HODII,mimi ni msichana mwenye umri wa miaka kadhaa,yaani umri wangu unaruhusu kuolewa, niliwahi kuumizwa na mapenzi kiasi kwamba sikuwaza kama nitakuja kutamani kuolewa.
Miaka kadhaa imepita karibu minne sijafanya ngono, sasa nimechoka, natamani mwenza angalau na mimi nipate mfariji, sasa nimepata boyfriend hajajitambulisha home siwezi kumuita mchumba.
Tatizo huyu kaka hanijali hata kidogo niliwahi kupata tatizo nikamuomba elfu 5 tu ya kitanzania yaani alinifokea kama mtoto mdogo eti mimi napenda pesa, sasa nikamchoka.
Nimepata mwingine bado hatujazoeana, sielewi kama na yeye mbahili au vp, je ni sahihi kumuacha yule wa kwanza na kuwa na huyu mpya au nimefuata matatizo zaidi?
Naombeni ushauri