Sijui mtego huu?

Sijui mtego huu?

Anaweza asiniamini...akampigia simu rafiki yake nae akimkatalia kasheshe lingine

Basi ktk hio story yako engezea kipengele cha kurecord conversation yenu mukikutana tena...
otherwise kafanye kazi saivi ujenge taifa...
 

Najua umeharibu gari yangu umevunja taa sitaki ununue ila nataka uwe mpenzi wangu,yalinitoka macho nikaropoka we si unajua nina mchumba wangu ambae ni rafiki yako akijua!? Akajibu kwa jeuri "utamwambia wewe" kama hutaki lipa.Nikipiga hesabu na hela saivi ilivyonipiga chenga taa ya mark x na fundi rangi lazima 1 mil vinitoke nikamwambia aniache nikajifikilie akasema kesho yaani leo anataka jibu na saivi kanipigia na kuniambia nimkute hotel flani.Sasa kinachoniuma ni usaliti kwa mpenzi wangu afu niliapa sitamsaliti mbele ya huyo huyo anaetaka nikamsaliti
na ki uchumi saivi siko vizuri sana. Au mtego yaani ananivuruga huyu mdada.

Nipeni ushauri

Nawasilisha kwenu wana Jf

Assuming ni kweli: Kosa namba moja ulilofanya ni hilo hapo (bold, red). Kuanzia hapo ilionekana kuwa tatizo kubwa kwako si kutembea naYe (kumsaliti mchumba wako) bali wasiwasi tu kuwa mchumba wako atajua. Kuanzia hapo ndio maana akakujibu kuwa labda utamwambia wewe, ili "kukutoa wasiwasi".

Inaelekea makuzi yako hayakuwa kipindi kile ambacho kutongoza ilikuwa mtihani mzito. Maana ulitegemea matusi au maneno makali sana ukimtamkia msichana habari za mapenzi enzi hizo especially kijijini. Na vitisho vya kwenda kushitaki nyumbani kwao au hata kwenu ukiendelea, jambo hili lilikuwa linakufanya uogope, na uwezekano wa kumtokea tena ulikuwa mdogo.

Ukiona msichana anadai anaogopa mama yake atajua, au aliambiwa na mama yake au dada yake kuwa ataumia, na vijisababu vingine vya namna hiyo ulikuwa unajua moja kwa moja huyo umempata maana kazi kwako ni kumridhisha kuwa anachokihofia hakitatokea.

Kama kweli story yako, na kama kweli huna mpango kula huo mzigo ambao umeshaanza kuusifia kuwa ni zaidi ya mkeo, lipa gharama.

BY THE WAY, GARI YAKO HAINA INSURANCE, HATA THIRD PARTY?
 
Utotole Ahsante mkuu kwa kutia neno kwani nimeona pale kwenye Red (akijua)ndio panapompa jeuri.
bima yangu ni third party siwezi kulipwa.
 
Last edited by a moderator:
Ahsante mkuu kwa kutia neno kwani nimeona pale kwenye Red (akijua)ndio panapompa jeuri.
bima yangu ni third party siwezi kulipwa

Kwani unataka kulipwa wewe au huyo uliyemgonga? Kwani bima third party maana yake nini na inahusikaje kwenye matukio ya ajali. Nilidhani inakusaidia wewe ukisababisha ajali, kusaidia kukulipia gharama kwa mtu mwingine ambaye otherwise ilitakiwa umlipe wewe. wenye kujua zaidi wakusaidie maelezo sahihi kuhusu hili.
 
ungemrekodi akat anakwambia af mckilizishe mchba ako... chakufanya mwambie utmlipa kopa kokote umpe af mazoea ndo yaishie hapo. be a man la cvyo atakupelekesha sana ukimkubalia ataendeleza huo mchezo mwisho wa cku atataka umuoe yeye.
 
mwanaume mzima unadrive gari huna hata milioni ya akiba

Inawezekana we unapanda bajaji au daladala, alafu bado unaona anaeendesha gari hana million mfukoni, kwanza anaetembea na million mfukoni kwa wakati huu hajielewi, vinginevo unajambo la msingi unaenda kufanyia, lakini kutembea nayo kwa fashion tu itaishia ktk pombe, au corner bar, kama gari ina full tank una 20,000 mfukoni inatosha jamani acheni mbwembwe za kutembea na million mfukoni wakati nyumbani umeacha 7,000 ya mboga
 
Back
Top Bottom