Siku ATCL itakapoitwa "Air Tanzania Express"

OkSIR

Senior Member
Joined
Jun 3, 2009
Posts
108
Reaction score
1
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kampuni ya ndege ya tanzania (ATCL)liko katika mchaakato wa kubadili jina na kuitwa AIRTANZANIA EXPRESS...akiongea na mtoa chanzo amesema wameambiwa tangu mwezi wa 4 kutafuta pesa kwa ajili ya redanders ya wafanyakazi wote inayokadiriwa kufikia billion 16.....na kuanza kuajiri upya.akiwa katika kuongea kwa machungu alisema laiti wanaotarajiwa kufanya haya mwl nyerere asikie na kuwahoji mmoja baada ya mwingine.......
Habari zaidi zinasema kampuni hiyo mpya inayotarajiwa kuanzishwa na wachina wanaoitwa sonagol ilitarajiwa kuanza kazi rasmi jul 02/2009 lakini kutokana na mchakato wa madeni ya kampuni hii wachina waliona kuibeba ATCL kama yenyewe bora waende sudan kusaka madini...wakiwa katika mikutano yao wachina hao ambao inasemekana walikuja kwa nia ya kusaini mikataba kulingana na makubaliano ya awali na serikali walijikuta wakiambiwa tofauti na hivyo kutoa mwongozo wao wa kuichukua kampuni hiyo ambapo moja ya mada iliyoitetemesha serikali ni swala la madeni ya kampuni.likifwatiwa na swala la nani awe CEO, nani awe CFO..katika mchakato huo viongozi wa sonagol kampuni iliokabidhiwa jukumu la kuinyanyua aitanzania wamesema na kuweka wazi vyeo vya CEO&CFO lazima vikaliwe na watu wao hapo moto mwingine ukaanza....., ilikubaliwa serikali waendelee kubeba madeni ya kampuni huku wachina wakijitayarisha kuanzisha shirika lao jipya litakalojulikana kaama AIRTANZANIA EXPRESS....
kwa mwenye dondooo zaidi atuletee jukwaani tutathmini kweli imefikia hatua ya kuanzishwa shirika jipya ama uzandiki wa viongozi wetu....

ukiwa katika kutoa mawazo yako binafsi kwa ajili ya ufanisi wa kampuni hii angalia mambo yafuatayo

1)))je ni kweli shirika limefikia hali mbaya kubadilishwa jina na kupewa wachina

2))je kuna haja ya kuwa na Top management itakayoongozwa na wachina...\

3)je ni kweli tanzania na serikali ya tanzania imeshindwa kabisa kulinyanyua kampuni hii bila kutegemea wawekezaji...ni kweli hakuna kiongozi ambae anajua airline industry vyema na kuweza kuikoa kampuni hii pasipo kutegemea hawa wachina...

4)tusiache kuangalia haswa nini chanzo kilichoipelekea kampuni hii kufikia hapo ilipo,,...

unakaribishwa
 

Sasa mkuu si ungetoa japo mapendekezo yako kuhusu hiyo top management wapewe kina nani?

Wamekuja Makaburu mmelalamika, Wahindi TRC, mmelalamika, Wakija Waarabu mna lalamika, Wawekezaji gani mnao wataka nyinyi?
 

1.Swali la kwanza lipo wazi kabisa. Shirika la ndege lina hali mbaya. Sidhani kama hili swala ni debatable.

2.Kwa nini wasiweke watu wao? Hata wewe ukiwa na biashara si utataka uajiri watu unaodhani wewe wanafaa? Sasa amuweke tu Mtanzania ili iweje? It is a business na hata ingekua mimi ningeweka mtu ninayeona mimi anafaa. Mambo ya kupeana nafasi kwa kuangalia fulani ana toka wapi haiko sehemu zote.

3.Obviously wameshindwa ndiyo maana wana tafuta wawekezaji. Ila hilo la wawekezaji sio neno. Kutafuta mbia anayeweza kukusaidia kufanikiwa zaidi siyo vibaya. Ethiopian, shirika la ndege la Ethiopia serikali ina ubia na wawekezaji tokea Marekani. Angali shirika lao lilivyo na mafanikio kuliko shirika letu. Partnership or investors is not the issue. Tatizo kubwa ni rushwa na kupeana nafasi kwa kujuana.
 
Kwa hiyo madeni tunaachiwa sisi, kampuni wanachukua wao? Hii ndo mikataba yetu TZ daily! Mtu ashakomba 15% hapo anatuachia sisi mzigo!

