Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,249
Majuzi nikiwa na kikosi cha watu wanne tulienda pale Escape One katika moja ya burudani hapa Jijini
Kiingilio 15,000@ mmoja hapo ni 60,000 fasta imekata, ndani kuagiza raundi moja tu bili ikaja 36,000
Baada ya muda tukaagiza Kuku wawili (maana vikuku vya siku hizi nusu ni kama robo) na chips nne hapo ikakata 80,000
Huenda wachangiaji walio wengi watakuja na KASI ya kusema hiyo ni anasa lakini ukweli ni kwamba hata ukiwa nyumbani tu ukivuta laki hadi jioni unaweza usiamini imeenda wapi na kama unchenji elfu kumi ni kama umechenji BUKU
Hayo ndiyo maisha ya leo