Sijui ya jeshini mie - Dk. Mwinyi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sijui ya jeshini mie - Dk. Mwinyi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 22, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Na Alfred Lucas - Imechapwa 19 October 2011

  [​IMG]
  [​IMG]
  WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, hajui "kinachoendelea" eneo la kambi ya jeshi ya usafirishaji-Kunduchi (KTC), MwanaHALISI limegundua.

  Waziri Dk. Mwinyi aliliambia gazeti hili kwamba hafahamu kinachoendelea katika eneo lenye machimbo ya kokoto Kunduchi-Mtongani, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

  Wakazi wa eneo la Kunduchi wanadai kuwa askari wa kambi hiyo, wamekuwa kwenye ‘operesheni maalum' ya kuwatimua kutoka eneo ambako yamekuwa makazi yao ya miaka mingi.


  Diwani wa kata ya Kunduchi, Janeth Rethe aliliambia gazeti hili juzi kuwa hadi kufikia Ijumaa iliyopita, watu watano walikuwa wameshinikizwa kuhama eneo hilo.

  Amesema askari waliofika kwenya makazi ya raia, wakiwa katika makundi, wamewajeruhi raia watano. Diwani amesema waliokumbwa na kadhia hiyo wamepigwa na kuchubuka mikono, miguu na usoni na nyumba 62 zimebomolewa.

  Waziri Mwinyi alipoulizwa juu ya kadhia hiyo, alisema hajui kinachoendelea na kwamba mwandishi aulize kwenye kambi husika.


  Hasa waziri aliulizwa juu ya taarifa za askari wanaodaiwa kubomoa nyumba za raia na kuwapiga.


  Alisema, "…bwana eeh! Wewe piga simu makao makuu ya jeshi bwana; mimi sina taarifa hizo. Fuatilia hukohuko," kisha alikata simu.


  Diwani Rethe amedai kuwa eneo la makazi ya raia na kule ambako ni machimbo ya kokoto "panatakiwa na wakubwa jeshini."


  Hakueleza waziwazi na kwa uhakika ni askari gani hasa wanataka eneo hilo ambako wananchi tayari wamejenga nyumba za kudumu.


  Diwani amesema juhudi zake na wenzake kukutana na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, "angalau kumuuliza kulikoni hazijaweza kufanikiwa."

  Rethe ametoa wito kwa serikali kuwafidia wakazi wa kata yake ambao amesema kwa zaidi ya miaka 10 sasa wamefanya eneo hilo kuwa makazi yao ya kudumu.

  "Hata kama wanataka kulichukua eneo hili na kuligawa kwa watu wao, basi ni vema serikali ikafuata taratibu ya kutoa fidia. Maana hawa wanaotaka kuondolewa hapa, ni binadamu pia. Serikali inapaswa kulinda raia wake," anasema diwani huyo kwa sauti ya uchungu.


  Anasema, "Pamoja na kwamba eneo hili liko nje kabisa ya kambi ya jeshi, lakini tunaona juhudi za kutuhamisha kwa nguvu na kuharibiwa mali zetu."


  Mwenyekiti wa kamati ya mipango miji wa manispaa ya Kinondoni, Tarimba Abbas ameliambia MwanaHALISI, "Nimelisikia hilo, bali lipo juu ya mamlaka yangu."

  Alisema, "Kwa sasa suala hili lipo mikononi mwa mkuu wa mkoa, halmashauri na jeshi lenyewe. Ukitaka kupata taarifa zaidi wasiliana na mkuu wa mkoa au mkurugenzi wa manispaa."

  Taarifa zinasema ubomoaji nyumba za wakazi wa Kunduchi-Mtongani ulianza 22 Julai mwaka huu.


  Imefahamika kuwa bomoabomoa imefuatia hatua ya mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni.


  Tarehe 14 Julai mwaka huu, mkurugenzi wa manispaa aliandika waraka kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa Kunduchi, akiagiza kuhama kwa wakazi hao kwa madai kuwa wako ndani ya eneo la jeshi na wanapasua mawe kwa kutumia baruti.

  Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kunduchi Mtongani, Richard Rusisye ambaye alihojiwa kwa njia ya simu kuhusiana na barua ya mkurugenzi, alisema, "Kinachofanyika sasa kiko nje ya uwezo wangu."

  Rusisye ndiye tarehe 20 Julai mwaka huu aliandika barua kwa mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni kupinga kubomolewa kwa nyumba hizo.


  Katika barua yake hiyo kwa mkurugenzi, yenye Kumb. Na. SM/KMT/No172/11, Rusisye anasema, "Wananchi hawamo ndani ya eneo la jeshi kama inavyodaiwa. Wapo nje ya beacon (alama za mipaka) ya jeshi."


  Rusisye alikuwa anajibu barua ya mkurugenzi wa manispaa ambayo iliagiza kuondolewa kwa aliowaita "wavamizi wachimba kokoto eneo linalomilikiwa na jeshi ifikapo 30 Julai 2011."


  Akiandika kwa njia ya msisitizo, Rusisye anasema, "Kwanza, notisi yako haikutaja majina ya walengwa…Huelezi watu hawa watapelekwa wapi baada ya kuondolewa hapa."

