Sijui ni ushamba au ni nini?

karume kenge

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
573
500
Habari zenu wakuu,

Mimi kifupi hua najishangaa sana najiona labda niko tofauti na wenzangu, sijali hata siku yangu ya kuzaliwa na mara nyingi hua inapitiliza hata bila kujielewa sina starehe yeyote sio mtu wa disco, beach, sinywi pombe, sivuti sigara, sipendi kula kula sipendi kila papuchi.

Kifupi sijui napenda nini kunasiku jamaa yangu mmoja alinipeleka sehemu walikuwepo hawa wanamuziki wa kizazi kipya ukweli niliyoyaona nikaapa sirudi tena ni upuuzi mtupu.

Nikawa nawaza naona wenzangu wanacheza na kufurahi, nikajiulizaaa pesa nitoe mimi na ku cheza nicheze mimi huku si kujichosha bure, bado tunaambiwa mikono juu mikono kama mateka wa kivita dah iliniuma saana.

Mara tuimbe wote kwa pamoja sasa wewe msanii au sisi wasanii iliniuma sana kukosa usingizi wangu, sijawahi kurudi tena.

Sasa wadau sijui mimi mshamba au mana sisi wasukuma huitwa washamba kila sehemu.
 
Uso wa nyoka

JF-Expert Member
Mar 17, 2014
4,798
2,000
Kwenye birthdays na club, hauko peke yako, wengine huwa tunakumbushwa na wake zetu. Birthday pekee nayoikumbuka bila kukosa nivya Baba yangu, huyu jamaa huwa nakumbuka sana siku yake ya kuzaliwa maana namjali sana. Kanitoa mbali sana na ni msingi wa kila nachokijua.
 
essaugervas

JF-Expert Member
Jun 25, 2016
586
250
habari zenu wakuu mimi kifupi hua najishangaa sana najiona labda niko tofauti na wenzangu, sijali hata siku yangu ya kuzaliwa na mara nyingi hua inapitiliza hata bila kujielewa sina starehe yyt sio mtu wa disco beach sinywi pombe sivuti sigara sipendi kula kula sipendi kila papuchi kifupi cjui napenda nini kunasiku jamaa yangu mmoja alinipeleka sehem walikuwepo hawa wanamuziki wa kizazi kipya ukweli niliyo yaona nikaapa sirudi tena ni upuuzi mtupu nikawa nawaza naona wenzangu wanacheza na kufurahi, nikajiulizaaa pesa nitoe mimi na ku cheza nicheze mimi huku si kujichosha bure bado tunaambiwa mikono juu mikono kama mateka wa kivita dah iliniuma saana maraa tuimbe wote kwa pamoja sasa ww msanii au sisi wasanii iliniuma sana kukosa usingizi wangu cjawahi kurudi tena sasa wadau sijui mimi mshamba au mana sisi wasukuma huitwa washamba kila sehem
safi mkuu sana kiongozi endelea na hyo hyo tabia,,tabia zingine zinapelekea matumizi ya pesa kua mabovu,,upo sawa na mm mkuu mm starehe yangu ni kucheki movie,,na mpira
 
Hongera mkuu bora kupunguza matumiz ambayo hayana maana
 
Uso wa nyoka

JF-Expert Member
Mar 17, 2014
4,798
2,000
safi mkuu sana kiongozi endelea na hyo hyo tabia,,tabia zingine zinapelekea matumizi ya pesa kua mabovu,,upo sawa na mm mkuu mm starehe yangu ni kucheki movie,,na mpira
Yangu ni kusaka pesa, kuhesabu noti zangu na kubuni njia mpya za kuzitengeneza. Hakuna kitu nachokipenda kama mlio wa ATM machine ikiwa inaanza kutoa pesa zangu au ninapoamka asubuhi nikiwa na ahadi ya kwenda kupokea pesa.
 
