Keagan Paul
JF-Expert Member
- Jul 19, 2018
- 500
- 3,057
Wakuu Nisiwachoshe sana
Nazungumzia mafanikio ya kweli katika maisha, sio mafanikio ya janja janja. Mafanikio ya janja janja ni kwamba leo una pesa nyingi, magari ya kifahari halafu baada ya miezi/miaka kadhaa unarudi tena kwenye maisha ya kuungaunga\kukosa pesa.
Ndugu zangu kama unataka kuwekeza kwenye jambo lolote ambalo litakukwamua kuondokana kwenye umaskini wa kudumu basi wekeza kwenye Miradi ya muda mrefu. Pengine wekeza kwenye miradi ya zaidi ya miaka 3 na zaidi. Hapo ukifanikiwa unakuwa umefanikiwa mazima. Ndani ya hiyo miaka 3 na zaid unakuwa ulishajifunza hasara na faida za huo mradi.
Wengi wetu tunapenda kupata faida za haraka hivyo hupelekea kufanya miradi ya kutupatia pesa za haraka. Kufanya miradi ambayo tutapata return ndani ya muda mfupi, lakini unatasahau kwamba uwezekano kwa kurudi nyuma ni wa muda mfupi hivyo hivyo.
Anza biashara yako polepole bila kuitegemea hiyo biashara yako muda wa miaka 3 na zaid lazima utaona mafanikio, lazima mtaji utakua.
Mfano: Nenda kanunue Hisa, Nenda kapande miti mingi ya mbao huko Njombe, Iringa, miti ya matunda huko Tanga, Lushoto. Ndani ya miaka 5 mpaka 7 unakuwa umepiga hatua kubwa kimaisha.
Nenda pole pole siku 365 pekee hazitoshi kukupatia mafanikio ya kudumu. Endelea kukuza mtaji wako. Usitumie hata senti 1 kutoka kwenye biashara yako changa ulioianzisha mpaka baada ya miaka 3 na zaidi lazima utatoboa. Hakuna mafanikio ya kweli chini ya siku 365.
Hata unayemuoa leo amefanikiwa kupitia Bar, aliwekeza kwenye hiyo Bar kwa zaidi ya siku 365, ndo leo wewe na mimi tunaona amefanikiwa sana. Kwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe, hata ujenge nyumba ili iwe nzuri kwa kiwango fulani ni lazima ujenzi huo utazidi simu 365, sasa kwa nini unadhani unaweza kufanikiwa kwenye maisha kwa chini ya siku 365?
Pambana bila kukata tamaa, usitumie kwenye mambo yako binafsi huo mtaji wako mdogo kama bado kujatoboa siku 365, achana na mambo ya kusaidia ndugu ovyo kama kweli unataka kufanikiwa. Utawasaidia mbele ya safari.