Wakati wa kufunga ndoa, baba mkwe alipendekeza kutupatia nyumba yake, Ilikuwa ni nyumba ya kisasa, ikiwa na baadhi ya samani tayari.
Baada ya kutafakari kwa kina, niliamua kukataa pendekezo hilo. Badala yake nilirudi na mke wangu kwenye nyumba ndogo ya kupanga. Ingawa ilikuwa ndogo, amani ya moyo niliyokuwa nikiipata ilikuwa ya thamani kubwa sana.
Hata baada ya familia yetu kuongezeka, niliendelea kushawishiwa kuhamia kwenye ile nyumba kubwa, lakini niliendelea kusimamia uamuzi wangu.
Nilijibana, nikapangisha nyumba kubwa zaidi kulingana na uwezo wangu, ambayo tunaishi hadi sasa, huku nikiendelea na ujenzi unaokaribia kukamilika.
Uamuzi wangu ulitokana na misingi kadhaa.
sikutaka kuingia katika hali ya kujiona mnyonge au kuhisi kuwa nalazimika kuishi kwa neema ya familia ya mke wangu.
nilielewa kuwa msaada wa aina hiyo unaweza kugeuka fedheha, nikimaanisha uwezekano wa kuja kutupiwa mabegi nje na kufukuzwa kwenye nyuma ambayo sio yako, hii inatokeaga mkipishana kauli na mke wako akirudi kwao unatishwa kufukuzwa au baba mkwe akifariki na watoto wake hawakuupenda uamuzi wake wa kukupa nyumba, watakufukuza kwa kukudhalilisha.
Zaidi ya hayo, nilitambua kuwa msaada unaweza kubadilika na kuwa chombo cha kukumbushia au kudai shukrani kupita kiasi, kiasi cha kudhoofisha heshima na uhuru wangu. utaanza kuambiwa wazi wazi kuwa shukrani ya punda ni mateke, ulipewa nyumba bure kwanini wewe husaidii, n.k.
Pia, hata masuala ya umiliki kama hati ya nyumba yangeweza kuwa chanzo cha migogoro, familia ya mke wangehisi hofu juu yangu kutaka kuuza nyumba yao.
Sikutaka kumpa nafasi hata siku moja mke wangu apate kiburi kuwa ninaishi kwao. Nilijua wazi kwamba siku moja tungeweza kugombana, na angeanza kusema "mwaname gani wewe unakaa nyumba ya baba mkwe", “niache kwanza hapa ni kwetu” Au pengine siku nikichelewa kurudi, wangeweza kumwambia anifungie nje kwa sababu hiyo ni nyumba yao.
Kwa ujumla, nilijifunza kuwa amani ya moyo, uhuru wa maamuzi, na kujitegemea ni misingi muhimu sana katika kujenga maisha ya familia yenye heshima na utulivu.