Sijutii kukataa kupewa nyumba nzuri na baba mkwe, nina amani sana na familia yangu kwenye nyumba ya kawaida niliyopanga

Mimi nililazimishwa tukakae ukweni kisa mama mtu alikuwa mgonjwa mgonjwa kwa lengo kwamba wife awe anamuhudumia kwa ukaribu. Wife naye alikuwa kashadadia tukakae tu kwani itatupunguzia ugumu wamaisha.

Nilichowaambia ni kwamba nimeoa kwa lengo la kujiongezea ugumu wa maisha sio kurahisisha maisha. Mama mkwe aliniona Nina roho mbaya sana.
Dah
 
Huo ndio mwanzo wa kuanza kuwekeana chuki hapo, wao wataanza kuona hutaki kuishi unataka kuja kuiuza nyumba yao.

Na mimi niliona hata nikiishi hapo basi siku za mbele nikigombana na wife wataanza zile dharau bila sisi usingepata pa kuishi au shudkrani ya punda mateke.

Kujiwekea kinga nilikataa

Uko sahihi, Hapo kuna siku ukigombana na Wife, unaeza sikia mwaname gani wewe unakaa nyumba ya baba mkwe, au niache kwanza hapa ni kwetu, au siku umechelewa kurudi akakufungia nje makusudi si kwao.

Bora kuchanja mbuga tuu.
 
umenielewa vizuri sana, ni ngumu kuwa kichwa cha nyumba kwenye nyumba ambayo sio yako wala huilipii kodi
 
Wakati wa kufunga ndoa, baba mkwe alipendekeza kutupatia nyumba yake, Ilikuwa ni nyumba ya kisasa, ikiwa na baadhi ya samani tayari.

Baada ya kutafakari kwa kina, niliamua kukataa pendekezo hilo. Badala yake nilirudi na mke wangu kwenye nyumba ndogo ya kupanga. Ingawa ilikuwa ndogo, amani ya moyo niliyokuwa nikiipata ilikuwa ya thamani kubwa sana.

Hata baada ya familia yetu kuongezeka, niliendelea kushawishiwa kuhamia kwenye ile nyumba kubwa, lakini niliendelea kusimamia uamuzi wangu.

Nilijibana, nikapangisha nyumba kubwa zaidi kulingana na uwezo wangu, ambayo tunaishi hadi sasa, huku nikiendelea na ujenzi unaokaribia kukamilika.

Uamuzi wangu ulitokana na misingi kadhaa.

sikutaka kuingia katika hali ya kujiona mnyonge au kuhisi kuwa nalazimika kuishi kwa neema ya familia ya mke wangu.

nilielewa kuwa msaada wa aina hiyo unaweza kugeuka fedheha, nikimaanisha uwezekano wa kuja kutupiwa mabegi nje na kufukuzwa kwenye nyuma ambayo sio yako, hii inatokeaga mkipishana kauli na mke wako akirudi kwao unatishwa kufukuzwa au baba mkwe akifariki na watoto wake hawakuupenda uamuzi wake wa kukupa nyumba, watakufukuza kwa kukudhalilisha.

Zaidi ya hayo, nilitambua kuwa msaada unaweza kubadilika na kuwa chombo cha kukumbushia au kudai shukrani kupita kiasi, kiasi cha kudhoofisha heshima na uhuru wangu. utaanza kuambiwa wazi wazi kuwa shukrani ya punda ni mateke, ulipewa nyumba bure kwanini wewe husaidii, n.k.

Pia, hata masuala ya umiliki kama hati ya nyumba yangeweza kuwa chanzo cha migogoro, familia ya mke wangehisi hofu juu yangu kutaka kuuza nyumba yao.

Sikutaka kumpa nafasi hata siku moja mke wangu apate kiburi kuwa ninaishi kwao. Nilijua wazi kwamba siku moja tungeweza kugombana, na angeanza kusema "mwaname gani wewe unakaa nyumba ya baba mkwe", “niache kwanza hapa ni kwetu” Au pengine siku nikichelewa kurudi, wangeweza kumwambia anifungie nje kwa sababu hiyo ni nyumba yao.

Kwa ujumla, nilijifunza kuwa amani ya moyo, uhuru wa maamuzi, na kujitegemea ni misingi muhimu sana katika kujenga maisha ya familia yenye heshima u
Ilikua sahihi upande wako. Nilipewa nyumba mbili na mama mkwe, hivyo sikuacha, kodi anachukua mke ndo zimemsomesha masters.
 
Maamuzi mazuri, siku ukizinguana na wife hiyo ndio ingekua fimbo ya kukuchapia mbona ungenyooka bora ulisanuka mapema.
 
Wakati wa kufunga ndoa, baba mkwe alipendekeza kutupatia nyumba yake, Ilikuwa ni nyumba ya kisasa, ikiwa na baadhi ya samani tayari.

