Sijui lini nitakuja kufika Dar!?

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,835
Mpaka leo Dar huwa naisikilizia tu kwenye TV na magazeti

Mara wengine wanakwambia Dar maisha magumu kweli huwezi toboa kirahisi.

Maji ni ya kununua na hakuna usawa mara matajiri wanaishi Masaki na masikini Bunju mara Tandale...

Wengine wanasema Dar ni raha tupu natamani nije kufika nijionee ninayoambiwa.

#Iam Zagarino
 
Kijana mbona kama umedata. Ndani ya lisaa umeshafungua nyuzi kama 5 hivii.

Screenshot_20200811-190018.jpg
 
Wa Dar na wenyewe wanatamani kuishi mikoani, hakuna raha kama mikoani bwana, jam hakuna, hali ya hewa swafi. Labda kibiashara hapo sawa+Mwanza, mbeya, dodoma na Arusha.
 
Dogo inaonekana alitenga kibubu kwa ajili ya kununua smartfone,hongera na karibu
Hapana mkuu Ila threads ninazodondosha natumia kama way of learning
Anyway nimejoin JF 26 July 2020 so bado I'm a newcomer mnivumilie
 
Mimi nilienda Dar nikiwa kichanga na mama mwaka 1978..

Pamoja na hayo yote najua Uwanja wa taifa upo Temeke.
Uwanja wa fisi ndiyo zimbo la Machangu plus Buguruni acha wale wa Sinza.
Gari za Gongo la Mboto na Mbagala ni Coaster ambazo ili upande hasa mida ya jioni ujipange.
Ubungo terminal na Mbagala terminal ni zaidi ya stendi za magari.
UDSM majengo baadhi yamechoka ila library waliyojenga now ni moto.
Wasafi ipo Mbezi pamoja na E FM
Tbc Fm ipo TAZARA but ofisi kubwa zipo Mikocheni ambako ITV, EA Radio, Radio Maria na zingine zipo huko.
Ukitaka kwenda kigamboni unaweza kupita kule feri au ukavuka daraja la Nyerere.
Mlimani City ni bonge la hall lenye huduma kibao yaani kwa Mwanza ni kama Rock City Mall.
Tandika kuna wadada na wamama wamepanga nyumba wakijiuza kama barafu.


Hapo nilienda nikiwa mtoto mchanga sijui nikifika leo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom