Sijui ni mimi tu au kuna wengine pia?

Sijui ni mimi tu au kuna wengine pia?

Joel360

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2013
Posts
986
Reaction score
657
Jamani mimi hata mwanamke awe mzuri namna gani, kama anachonga/ananyoa/anapunguza nyusi lazima anishinde. Sipendi kuona nyusi za mwanamke zimechongwa.

Yaani niko tayari kumvumilia mwanamke mchafu, mvaa mawigi, muweka mikope ili mradi tu hachongi nyusi. Siku hizi najitahidi sana ninapozungumza na mwanamke simkazii fikra kwenye nyusi ili nisikereke na nisimkere na yeye. Nikitizama nyusi tu nikaona zimekatwa katwa/zimepunguzwa/zimechongwa basi naahindwa hata kuendelea kuongea nae.

Baadhi yao (majirani) washanishtukia maana nikiongea nao siwatazami usoni. Hapo naondoka na "jioni nikiwa free ntakutafuta"

Niliwahi kumpenda mwanamke kwa sababu moja tu: HAPENDI KUCHONGA NYUSI ZAKE, na nilidumu nae sana, nikataka nifunge nae ndoa ila tu alikuwa wa imani na mtazamo tofauti ikashindikana.

Hata hivyo, yawezekana ni mimi tu ila kuna wanaume wenzangu wanapenda mwanamke akate kate nyusi au hawajali kabisa kuhusu hilo ila binafsi nimeshindwa kupuuzia. Namwambiaga mke wangu ajae (japo sijamjua), "ukichonga nyusi tutashindwa kutazamana usoni kabisaaa".

Sorry kwa ambao nimewakera ila ni mtazamo tu.

Kuna wale ndugu zangu watakaohisi labda nikikua nitabadilika, Kwa sasa nipo kwenye early 30, nimeshakuwa na nnazeeka sasa hivi ila hii tabia bado nnayo toka niko 19.
 
Binafsi zivutiwi na hilo.
Ni kitu cha kawaida kwa kuwa binadamu hatufanani, so kila mtu anamachagu yake.
Kw mfano: mimj sipendi mawigi napenda nyele ziwe zake. So ni machaguo tu sio lazima wote tufanane
 
ndo mnasemaga hivi mkiwa hamna hela ngoja mzipate ooh sura ya baba yanini?
FB_IMG_16454787876789262.jpg
 
Binafsi zivutiwi na hilo.
Ni kitu cha kawaida kwa kuwa binadamu hatufanani, so kila mtu anamachagu yake.
Kw mfano: mimj sipendi mawigi napenda nyele ziwe zake. So ni machaguo tu sio lazima wote tufanane
Kweli ndugu yangu, binadamu tumetofautiana.
 
Mmehamia kwenye nyusi
kwahiyo unapenda nyusi natural zimejaa kama kichaka cha wanyang'anyi
Yaaani natural.

Ziachie uone jinsi utakavyopendeza.

Ila dada zangu mi huwa nawashangaa. Mna vitu vingi vya kuviremba, mna nywele, pua, maskio, mdomo, lakini hamjaridhika mkaamia mpaka kwenye nyusi.
 
Jamani mimi hata mwanamke awe mzuri namna gani, kama anachonga/ananyoa/anapunguza nyusi lazima anishinde. Sipendi kuona nyusi za mwanamke zimechongwa.
Tuko ila kila mtu anachake,mie tako ndio kila kitu....ambae hana hilo kwa kweli hata mkono simpi.
 
Back
Top Bottom