Sijui kiingereza, nimlaumu nani?

Sijui kiingereza, nimlaumu nani?

Pamoja na kupata Shahada ya Chuo Kikuu kwa mkopo toka HESLB bado kiingereza changu kina UKUNGU na ulimi bado mzito ajabu. Napata kigugumizi kikali nikijaribu kuongea kiingereza. Lawama nimtupie nani kati ya hawa?
1. Baba wa Taifa; kwa kuamua kiswahili iwe lugha ya taifa;
2. Mzazi wangu kwa kunipeleka shule za kayumba;
3. Mwalimu wangu wa Shule ya Msingi Muungano;
4. Ama NIJILAUMU mwenyewe kwa kutojibisha kupata maarifa kwa lugha Tajwa? kutwa kusoma migazeti ya udaku kwa kiswahili, na aina ya marafiki nilionao wasio leta changamoto yoyote.
5. Waziri mwenye dhamana!!!
Ungeandika kingereza basi!
 
Duuh..mleta post amejaribu kuwa sarcastic..."eti Ama NIJILAUMU mwenyewe kwa kutojibisha kupata maarifa kwa lugha Tajwa? kutwa kusoma migazeti ya udaku kwa kiswahili, na aina ya marafiki nilionao wasio leta changamoto yoyote". hahah..anyway, kwa graduate kutojua lugha ni tatizo kidogo. Nina ushauri kwako, don't let the past destroy you...bse there is an answer for everything. amka, songa mbele.. nenda british council, waelezee shida yako and be teachable. Hutojutia ndugu. kuwa tayari kujifunza na ukubali kuanza upya kama ulivyokuwa unaanza form one zama hizo...wish you luck
 
Pamoja na kupata Shahada ya Chuo Kikuu kwa mkopo toka HESLB bado kiingereza changu kina UKUNGU na ulimi bado mzito ajabu. Napata kigugumizi kikali nikijaribu kuongea kiingereza. Lawama nimtupie nani kati ya hawa?
1. Baba wa Taifa; kwa kuamua kiswahili iwe lugha ya taifa;
2. Mzazi wangu kwa kunipeleka shule za kayumba;
3. Mwalimu wangu wa Shule ya Msingi Muungano;
4. Ama NIJILAUMU mwenyewe kwa kutojibisha kupata maarifa kwa lugha Tajwa? kutwa kusoma migazeti ya udaku kwa kiswahili, na aina ya marafiki nilionao wasio leta changamoto yoyote.
5. Waziri mwenye dhamana!!!

Unapata kigugumizi ukijaribu kuongea Kiingereza wapi? Unaongea na nani? Umemsikia nani anaongea hana kigugumizi?

Au ungependa kujua Kiingereza ili ukaongee wapi, kitaa? Bungeni? Kanisani? Kwenye daladala? Au unafanya ulinzi kwa mzungu na huyo mzungu unaongea nae nini saa ngapi?
 
Pamoja na kupata Shahada ya Chuo Kikuu kwa mkopo toka HESLB bado kiingereza changu kina UKUNGU na ulimi bado mzito ajabu. Napata kigugumizi kikali nikijaribu kuongea kiingereza. Lawama nimtupie nani kati ya hawa?
1. Baba wa Taifa; kwa kuamua kiswahili iwe lugha ya taifa;
2. Mzazi wangu kwa kunipeleka shule za kayumba;
3. Mwalimu wangu wa Shule ya Msingi Muungano;
4. Ama NIJILAUMU mwenyewe kwa kutojibisha kupata maarifa kwa lugha Tajwa? kutwa kusoma migazeti ya udaku kwa kiswahili, na aina ya marafiki nilionao wasio leta changamoto yoyote.
5. Waziri mwenye dhamana!!!
Mlaumu aliekuwa anakubeba kwenye result za shule
 
Unakitaka cha nini? ulimi wetu sio wa kizungu,tutazungumza hivyohivyo tuu kama hawatuelewi basi
 
Kwani lazima kukijua mkuu?
kama kigumu jifunze hata spanish.....
lazima kitushinde kwasababu ya Lafudhi yetu.... na muda mwingi tunasoma & kuandika kingereza, wala sio kuongea.
ndio maana tunaweza zaidi kusoma na kuandika.

ukizingatia sisi sio wale wa "dady" "momy"
 
Hapo mkuu , nikujilaumu wewe mwenyewe , kwani hukuzingatia somo hilo shuleni na hayo ndio madhara yake sasa,
 
Back
Top Bottom