Sijui kwanini naogopa sana nyoka

teledam

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
927
1,239
Habari zenu wadau/washikadau
Kuna huyu mdudu anaitwa nyoka nikimuona huwa nashituka kama nadondoka kwa shimo la futi mia. Awe mdogo Mkubwa mkali ama hawa wanaoitwa kibisa yani nashituka vibaya. Naweza kushambulia ingawaje kwa ujasiri mdogo sana, sasa toka juzi nimefika hapa Gomba kila siku lazima nikutane na joka yani utafikiri wanajua nawaogopa. Kwa hofu niliyonayo kwa nyoka nahisi ntapata bp aisee, kwa sababu kutoka hapa ni baadae sana kila nikikaa alone zinakuja mapicha majoka..nimechoka manzee
 
Wewe ni me?Umeoa mkuu? sasa kama unaogopa wife itakuwaje? anyway nyoka ni mboga tu na akikuuma sio kifo cha papo hapo kuna dawa nyingi tu. Ni menu tamu sana nilikua sijui mpaka nilipokula bila kujua China, na nikawa naagiza kabisa lete msosi "snake in the monkey's shadow"
 
Hata nikikuta mzoga mahali nasisimka kinoma. Wewe hadi kula umekula,Ila nafikiri hukujua kama ni nyoka kabla
 
'Amphibians' wanaitwaje kwa kiswahili? Tusaidiane

hata bibi alikuwa binti.
nyoka ni reptilia mkuu sio amfibia.
nyoka huwa wanaogopa watu zaidi ya wewe isipokuwa chatu tu.
pia usijifanye mjanja kumuua nyoka kabla hujajua ni nyoka gani au hauna ujuzimaana wengine wakikuuma kama ukikosea timing dakika 30 ni nyingi utakuwa hayati wa JF.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom