Sijui niende kila sehemu beki zimekaba

Sijui niende kila sehemu beki zimekaba

jf user

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
777
Reaction score
625
Habari wanajamvi.
Miaka ya nyuma nilijipaga matumaini kuwa watu wanaomwabudu MUNGU ni safi kumbe wapi kenge nao wamo.
Sisemi kwamba ni wote ila wachache watoe/exception.
Sijui ni utoto au akili finyu ila baadae nilijifunza kitu na kama mnavyojua elimu haina mwisho kwa kila siku mengi yanaibuka.
Huko kanisani wengi hujipa matumaini kumbe kwa bahati mbaya wanaweza pata matumaini yao na at the same time wanaweza kosa matumaini yao.

Wale wahuni, walevi, wasiomwabudu MUNGU na kila aina ya waovu walioamua kuiacha njia ya shetani wapo humo sasa ndugu yangu usijipe matumaini kila mwanamke alieko huko ni msafi!Japo wapo ila wengine wameamua kumrudia MUNGU! Kwa hiyo ukikutana na mauza uza take easy it's normal... usipatwe na bumbuwazi.

Huwa tunasikia malalamiko ya wengi hapa kwamba wamekutana na visivyo na kuishia kutoa lawama hawaji tuu watu wanatubu na wengine wameamua kumrudia MUNGU kwa hiyo kuweni makini popote pale. Ulimwengu umejaa uovu! wema nao wapo ila wachache.
Bahati mbaya sana waovu pia hutumia hiyo njia ya kwa MUNGU kuwaibia na kuwapotosha watu.

Change your mentality ndugu usichukulie vitu kimazoea.
 
Back
Top Bottom