Sijielewi

Nyakwaratony

JF-Expert Member
Dec 21, 2011
574
195
Asalaam Aleikum!
Bwana Yesu asifiwe!

Nilimpenda sana kaka mmoja aliyekuwa mwalimu wangu, kumbe na yeye kwa wakati huo alikuwa ananipenda ila hakutaka kuniambia. Tuliheshimiana sana pia tulikuwa marafiki sana. Baada ya kumaliza chuo niliondoka mkoan hapo lakini nawasiliano yaliendelea, hapo ndipo alipoanza kusema lake la moyoni.

Woooh, nilifurahi sana na kujisemea moyoni ulikuwa wapi? mawasiliano yaliendelea kuwa mazuri zaidi na zaidi, baada ya mwaka nilikwenda kumtembelea ila sikufika anapoishi kwani nilihisi kwa jinsi ninavyomfeel na yeye anavyonifeel tunawezajikuta tumeishia kubanjuja. Nilifanya hivyo kila mwaka nilipopata likizo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Tulizungumza mambo mengi hasa kuhusu kuanzisha familia na alionekana kukubali,mwaka wa nne tulianza mapenzi rasmi nikiamini kuwa tunaelekea kuanzisha familia kwani ni muda tosha wa kusomana tabia (hayo ndio yalikuwa mawazo yangu) baada ya miezi minne ya mapenzi motomoto alianza kubadilika, mara hapatikani siku nzima ukimuuliza anadai simu haikuwa na charge, mara line iliblock na sababu chungu nzima.

Kwa vile sikuwahi kufika kwake niliamua kufunga safari na kwenda mpaka ofisini kwake, nilichoambiwa ni kwamba kasafiri kwenda mkoani anakaribia wiki, kabla ya hapo alikuwa na wiki nzima hapokei wala kujibu sms zangu na hatukuwa tumegombana. Nilichukia na kumuandikia sms kali ya kusitisha uhusiano. Nahisi alishukuru sana kwani hakujibu kabisa. Na uhusiano tulikuokuwa tumeudumisha kwa muda wa miaka minne ukaishia hapo....

Ilikuwa ni mwezi wa tano tangu nimeachana na huyo kaka. Ilipofika mwezi wa nane nilipigiwa simu na kaka mwingine niliyesoma nae course flani miaka ya nyuma, wakati tunasoma alinidatilia sana ila sikumkubalii. Alinikaribisha kwake nikamuhaidi ningeenda wiki iliyofata, kweli nilienda tuliongea mambo mengi hatimaye tukaanza uhusiano, baada ya mwezi tukapeana maraha. Kiukweli ndani ya mwezi kabla ya ku-do alinicare sana. Outing kibao, shopping za kufa mtu n.k.

Ila baada ya ku-do tu mapenzi yalipungua hatimaye nilimchukia sana na mapenzi yakaisha. Huyu wa mwisho sasa yeye nilimzungusha kwa muda wa miezi sita baadaye nikaamua kujilipua nikampa tundi... Weee yan yeye alikuwa akijisikia ndio ananitafuta "wewe uko wapi nikufate" akinifata ni direct kwake ku-do tu. Baada ya hapo anaweza asipokee simu au asijibu sms. Na ikitokea kajibu jua kuwa anahitaji. Ukisema basi tutoke tukazungumze kuhusu mahusiano yetu anadai yupo busy.

Je nifanyeje, mapenzi kwangu yamekuwa shubiri, ni miezi miwili sasa mawasiliano yamekatika baina yangu na boyfriend wangu wa mwisho. Je nimekuwa rahisi sana? Lakini mbona nachukua muda mrefu kukubali kutoa tundi labda ungesema ni Easy Going? Msaada wenu ni muhimu kwangu. Samahani kwa maneno mengi. Ahsanteni.
 
lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,710
2,000
Mhhhhhhhhhh! Pole Sana Aiseeeeeeeee!!!!!! Ushauri wangu LEARN THE RULES OF THE GAME AND PLAY BY THE RULES!!!!!!!!!
 
Nyakwaratony

JF-Expert Member
Dec 21, 2011
574
195
Mhhhhhhhhhh! Pole Sana Aiseeeeeeeee!!!!!! Ushauri wangu LEARN THE RULES OF THE GAME AND PLAY BY THE RULES!!!!!!!!!

