE
Baada ya amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mdee alianza harakati za kutoroka na kuruka mtego wa Polisi. Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni lilimkamata akiwa amejificha nyumbani kwa mama yake Kibamba wilayani Ubungo tayari kwa kutoroka.

RUMANDE
Halima Mdee anatajwa kuhifadhiwa katika rumande ya watuhumiwa wa uhalifu wa jinsia ya kike katika kituo cha Oysterbay Kinondoni.

BUNGE KUMUWAJIBISHA TENA
Akiwa bado anatumikia kifungo cha kutohudhuria Bunge hadi mwaka 2018, Halima Mdee ameingia tena matatani.

Kufuatia matamshi ya Mdee na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chadema, Spika wa Bunge Job Ndugai ameagiza kamati ya Kinga na Madaraka ya Bunge kukutana haraka kujadili kitendo cha Mbunge huyo kutoa matashi ya kulifedhehesha Bunge. Akikutwa na hatia huenda akaongezewa adhabu nyingine.
Umeweka mtiririko mzuri na binafsi sikujua kama alikamatiwa kwa mama yake na kitendo cha kuwa kwa mama yake ni namna mojawapo ya kutaka kutororka.
Jambo moja ni wazi nalo ni kuwa kila mtu anataka kumfurahisha Mheshimiwa Raisi kwa kadri inavyowezekana.Wateule wote wameshasoma ni kitu gani ambacho aliyewateua anataka na wanaitumia nafasi hiyo kiukamilifu,ni jambo jema kwani wanajihakikishia kula kwao na wapendwa wao.
Mkuu wa wilaya ametumia mamlaka yake kikatiba na tunaamini saa 48 zitaisha na atatoka sasa tuangalie huyu wa Dodoma naye kimemuumiza nini?Hivi kweli kwa matamshi hayo ukilinganisha na yule aliyesema bungeni watu wanalala tu ni nani kaliabisha bunge zaidi?
Binafsi naomba JPM asimame tena katika uchaguzi wa 2020 na upinzani wapate wabunge wachache mno na ikiwezekana wakosekane kabisa, si ajabu tukapiga hatua kubwa mno katika nchi hii.
 
Mi nadhani wewe ndio unatakiwa ubadilike, watanisasa hatutakiwi kuwaona viongozi kama Miungu, kinyago tumechonga wenyewe inakuwaje kitutishe!!.

Ukome kumuita Rais wetu wa JMT ' Kinyago ' sawa? au undhani na sisi hatuyajui ' mapungufu ' na ' madhaifu ' ya Edward N. Lowassa? Rais aheshimiwe tafadhali sawa? Yaani kabisa unamuita Rais wetu Kinyago? Umeshaharibu siku yangu tayari. Nitarudi.
 
Back
Top Bottom