sijui wasira anafikiria kwa kutumia nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

sijui wasira anafikiria kwa kutumia nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by VIKWAZO, May 26, 2011.

 1. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  MAMLAKA za vijiji, kata na wilaya zimeagizwa kuhakikisha vijana wanajiunga katika vikundi vya uzalishaji mali kwa kuwawezesha ili waondokane na umasikini unaowakabili na wengi wao kutokuwa na ajira.

  Kauli hiyo imetolewa mjini hapa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira wakati alipokuwa akihutubia mikutano ya hadhara katika vijiji vya Tairo na Nyamatoke wilayani humo.

  Wassira ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Bunda amesema kuwa ni wajibu wa serikali za vijiji na wilaya kote nchini kuweka mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa vijana ambao ni nguvu kazi tegemezi ya taifa kuwezeshwa kwa kadri inavyowezekana ili waweze kujiajiri badala ya
  kuwaacha wazurure mitaani.


  "Vijana wetu hawa tunawasomesha sawa, lakini lazima tuwawekee misingi imara ya maisha yao ya kesho maana hawa ndio nguvukazi ya taifa hili.

  Lazima serikali za vijiji, kata na wilaya muone namna ya kuwaokoa mara moja," alisema
  Wassira.

  Alisema serikali za vijiji na kata zinapaswa kuwahamasisha vijana hao kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali kama vile vya kilimo, uvuvi na ufugaji na kuvisaidia kupatiwa mikopo ya mitaji na nyenzo za kazi.

  Alisema kutokana na vijana wengi kutokuwa na ajira za kuwaingizia mapato ndiyo sababu wanachotwa kirahisi na wanasiasa uchwara wanaowahamasisha kushiriki katika vurugu za kile kinachoitwa kudai haki.

  "Wasipowezeshwa ndio maana wanasiasa uchwara wanawashawishi kirahisi kushiriki katika
  maandamano ambayo wengi wao wanapoteza maisha yao na hivyo kupotea kwa nguvu kazi muhimu ya taifa hili," amesema Wassira

  maoni yangu: hivi kwa hali ilivyo sasa kuna kijiji kinaweza kusaidia kuondoa tatizo la ajira kwa wasome wa nchi hii?
  hizo wilaya anazosema ni lini zimeanza kupanga mipango ya taifa ili?
  kama wameshindwa kuzalisha ajira walisosema waseme mapema ili tujua cha kufanya,
  habari ya kuita watu wanasiasa uchwara yeye na sisi vijana nani anatumia akili?
  mimi nadhani huyu ana petrol kichwa jua ikiwaka anakuwa kama analipuka, maana petrol inaweza kuwa hata kwa jua
   
 2. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,167
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Hahahaaa, anawaza kwa kutumia Tumbo
   
 3. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  kwani hili zee (tyson) bado lipo? siku hizi halisikiki kabisa, sijui lilipigwa stop kuongea pumba? naona limejisahau limeanza tena kuropoka, huyu si ndio mbunge wa bunda? wilaya masikini kuliko zote tanzania na kusini mwa jangwa la sahara? shame on him, hebu mtoa taarifa tujuze taarifa hiyo aliitoa katika mkutano wa waandishi wa habari? au mkutano wa hadhara? hivi kuna mtu alikuwa anamsikiliza kweli?
   
 4. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Litakuwa jambo la busara kama akionesha mfano wa kuwahamasisha vijana wa huko Bunda aliowatukana walipotaka kumuondoa ubunge kuwa ASINGEWAACHIA ubunge kwani ni wavuta bangi!! Akiwahamasisha bila shaka hata hiyo bangi wataacha kuvuta!!
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,910
  Trophy Points: 280
  anatumia pua lake kuwaza
   
 6. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,358
  Likes Received: 6,700
  Trophy Points: 280
  ndo tatizo la kuwaza kwa kutumia moyo!
   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  May 26, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  HTML:
  Alisema kutokana na vijana wengi kutokuwa na ajira za kuwaingizia mapato ndiyo sababu wanachotwa kirahisi na wanasiasa uchwara wanaowahamasisha kushiriki katika vurugu za kile kinachoitwa kudai haki. 
  
  
  Wasira anafikiri kwa kutumia kiuno, anawaza chini ya uwezo wake, amezeeka anakaribia kufa kifo cha asili ikiwa ni matokeo ya kuzeeka .
  IQ yake ni sawa na mtoto wa miaka 9 , na inazidi kushuka, Kikwete akimaliza nae , bila shaka atakua na IQ SAWA na mtoto wa mwaka mmoja, Uelewa wake upo kaputi.
  [​IMG]
   
 8. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Anatumia masikio.
   
 9. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  anatumia makalio
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  hili zee silipendi mungu anisamehe lkn nadhani litakuwa na mwisho mbaya saaaana hili GENDAEKA!!!!
   
 11. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #11
  May 26, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mimi nadhani huyu mzee anakosa cha kuongea.......ushawishi gani huu!
   
 12. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #12
  May 26, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  kuongea anaonea ila tatizo ni hayo anayoongea yanatoka wapi? ni kichwani kweli?

  mimi sidhani kama huyu tunaishi naye tanzania anaweza kuwa anaishi kwenye vitabu vya NYANGWINE AU chenua achebe
   
 13. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  najiuliza kwa hiyo alipotoka kuhutubia aliona ameongea chochote cha kueleweka hapo? vitu vingine bwana kama hakuna chakuongea c unyamaze 2 kwani lazima kusimama kwenye majukwaa na kuhutubia? siipendi ccm lkn vitu kama hivi ndo vinawaonesha watu kuwa hawa ni wao na cc tuko wenyewe. what pumba such a senior minister can utter. aibu kwake, chama chake na watawala wenzake, phuuu!
   
Loading...