GAGL
JF-Expert Member
- Aug 5, 2010
- 390
- 395
Mhe. Waziri wa uchukuzi Dr. Mwakyembe nakumbuka uliwahi kufanya ziara ya kustukiza pale ubungu bus terminal na ukagundua madudu katika suala la nauli, sasa tunakuomba uyageuzie macho yako magari yanayokwenda lindi na mtwara. Hawa jamaa nauli ya lindi na mtwara ni moja, kwa hiyo anayeishia lindi anatakiwa kulipia zaidi ya km 100 ambazo hazisafiri, hii si haki. Tafadhari ingilia kati suala hili, tunaonewa sisi tunaoishia lindi, kwanini nauli isiwe pungufu ya ile ya mtwara.