What are those rules my dear??? Hebu nifafanulie mwenzio yaani sijielewi elewi kabisa. Natamani kufurahia mapenzi kama wengine.......
 
Franky

JF-Expert Member
Apr 27, 2012
1,467
2,000
mabraza wanatusua na kuxepa....em jichunguze kwanza wewe mwenyewe kabla ujawakumbuka hao ma alumni
 
snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
17,292
2,000
sorry to say this!
ukiamua kukubali mtu kubali kwa moyo tu!ukiamua kukataa kataa mwanzo mwisho!
bahati mbya wanaume unaowavulia pichu unawavulia baada ya kuwaweka muda mreeeefu matokeo yake wakija kukupata tayari wana hasira za kuzungushswa hivo pengine muda ulioamua wewe kurudi yeye tayari ana mtu wake na since unakirudhisha mwenyewe wao wanamega wanasepa!
its like wanakutia kukukomoa sio kwamba wanahisia kweli!
WAY FORWARD
1.hebu jikubali kwanza na utambue mwanaume kwako ni wa aina gani!(vigezo vyako vya kudate mtu mpaka mpeane maraha huwa ni vipi)......................hii itakusaidia kuwa na maamuzi at hand huyu ananifaa fine hanifai tupa kule(for good)

2.jipe muda wa kujitambua wewe ni mwanamke wa aina gani................hii itakusaida kujjifahamu kike hasa na kuset ur principles if not boundaries

3.tambua na ukubali si wakati wote mwanaume akikwambia anakupenda anamaanisha wengine neno anakupenda wanamaanisha "kichupa kimejaa unaweza kunisaidia kipungue" .....................hii itakusaidia kutokulazimika kuvua pichu iwe ni mapema au baadae sababu tu mwanaume amekwambia anakupenda

4.fanya wengine watambue haiba yako,si kila mtu akuone anaweza akawa na wewe!wajichuje wenye huko huko kabla ya kuja kwako!......................hii itakusaidia kupunguza risk za kuanguka kwa mtu ambaye hudhani kuwa perfect kwako

5.JIKUBALI kuwa wewe ni wa pekee na upekee wako haubebwi na utambuzi wa mtu mwingine UPO NDANI YAKO!

UMEANGUKA,SIMAMA,FUTA VUMBI,TAZAMA MBELE,ISHI!
all the best!
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
24,392

Hapa umemsaidia kila atakayesoma ulichoandika, hata kama bado hayajamkuta.
 
jouneGwalu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,683
1,250

Nahisi kuna mtu unataka kumrithi, maana dalili zote naziona, ngoja nkachukue ushauri kwa Kongosho!
 
MadameX

JF-Expert Member
Dec 27, 2009
7,812
2,000
Sioni kama umekuwa rahisi au umebania sana, mapenzi kwa kweli hayana formula. Mimi naona sometimes its works if you don't take the person serious, kuna watu wanazidi hamu wakiwa ignored.
 
Nyakwaratony

JF-Expert Member
Dec 21, 2011
574
195
asante sana snowhite kwa kunitia moyo. Mwanzo umesema kuwa (Nawavulia chupii badaa ya kuwaweka muda mrefu) Je unataka kuniambia kuwa niwavulie kwa muda mfupi? Let say muda gani? Mimi nafikiri mtu anapotaka kuanzisha mahusiano ya kimapenzi anatakiwa kwanza awe anamfahamu mwenzie walau kwa kipindi fulani. Si kwamba wanaponitaka huwa nawapa makavu live ndipo nakuja kuwakubali, but huwa wanakuwa ni wapenzi bubu yaani huwa tunaongelea mapenzi kama wapenzi ila huwa nawabania tunda kwanza. Hapo huwa nakosea wapi?
 
Nyakwaratony

JF-Expert Member
Dec 21, 2011
574
195
Kwanini ungoje utongozwe na loosers uliowakataaa mwanzoni, ujue ulambe matapishi yako? You have a long way to go! Nina hamu kweli nikushauri ila sina pakuanzia!