Baada ya kutafakari kwa kina, niliamua kukataa pendekezo hilo. Badala yake nilirudi na mke wangu kwenye nyumba ndogo ya kupanga. Ingawa ilikuwa ndogo, amani ya moyo niliyokuwa nikiipata ilikuwa ya thamani kubwa sana.

Hata baada ya familia yetu kuongezeka, niliendelea kushawishiwa kuhamia kwenye ile nyumba kubwa, lakini niliendelea kusimamia uamuzi wangu.

Nilijibana, nikapangisha nyumba kubwa zaidi kulingana na uwezo wangu, ambayo tunaishi hadi sasa, huku nikiendelea na ujenzi unaokaribia kukamilika.

Uamuzi wangu ulitokana na misingi kadhaa.

sikutaka kuingia katika hali ya kujiona mnyonge au kuhisi kuwa nalazimika kuishi kwa neema ya familia ya mke wangu.

nilielewa kuwa msaada wa aina hiyo unaweza kugeuka fedheha, nikimaanisha uwezekano wa kuja kutupiwa mabegi nje na kufukuzwa kwenye nyuma ambayo sio yako, hii inatokeaga mkipishana kauli na mke wako akirudi kwao unatishwa kufukuzwa au baba mkwe akifariki na watoto wake hawakuupenda uamuzi wake wa kukupa nyumba, watakufukuza kwa kukudhalilisha.

Zaidi ya hayo, nilitambua kuwa msaada unaweza kubadilika na kuwa chombo cha kukumbushia au kudai shukrani kupita kiasi, kiasi cha kudhoofisha heshima na uhuru wangu. utaanza kuambiwa wazi wazi kuwa shukrani ya punda ni mateke, ulipewa nyumba bure kwanini wewe husaidii, n.k.

Pia, hata masuala ya umiliki kama hati ya nyumba yangeweza kuwa chanzo cha migogoro, familia ya mke wangehisi hofu juu yangu kutaka kuuza nyumba yao.

Sikutaka kumpa nafasi hata siku moja mke wangu apate kiburi kuwa ninaishi kwao. Nilijua wazi kwamba siku moja tungeweza kugombana, na angeanza kusema "mwaname gani wewe unakaa nyumba ya baba mkwe", “niache kwanza hapa ni kwetu” Au pengine siku nikichelewa kurudi, wangeweza kumwambia anifungie nje kwa sababu hiyo ni nyumba yao.

Kwa ujumla, nilijifunza kuwa amani ya moyo, uhuru wa maamuzi, na kujitegemea ni misingi muhimu sana katika kujenga maisha ya familia yenye heshima na utulivu.
Ulikosea big time ndugu
 
Wewe sio mjasiriamali. Hujui kutumia fursa. Ni wale watu wanaojiuliza "watanionaje?".... ungekaa hapo kwa muda ungesevu pesa na huenda huo ujenzi wa nyumba yako ungeshaisha.
 
Hongera,jirani hapa mara atupiwe nguo nje,mara akapange,ndugu zake wakija wanasimangwa na kufukuzwa,,huyu mwanaume ni nes sijui Dr lkn Hana ajira anajishikiza kwenye vihospital,mwanamke nae Hana ajira now kafunguliwa ofisi ya muamala na baba yake ,mwanamke kwao pesa zipo na wapo watoto wawili TU, huyu mwanaume ni manyanyaso tupu🙌

Alifukuzwa karudi tena,anasema anarudi kwaajili ya watoto. Anafokewa kama mtoto daah,inasikitisha.
NI fedheha sana mwanaume kuishi ukweni
 
Wakwe ni sawa na wazazi wako
Tatizo humuoni mkwe wako kama baba yako
Kwani angekupa baba yako mzazi pia ungekataa?!?
 
Baba mkwe ni baba, Ichukue hiyo nyumba ipangishe.
 
Maamuzi mazuri, siku ukizinguana na wife hiyo ndio ingekua fimbo ya kukuchapia mbona ungenyooka bora ulisanuka mapema.
Kwanza hata dugu zake wanaweza kukudharau, watamwambia akufungie nje, nyumba ni yao
 
Wewe sio mjasiriamali. Hujui kutumia fursa. Ni wale watu wanaojiuliza "watanionaje?".... ungekaa hapo kwa muda ungesevu pesa na huenda huo ujenzi wa nyumba yako ungeshaisha.
Haya maisha sio kila kitu ni pesa
 
Umejiumiza bure tu ungekaa kwenye hiyo nyumba then hela uliyotumia kujengea kwa mateso na damu ungeizungushia kwenye biashara leo ungekuwa tajiri mkubwa tu na ungeweza kujenga nyumba 2, baba mkwe ungemrudishia nyumba yake kwa furaha na vigelegele tena ungemwambia nyumba yake imezaa nyumba 2 na 1 umepangisha.
There is no such a thing as free lunch. Never.
 
Back
Top Bottom