Siku Dkt. Bashiru, Prof. Kabudi au Balozi Polepole wakisimama dhidi ya CCM nitaogopa sana lakini Lissu, Lema na Mbowe hawana maajabu

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,201
1,839
Hapa nayazungumzia magijwi hodari wa kujenga na kutetea hoja. Ni watu ambao kwa mfanano wamebeba taswira za Baba wa taifa kimaono, Dkt. Magufuli kiutendaji na Dkt. Kikwete kiuzungumzaji. 'Combination' ya watu hao kwa hakika ndio itakayeleta upinzani wa kweli kwa CCM.

Siku ambayo hao watatu wakiungana kuna uwezekana CCM itapata tabu kwa kiasi fulani lakini kama sio hao kizazi hiki hakina mtu nje ya hao wa kuitetemesha CCM.

Sio Lissu, Lema au Mbowe wataweza kuiondoa CCM madarakani wala kizazi kinachotokana na wao.
 
Hivi we jamaa unadhani katika hao uliowataja wanaweza kumfikia walau nusu ya nguvu aliyokuwa nayo Edo wa 2015?

Kwa mfumo wetu wa Siasa za Nchi hii, hakuna Mwanasiasa mwenye nguvu Nje ya CCM, wengi wakitoka wanakuwa kama Watoto wa Paka waliyomwagiwa Maji.

Nguvu unazodhani Wanazo, Wanazo kwa sababu ya Mfumo umeruhusu wawe nazo, Nje ya Hapo wanakuwa kama Mandonga tu Kila kiwanja wanapigwa kwa Knock out
 
Hapa nayazungumzia magijwi hodari wa kujenga na kutetea hoja. Ni watu ambao kwa mfanano wamebeba taswira za Baba wa taifa kimaono...

Hao pamoja na wengine wengi wanaungana ndani ya chama kuimarisha chama na kujenga serikali yenye nguvu.

Hawawezi fanana na walioamua kuwa wakimbizi na kwenda kuishi ughaibuni huku wakitaka madaraka Tanzania

Chama chetu Cha Mapinduzi chajenga nchi
 
Back
Top Bottom