  Anasema, "Katika azimio la serikali ya mtaa, tulikubaliana watu hawa wasichimbe tena mawe kwa kutumia baruti bali watumie eneo hilo kwa kuishi tu. Hivyo ndivyo wanavyofanya sasa."

  Tayari kuna kesi Na. 90 ya mwaka 2009 katika mahakama kuu kitengo cha ardhi ambapo wakazi wa Kunduchi-Mtongani wanapinga kuhamishwa. Kesi hiyo bado haijaamuliwa.


  Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda amesema, anachofahamu yeye ni kwamba nyumba zinazobomolewa ni zile zilizoko ndani ya eneo la jeshi.


  Mkuu wa mkoa, Said Meck Sadick, wala msemaji wa jeshi, hawakupatikana baada ya simu kuita bila kupokelewa.


  Lakini mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alipoulizwa iwapo anafahamu lolote kuhusu suala hili, alikata simu. Mwandishi alipiga tena na tena, lakini simu haikupokelewa.
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Hapa kuna utratra wanawaogopa wanageshi rao..wanaona wale wakitaka lao hawana siasa na itakuwa wameshawaambia kwa barua rasmi!!
   
 3. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Huyu waziri ni kiazi kweli, hajui mambo ya Wizara yake, nani atayajua2
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sijui mimi sijui na kama wamekwambia wanatimuliwa mimi sijui
  nani kakuambia, nimesema sijui na hata rais pia husema hajui na mimi sijui

  tena na wewe sikujui, jeshi silijui, hao wakwezi wa minazi nao siwajui
  sijui chochote na mambo yenu hayo ya jeshi siyajui, na jeshi silijui
  nani alikwambia mimi ni mwanajeshi, nasema sijui na ukiuliza zaidi na wewe sikujui

  sijui chochote yakheeeeeeeeeeeeeeee
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  YEYE HAJUI, MKULU NAE HAJUI YUKO BIZE NA PhD

  HIVI AKIJUA ITAKUAJE

  HAJUI NA SI LAZIMA KUJUA NA KUANZIA LEO YEYEY HAJUI HATA HIYO WIZARA YA ULINZI YEYE HAJUI NA YEYE SIO MLINZI NA HAFANYI KAZI ULTIMATE SECURITY WALA GROUP FOUR
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Lol!the land of sijui. Such an upgrade from 'naomba'. Nice one mtm
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  TENA NA WEWE SIKUJUI, JF SIIJUI, TANZANIA SIIJUI WIZARA SIIJUI, MIMI KILA KITU SIJUI NA NAJUA KWAMBA SIJUI

  THIS IS OUR COUNTRY WHERE ALL TEH "SIJUI" PEOPLE ARE GIVEN A LEADERSHIP ROLE..... POOOOOOffff!!!

  INAKERA MTU WANGU MWENYEWE.... INATIA KINYA,

  KIBAYA ZAIDI UNAPISHANA NAE MJINI ANA GARI INA LEBO YAKE PEKEE.... WAWEZA KUMUULIZA "HABARI ZA MCHANA" NA AKAJIBU SIJUI

  LAKINI KWENYE KULITAFUNA TAIFA WOTE WANAJUA WANG'ATE WAPI

  MAMBAFFFFFFFFFFFFFF
   
 8. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,373
  Likes Received: 2,420
  Trophy Points: 280
  Ndio tatizo kupewa cheo bila ya kuwa na sifa, haya ndio mambo ya kiafrika, wanashangaa ya LIbya yalianza kivipi, yeye yuko tayari kuchota ma allowances, per diem, mshahara na rushwa tu!
  Kwanza naona yuko pale kama kinyago tu, sidhani kama anajua chochote pale!
  Tanzania Tanzania!
   
 9. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  KIAZI tena kibovu-ukipika/kaanga hakiivi! Bahati mbaya ukiondoa Mawaziri wachache ktk jibaraza (too big kuitwa Baraza) la Mawaziri la nchi yetu waliowengi hawajui yanayoendelea katika Wizara zao husika. Wanayoyajua zaidi ni yale yanayokuwa na manufaa kwao na wevi wenzao wanaowatumia kujinufaisha!
   
 10. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nasema tena wakuu mtu yeyote akijenga kwenye eneo fulani na akakaa kwa miaka mitatu bila kubughudhiwa hata kama eneo siyo la kwake huyu kisheria lile eneo linaturn kuwa lake na hata ikibidi kumhamisha inabidi alipwe full compasation!
   
 11. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  hata aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani lawrence masha hajui idadi ya magereza yaliyo nchini.hawa mawaziri hawapo kwa maslahi ya nchi bali familia zao
   
 12. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Waziri mzima hajui majukumu yake kama waziri. Hajui mipaka ya majukumu yake!!.

  Inahitaji ujasiri zaidi wa kichaa kutembea uchi, waziri mzima kukiri hadharani kuwa hajui majukumu yake.

  Kama waziri anakiri kuwa hajui majukumu yake, nani atayajua!.. Shame on you!
   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  ahahaha CCM bwana mh
   
 14. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Da hilo jibu la huyo waziri sharobaro kiboko.... Hivi hawa watu walio kwenye hili genge la ufisadi ( sababu kukubali kuwa waziri ktk wizara ambayo hujui wala huguswi na mambo/matukio yake ni ufisadi mkuu) hawana hata ile aibu ya kawaida tu ya binadamu?!
   
Loading...