Siku 20 za TUCTA hazijaisha tu?

Siku 20 za TUCTA hazijaisha tu?

MkamaP

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2007
Posts
8,167
Reaction score
3,272
Wana-jamvi nina shauku ya kujua siku za TUCTA 20 bado kutimilika tu? maana naona hata serikali haina mpango wa siku 20 za TUCTA. Labda nilipitwa na news tuhabarishane.
 
kwahiyo swala la tucta ndo limekwisha nini, walai haki yanani hapo!!!!!!!!
 
Kwa ule mkwara wa kaka sindibadi unadhani atafurukuta mtu?
 
Kisheria mnajua kwamba ule mkwara wa JK alivunja sheria za ajira kimataifa?.. hakuna rais anayeweza kuvunja maandamano ya wananchi wake (kisheria) kwa kuwaambia wakiandamana watafukuzwa kazi..Lakini ajabu ya Mungu, kwa umaskini na njaa yetu watu tumeshindwa hata kuwatetea - Utakosa kumpenda JK!
 
Hivi hao Tanganyika law chambers kazi yao ni nini?? Lakini tarehe ya mwisho kwa hawa ghasia kutoa tamko la serikali ni 29/5/2010 kwa hiyo nadhani wiki ijayo TUCTA wata twambia wanafikiria nini.
 
kazi kwa wafanyakazi kukumbushia wapi wamefikiakama viongozi wao wamenyamaza basi wachague wengine wa kuendeleza mapambano
 
Kisheria mnajua kwamba ule mkwara wa JK alivunja sheria za ajira kimataifa?.. hakuna rais anayeweza kuvunja maandamano ya wananchi wake (kisheria) kwa kuwaambia wakiandamana watafukuzwa kazi..Lakini ajabu ya Mungu, kwa umaskini na njaa yetu watu tumeshindwa hata kuwatetea - Utakosa kumpenda JK!

Sasa nani awatetee wafanyakazi, sisi walala hoi ndo tunawategemea wafanyakazi watetee maslahi yetu na ya nchi hii. Sisi wakulima tumewapeleka vijana wetu(wafanyakazi) shule watakapoelimika waje watutetee sie wachunga ng'ombe na wasaka nyoka sisi.Sasa ninani wakututetea mwingine ?
 
MkamaP,
Hapa mkuu unazungumza siasa za JF...
Mfanyakazi ndiye anayenunua mazao yenu wakulima, bila yeye kupata mshahara mzuri hawezi kununua mali zetu hivyo unapomtetea Mfanyakazi unatetea maslahi yako vile vile..
 
MkamaP,
Hapa mkuu unazungumza siasa za JF...
Mfanyakazi ndiye anayenunua mazao yenu wakulima, bila yeye kupata mshahara mzuri hawezi kununua mali zetu hivyo unapomtetea Mfanyakazi unatetea maslahi yako vile vile..

Kivipi sasa mkuu,
Msomi atatetewa vipi na mtu ambaye hakwenda shule? tumepeleka wasomi ili waje watutee na kutufanyiza maisha bora, hatujapeleka wasomi waje kugombea mshahara ili wanunue gogogo ama nembe nilizomvua na hata hivyo ikitokea hivyo basi ni kisifa kisaidizi.

Sasa kwa namna unavyo-ongea ina maana kwamba tumepeleka wasomi kwa kukamua ji -ng'a (ng'ombe) zangu ili aje apate kazi na baadae nimtetee kupata mshahara mzuri ili aje anunue ma-numbu(viazi) yangu.? .Bado sijaona sense, labda unipe shule zaidi.
 
Eeeeh bwana eeeh umenikumbusha mbali sana - Unajua Nembe hazipo tena?. zimebakia ngere (gogogo) tu unajua tena zimekaa kama papa sangara hawezi kuwameza.

Ni hivi mkuu, wee mkulima ukivuna mazao yako sii unayapeleka sokoni? na huko sokoni unategemea nani atakuwa mteja wako kama sii mfanyakazi? Na sisi wavuvi tunawapeleka vijana wetu shule ili wapate mtaji wa maisha nasi tupate kuuza kesho samaki wetu kwa wasomi hawa bei juu tukikuza soko la ndani.

Aliyeko Dar akija likizo atuletee mtaji wa kuongeza mitumbwi na nyavu, maisha yanaendelea hatuhitaji msaada wa mzungu kutupa misaada yenye masharti. Na laukama hatukuwapeleka watoto wetu shule wangebakia kuvua samaki na kijiji kizima sote tungekuwa wavuvi sijui wangemuuzia nani hizo samaki...

Sasa ile hasira ya kulea, mifeza ulopoteza kumpeleka shule halafu haleti ngawila nyumbani, haya samaki nao wanaoza sokoni hawa wasomi wakidai bei juu ndio inatakiwa kukusukuma wewe kuingia barabarani na mabango...
Bado tu Wasu?
 
Kimya kingi kina mshindo mkuu; Tanzania ya sasa si ya jana!
 
Back
Top Bottom