Sijui kama ni sehemu sahihi, lakini naomba hii imfikie Waziri wa uchukuzi.

GAGL

JF-Expert Member
Aug 5, 2010
390
395
Mhe. Waziri wa uchukuzi Dr. Mwakyembe nakumbuka uliwahi kufanya ziara ya kustukiza pale ubungu bus terminal na ukagundua madudu katika suala la nauli, sasa tunakuomba uyageuzie macho yako magari yanayokwenda lindi na mtwara. Hawa jamaa nauli ya lindi na mtwara ni moja, kwa hiyo anayeishia lindi anatakiwa kulipia zaidi ya km 100 ambazo hazisafiri, hii si haki. Tafadhari ingilia kati suala hili, tunaonewa sisi tunaoishia lindi, kwanini nauli isiwe pungufu ya ile ya mtwara.
 
Route za huko magari yanahesabika wakigoma mtaweza kutembea au kupiga mbizi.? Hamia Airtel ambako ni Dar, Mwanza, Mbeya au Moro magari unajichagulia km ya kwako, dah mikoa hii raha kweli welcome. Ila pole.
 
Mhe. Waziri wa uchukuzi Dr. Mwakyembe nakumbuka uliwahi kufanya ziara ya kustukiza pale ubungu bus terminal na ukagundua madudu katika suala la nauli, sasa tunakuomba uyageuzie macho yako magari yanayokwenda lindi na mtwara. Hawa jamaa nauli ya lindi na mtwara ni moja, kwa hiyo anayeishia lindi anatakiwa kulipia zaidi ya km 100 ambazo hazisafiri, hii si haki. Tafadhari ingilia kati suala hili, tunaonewa sisi tunaoishia lindi, kwanini nauli isiwe pungufu ya ile ya mtwara.
Kabla ya yote unatakiwa kujua nauli halisi inayotolewa na SUMATRA.
Nikutolee mfano: unaweza kukuta nauli halisi ya kutoka Dar kwenda Mtwara ni 35,000/=(sijui kama sawa)
Na wale wa Lindi labda tuseme nauli kwa viwango vya sumatra yako 30,000/=(sijui kama sawa)
Wafanyabiashara kwa kuangalia ushindani na ukosefu wa abiria wao wakatoza 25,000/= kwenda Mtwara, iwe unashuka Lindi nauli hiyo hiyo.

Sasa hapo Mwakyembe akusaidie nini? au awasaidie wasafirishaji wasiwasaidie kupunguza nauli?
We unaishangaa hiyo km 100, Mwenzio anatoka Mwanza nauli 45,000/= mpaka Dar, anaeshuka Moro nae analipa 45,000/=
Dar Moro km ngapi?

Back
Top Bottom