masopakyindi

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
14,793
2,000
habari zenu wakuu mimi kifupi hua najishangaa sana najiona labda niko tofauti na wenzangu, sijali hata siku yangu ya kuzaliwa na mara nyingi hua inapitiliza hata bila kujielewa sina starehe yyt sio mtu wa disco beach sinywi pombe sivuti sigara sipendi kula kula sipendi kila papuchi kifupi cjui napenda nini kunasiku jamaa yangu mmoja alinipeleka sehem walikuwepo hawa wanamuziki wa kizazi kipya ukweli niliyo yaona nikaapa sirudi tena ni upuuzi mtupu nikawa nawaza naona wenzangu wanacheza na kufurahi, nikajiulizaaa pesa nitoe mimi na ku cheza nicheze mimi huku si kujichosha bure bado tunaambiwa mikono juu mikono kama mateka wa kivita dah iliniuma saana maraa tuimbe wote kwa pamoja sasa ww msanii au sisi wasanii iliniuma sana kukosa usingizi wangu cjawahi kurudi tena sasa wadau sijui mimi mshamba au mana sisi wasukuma huitwa washamba kila sehem
Una tatizo kubwa sana la Social Deficiency Disorder(SDD).
Kunywa bia mbili asubuhi, mbili mchana na mbili usiku.
Usinywe dawa aina ya kiroba-hiyo ni kali na itakupelekesha.
Utapona tu.
 
Uso wa nyoka

JF-Expert Member
Mar 17, 2014
4,798
2,000
Hongera mkuu bora kupunguza matumiz ambayo hayana maana
Ndiyo maana yake. Mambo mengine ni kujipotezea muda na rasilimali tunazotafuta.
Mimi nikiwa na hamu ya kujiliwaza, naweza kuchukua watoto wangu na kwenda nao beach au kuchinja mbuzi na kualika ndugu na marafiki bila sababu yoyote. Siku hiyo nitanunua vinywaji na chakula kitapikwa na tutazungumza mpaka basi tukiburudika na mziki.
Sipendi kucomplicate mambo na swala la Club, sijawahi kulipenda kabisa.
Kuna wakati Nilikuwa kwenye kanchi fulani ka jumuiya ya schengen ambako club ni kama utamaduni wao. Nikaokota mdada mmoja wa kizungu ambae club ilikuwa kama dini kwake, aisee Niliona kama adhabu. Maana mnajirusha karibu kila siku na hakubali ubaki home peke yako kwa kuhisi utatongoza majirani, basi maisha yalikuwa pombe, club, club,pombe. Sitasahau.
 
Dah pole sana mkuu
 
karume kenge

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
573
500
Sababu inaonekana unakimbia sehemu za matumizi
I nawezakana kweli labda nikawa cna pesa mkuu lakin najiuliza au fuatilia wengi wanao penda mambo hayo ni wa kipato cha Kati kama mimi na wengine hawana kabisa mkuu
 
Flexi lady

JF-Expert Member
Nov 14, 2014
281
250
habari zenu wakuu mimi kifupi hua najishangaa sana najiona labda niko tofauti na wenzangu, sijali hata siku yangu ya kuzaliwa na mara nyingi hua inapitiliza hata bila kujielewa sina starehe yyt sio mtu wa disco beach sinywi pombe sivuti sigara sipendi kula kula sipendi kila papuchi kifupi cjui napenda nini kunasiku jamaa yangu mmoja alinipeleka sehem walikuwepo hawa wanamuziki wa kizazi kipya ukweli niliyo yaona nikaapa sirudi tena ni upuuzi mtupu nikawa nawaza naona wenzangu wanacheza na kufurahi, nikajiulizaaa pesa nitoe mimi na ku cheza nicheze mimi huku si kujichosha bure bado tunaambiwa mikono juu mikono kama mateka wa kivita dah iliniuma saana maraa tuimbe wote kwa pamoja sasa ww msanii au sisi wasanii iliniuma sana kukosa usingizi wangu cjawahi kurudi tena sasa wadau sijui mimi mshamba au mana sisi wasukuma huitwa washamba kila sehem
Sio mshamba ila ni mazingira uliyokulia, kifupi uwe tu na furaha ya moyo basi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom