knows
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,453
- 2,237
Habari wana JF, natumaini wote wazima, niende kwenye mada moja kwa moja.
Kiukweli nipo na mke wangu nampenda sana mke wangu na tunaishi vizuri tu. Mwezi huu umeanza nashukuru Mungu mke wangu ni mjamzito, na nilimpeleka hospital akapima kweli ni mjamzito wote tukafurahi kwa hilo maisha yanaendelea.
Lakini sielewi nimepatwa na nini, yaani kila siku zinavyozidi kwenda najikuta nimepatwa na hali ya kumchukia mke wangu. Sielew hii hali inatokana na nini, wakati yeye mke wangu ndiyo upendo umezidi hatari, ananipenda sana. Nashangaa sana wakati yeye ndiyo mjamzito, yaani hata nikiwa kazini siku hizi amekuwa muda wowote anapiga simu, yaani nikiona tu simu yake hali yangu inabadilika.
Siku hizi hata kurudi nyumbani najikuta nachelewa kidogo ili nikute kashapumzika, basi nikifika nilale tu tutaonana asubuhi. Na kashaanza kugundua hali yangu hii lakini anabaki akijiuliza kwanini? kiukweli mke nampenda lakini hii hali imekuja tu ghafla baada ya ujauzito wa mke daah.
Wakuu embu niambieni hii imekaaje kitaalamu zaidi na inauhusiano wowote na mimba ya mke wangu? Karibuni wataalamu labda mnaweza nishauri nifanye kitu au labda ni hali tu ya muda itaisha au ni vipi?
Mungu awabariki.