Kama hivyo bora kampuni iachiwe iingie kwenye bankruptcy ili waweze kupunguza hayo madeni, kama GM walivyofanya.
 
ATCL ilipokuwa inabinafsishwa kwa makaburu haikuwa na hali mbaya kama ilivyo sasa. Lakini hata hivyo isionekane kwamba kubinafsisha ndio njia pekee ya kuyaendesha makampuni/mashirika kwa tija, kwani hata wazalendo wanaweza kufanya makubwa zaidi; mfano CRDB bank. Hapa kwetu kuna nini? Mbona uwekezaji wa kigeni kwenye nchi nyingine umekuwa na faida? Mbona hatujifunzi?
 
Una uhakika na unacho kisema ndugu!?

DANIDA wanafanya nini CRDB? Au nalo ni shirika la wazalendo wa Kitanzania?

Gonga hapa upate kufunua masikio. CRDB
 
Watafute wawekezaji toka kwenye airlines hivi hao wachina wachimba madini kweli nao si watauza share zao kwa kampuni za ndege jamani hapa mbona iko wazi!!haihitaji kuwa PHD kujua....sasa nini jamani??mbona tunatetemeka sana na jina wawekezaji??tuitishe mchakato watakuja tu ila hao wachina fake....
 
Jamani kweli tungependa hili kampuni lichukuliwe na watu lakini tunachoomba kwa serikali wawape watu walio serious..s...........jamani mmeona ile barabara ya sam nujoma;wengi walilamika jamani wachina na barabara wapi na wapi....waliokaa kimya wakaakaa kimya...hivi sasa tuongeapo nimekuta folen kubwa pale barabarani....ujenzi wameanza kuichimba upya sikuishia hapo .nikaamua kusimama na kuuliza nikaambiwa kuna sehemu nyingi tu zina mawimbi......,ati wameamuriwa kuzirekebisha na katibu wa wizarani.....niliskitika sana...kinachosemekana na ambacho hakuna uwazi hawa wah walitaka kupewa vitalu kule mtwara....,wachimbe mafuta ikashindikana..,nikaona vyema tulete hoja kwa watanzania wenyewe...
 
mimi kinachonitatiza ni hawa wachina;...;jamani leo hii nimepita pale barabara ya sam nujoma wameanza kuirekebisha tena upya..wakati wa ujenzi watu wengi waliongea jamani wachina na bara bara wapi na wapi
 
mimi kinachonitatiza ni hawa wachina;...;jamani leo hii nimepita pale barabara ya sam nujoma wameanza kuirekebisha tena upya..wakati wa ujenzi watu wengi waliongea jamani wachina na bara bara wapi na wapi

kama ulikuwepo nami nimepita hapo jioni hii aiibu aiibu anyway sijui...tuwapeni as long nasikia hizo ndege zinazofanya kazi atc ni zao tutafanyaje??
 
 
Last edited:
last night nimeona kitu CBS (letterman show) sikuamini lakini baada ya muda one of my friends akaniambia same thing ndio nikaamini nilichoona ni kweli....AIRTANZANIA walikuwa wanatangaza shirika lao kwenye kipindi cha letterman,hivi wana ndege hata moja inayo operate states? au target yao ni nini? au ndio ulaji wa wajanja tu...naomba maelezo!
 
Sasa mkuu si ungetoa japo mapendekezo yako kuhusu hiyo top management wapewe kina nani?

Wamekuja Makaburu mmelalamika, Wahindi TRC, mmelalamika, Wakija Waarabu mna lalamika, Wawekezaji gani mnao wataka nyinyi?
Ungeongezea kwamba "wabongo" wameshindwa walipewa for 50 years wanaiba na kujaza matumbo yao.
 
Ukweli ni kwamba kampuni ilitakiwa iachwe ife! Kama kuna haja ya kuwa na National carrier basi wangeanza mwanzo kabisa.
 
Ukweli ni kwamba kampuni ilitakiwa iachwe ife! Kama kuna haja ya kuwa na National carrier basi wangeanza mwanzo kabisa.

Mie kuna kitu sielewi... Kila move inayopendekezwa, tunaizika mapema sana kabla ya kupima!!! Sasa tufanyeje na ATC? au tuliache ndege zichoke mpaka zianguke ziue ziishe halafu ibaki historia kama dinosaurs??

Wasauzi, wamasai, wachagga, wanyasa wote tuliwawasha na sasa wachina!! kwangu tatizo si nani anawekeza, tatizo ni uwezo wa baadhi ya watendaji kusimami utekelezaji

Wale wenzetu weledi--- hedu saidia masikini kimawazo naye arushe ndege!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…