Sijui kama nitapata mpenzi kama huyu tena. Ameniachia mateso makubwa sana

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,982
Mwaka jana tulikuwa kikazi mkoa flani katikati ya pori. Mimi na wenzangu kadhaa. Tulikuwa tumeenda na tents na vyakula, maji na mahitaji yote muhimu maana tulikaa kwa muda wa week 6.

Huyu dada mzuri sana nilianza fahamiana naye huko na ilitokea yeye alipanda gari niliyopanda mimi. Nikampa uhuru wa kunilalia au kuniegemea kila alipohitaji.

Kifupi nlimdekeza sana na ni mdada ambaye alitokea kunizoea na kuonekana kunipenda sana ikawa hivyo njiani tunashuka wote, tunaenda kila sehemu wote mpaka porini akaomba tent yake nimfungie karibu na yangu.

The dada alikuwa mzuri sana, ila mkimya but mwenye tabasamu kila mara. Siku ya kwanza nakumbuka imefika around saa nne usiku anasema nimsindike akajisaidie haja kubwa.

Alitamka bila woga kama mtoto anavyomwambia baba yake, nlibeba kijikoleo akachukua tishue na maji kwenye chupa tukaondoka kwenda sehemu ya mbali kidogo maana hamna vyoo. Giza lilikuwa kubwa, akachuchumaa nyuma yangu na kuanza jisaidia. Nlipotaka kuondoka kusogea mbali alinikatalia na kunambia tu nigeukie kule nsimwangalie atashindwa jisaidia.

Kule niliposimama ndo upepo ulikuwa unakuja toka kwake, akanambia "ondoka huko simama huku maana harufu itakujia huko nawe unaona aibu kuikimbia"

Nlicheka sana kwa jinsi dada alivyokuwa huru, nlianza mpenda maana kweli alikuwa huru sana kwangu. Hali hii ikaendelea kiasi watu walianza amini nina mahusiano naye.

Yule dada ilikuwa kama chakula atanipakulia. Atanibebea kuniletea atanitunzia somethings. Yaani nikitoka kama nimemwacha kambini nikirudi anakuwa na furaha sana. Ataniletea maji ya kunawa n.k

Tuliendelea hivi mpaka sometimes anaweza akaamua usiku aje kulala mwenye tent langu akidai anaogopa but alikuwa makini sana ktk kila kitu alichofanya, alifanya kama rafiki.

Nlikuwa napata wakati mgumu sana na kuna wakati nikisimamisha anafanya kama anaichapa mashine "acha ujinga wewe lala..." Basi baada ya hapo ananikumbatia yeye analala mimi nabaki tu naumia.

Huyu dada tuliendelea hivi tukiwa na mapenzi sana. Nikimtizama dada mwenyewe nlikuwa nashindwa elewa. She was so pretty sura na umbo pia. Muda wote huo porini hatukuwahi fanya kitu.

Tukarudi mjini akawa anaendelea kunitafuta na kunisalimia na siku moja nakumbuka Jumamosi aliniomba siku nzima achukue muda wangu, nilimkubalia akaja nichukua akiwa na gari yake tukaenda Amref kupima HIV/AIDS. Alianza yeye na pia akaniuliza kama nami nipo tayari, sikuwa na shaka maana week moja nlipima nikawa negative, tukapima sote.

Akafurahi na tukaondoka yeye akiendesha kuelekea Hotel moja akinambia twende tukale, aliniacha ameagiza kinywaji na kupotea kisha baada ya dk chache alirudi na kubeba kinywaji changu akataka nimfuate.

Ndio ilikuwa siku ya kwanza kufanya naye mapenzi, dada alikuwa mzuri akinielekeza nifanye naye taratibu na kwa vituo. Tuli enjoy sana tukifanya mapenzi kwa hisia na taratibu sana.

From there tukawa wapenzi mpaka siku alipokuja nambia ana matatizo ya moyo ambayo nijiepushe nisimpe stress, nimpende na kumheshimu the way she does.

Last week nlipata simu toka kwa rafikiye akiwa analia, alinambia xxxxx amefariki ghafla baada ya kuwahishwa hosp. Nililia sana kumpoteza dada yule mzuri tuliyependana ndani ya muda mfupi sana. Alinibadilisha sana nlianza kutotamani kabisa wanawake wengine.

Nlikuwa namwona yeye everytime, nilijawa na hisia ambazo sikuwahi kuwa nazo. I loved her and she made me love her more. Leo hii hayupo nami tena. Nani atanambia nimnawishe baada ya kwenda haja ndogo? Nani atadeka kwangu na kunidekeza the way she did?

Huyu dada iliweza kuni control kwa mapenzi na kunifanya alivyotaka niwe. Nlishazoea kuchaguliwa chakula na kinywaji. Nlishazoea kuchaguliwa nguo za kuvaa, aliuchukua uhuru wangu na kunipa wake. Tulifahamiana ndani ya muda mfupi sana.

Naumia naandika uzi huu kwa machungu, niliamini nimefika kwake. Nasikitika sasa nagundua safari bado. Kinachoniuma ni kuwa pengine nisipate mwanamke wa aina yake tena. Why alinitengenezea delicate heart katika mapenzi na sasa ameniacha peke yangu porini? Siku zote alikuwa akinambia hawezi enda popote bila kuniaga. This time katika maisha yake amedanganya. Hakuniaga.
 
FB_IMG_1610129629774.jpg

Pole maana alikufanya uone dunia ni yako na yeye
 
Dah pole Sana mkuu

Lia hadi machungu yaishe.

Usikurupuke kuingia kwenye mahusiano kwa Sasa kwa kuwa utamuumiza utakayekuwa nae, niamini Mimi hutampenda Ila utamtumia tu kupata faraja

Ukipata faraja na ukiwa sawa utagundua ulikosea kuchagua, lakini pia utakuwa unamlinganisha Sana na utagundua kasoro nyingi kiasi hutafurahia hayo mahusiano

Lia uwezavyo, tafuta njia ya kupata faraja Ila sio mahusiano mapya
 
Dah pole Sana mkuu

Lia Hadi machungu yaishe.

Usikurupuke kuingia kwenye mahusiano kwa Sasa kwa kuwa utamuumiza utakayekuwa nae, niamini Mimi hutampenda Ila utamtumia tu kupata faraja

Ukipata faraja na ukiwa sawa utagundua ulikosea kuchagua, lakini pia utakuwa unamlinganisha Sana na utagundua kasoro nyingi kiasi hutafurahia hayo mahusiano

Lia uwezavyo, tafuta njia ya kupata faraja Ila sio mahusiano mapya
Sure hata mimi nimekuelewa sana mkuu, zingatia hichi sana mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom