Siku hizi maneno hayaendani na matendo

Siku hizi maneno hayaendani na matendo

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,548
Reaction score
860,660
Kuna nyakati watu walifanya vitu kwa vitendo, walijifunza nadharia kisha wakaenda kufanya katika uhalisia wake kwa vitendo.

Kwamba kama zilikuwa habari za kuokoka watu walikuwa wanaokoka kweli kwa kweli na kuzishika sheria za ulokole hasa.

Kwamba kama mtu alikuwa kiongozi wa dini alimaanisha toka rohoni na alitenda na kuenenda kulingana na cheo chake, aliheshimu miiko na tarartibu, sheria na makatazo yote yanayokwenda kinyume na mafundisho...haikuwa rahisi kumkuta kiongozi wa dini kakengeuka.

Kwamba haikuwa rahisi kumkuta binti amedanganya kwa mchumbaake kuwa 'hajawahi' alimaanisha alichosema na alisema alichomaanisha....danganya toto ilikuwa ni msamiati na dhambi kubwa.

Kwamba kila mmoja kwa fani yake alitenda kama ilivyotakiwa na hakukuwa na kinyume kwenye lolote, kila mtu alitenda kwa uaminifu na weledi...mwanasiasa, daktari mwalimu, bwana shamba, Fundi mwashi nknk hakuna hata mmoja aliyefanya bora liende.

Lakini dunia imebadilika mambo yamebadilika mwanadamu naye kabadilika, hakuna kweli tena ndani yetu hatumaanishi tunachokisema wala kukitenda na hatutendi tunachomaanisha na kukisema, tumekuwa na umahiri mmoja tuu...kuongea sana bila kutenda hilo tumeliweza

Jamii forums haina jinsi ya kulikwepa hili, kwakuwa wanadamu hao ndio hawahawa, kuna elimu kubwa sana humu ya mambo anuwai tunaipata kila siku, shukraani kwa kila mmoja kwa mchango wake....shida iliyopo ni kwamba hatuna vitendo kwenye elimu na maarifa tunayopata hapa

Tulikuwa na masomo mazuri sana ya ufahamu na meditation, kuna mabandiko yaliyoshiba hasa, lakini kwa bahati mbaya sana tunaishia kusoma kuchangia, kuchagiza kusifu na kulikemea halafu maisha yanasonga, natamani tuwe na kikundi cha watu wachache ambao tunaweza japo kufanya kwa vitendo japo mada chache tunazojadili hapa zile zinazoleta afya ya mwili na akili(ufahamu).

Tusiwe tu watu wa kuonyesha umahiri wa kuandika hapa tujaribu na vitendo pia, nimeshakutana na baadhi ya members na tukajaribu hili lakini nafikiri changamoto za maisha na kutaka matokeo ya haraka vimekuwa kikwazo kikubwa kusonga mbele.

Zisibaki story ndani ya JF tukiamua tutaweza kwa wingi au uchache wetu...long live JF
 
Kama haya mazoezi ya utambuzi na kujitambua natamani sana niwe na mwalimu ana kwa ana akinifundisha lakini tatizo kipato.
 
Nondo zilizoshiba..rakism wa meditation mbona siku kapotea sana,yupo kweli?
 
mafunzo bei gani mkuu nahitaji kujifunza na mimi

Kabla hujauliza bei kumbuka lazima umfate mwalimu mwenye,kama yupo mtwara ufunge safari uende.
Wangekuwa wapo kila mahali ingekuwa ni vizuri, hapa Tanzania wanahesabika, sidhani kama wanafika 15.
 
JamboForums, Enzi hizo unachat huku unasikiliza mziki japo siku hizi hawaweki.....Imebaki Story tu
 
Watu wanafanya PRACTICAL zaidi yale wanayojifunza kule kwenye janvi la wakubwa!!
 
Back
Top Bottom