Dada yangu sio kwamba nawakataa ila huwa nawaweka pending walau nipate muda wa kufahamiana kidogo. Huyo niliyesoma nae nilikuwa nafahamu kabisa kuwa alikuwa na girlfriend wake pale pale class. Na kwa bahati mbaya au nzuri kuna rafiki yangu alikuwa anafahamiana na huyo girlfriend wake. Wali break up hata kabla hatujamaliza course. Hiyo ndo ilinipelekea mimi kumkubali baada ya kujua kuwa kaachana na huyo gf wake. Je hapo nilifanya kosa?
 
Neylu

JF-Expert Member
May 28, 2012
2,943
2,000
Sioni kama umekuwa rahisi au umebania sana, mapenzi kwa kweli hayana formula. Mimi naona sometimes its works if you don't take the person serious, kuna watu wanazidi hamu wakiwa ignored.

Hapa kuna ukweli...!!
 
kibol

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
4,476
2,000
Inawezekana hao uliokutana nao haikupangwa wewe kuwa nao thats why mli-break up,kabla ya kuanzisha mahusiano chukua muda wako umuombe kwanza muumba wako akufungulie macho ya ndani umuone yule uliyepangiwa.jichunguze wewe kama wewe una mapungufu/kasoro gani,au una tabia gani ambayo unahisi hao wanaume uliokutana nao hawaipendi thats why wanakukimbia soon baada ya ku do?pengine tatizo linaweza kuwa more internally than externally...jichunguze vizuri dada yangu utapata jawabu,au labda wewe ni mzuri sana hivyo wanaume wengi wanatamani ku do na wewe thereafter wanakimbia nini?i think it is a million dollar question.
 
prianka

JF-Expert Member
Aug 29, 2012
684
195
baadhi ya wanaume ndivyo walivyo wakisha kupata na kukumega wanakua hawana haja na wewe tena cha msingi ukimpata mwanaume shariti la kwanza mwambie siwezi kusex hadi siku ya ndoa yetu kama anakupenda basi atazingatia na kama ni mbabaishaji atasepa na yakupasa ujiheshim mwenyewe
 
Joseph Isaack

JF-Expert Member
Aug 8, 2011
451
225
Pole xana dada yangu. Najua wewe ni binadamu na una mahitaji ya kimwili hilo halina ubishi. Ila fahamu kwamba kunatofauti kubwa sana juu ya mtizamo wa mapenzi kati ya mwanamke na mwanaume. Wanaume wengi kabla ya kumtongoza mwanamke huwa tunasex nae mentally na kwa kujenga dhana dhania juu ya muonekano wa nje wa mwanamke na kilichopo katikati ya mapaja yake. Hivyo kama utamvulia nguo mwanaume na akakujua vile ulivyo tayari thamani yako kwake itakuwa imeshuka. Ushauri wangu, usikubali kumvulia pichu mwanaume ambaye ungependa aje kuwa mumeo wa ndoa kabla ya wakt.
 
Menyous

Senior Member
Mar 17, 2009
136
0
Sioni kama umekuwa rahisi au umebania sana, mapenzi kwa kweli hayana formula. Mimi naona sometimes its works if you don't take the person serious, kuna watu wanazidi hamu wakiwa ignored.

Hii ni kweli kabisa. Na pia wanasema a man loves a woman who is not afraid to leave him and a woman loves a man who doesn't want to leave her. Kuongezea ningekushauri kwanza kuwa karibu na Mungu wako, focus on yourself na maendeleo yako, carry yourself with confidence na jipende na kujijali (hii inajumlisha usafi, afya yako, umaridadi na ulimbwende wa kiasi) usionyeshe wazi kuwa single au desperate kupata mtu, watu wasikufahamu maisha yako binafsi saana lakini haimaanishi uwe unajitenga hii itakuepusha na mikumbo. Usiwe mwepesi kumuamini, pale mtu anapoonyesha interest don't take it serious mchunguze tabia zake, mitazamo na pespective yake juu ya wanawake na expectations zake juu ya aina ya mwanamke anayetaka kuwa naye maishani, ujipimie kama viatu ni size yako au sivyo mapema.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
2,000
Kuwa mwanaume ni kazi lakini kuwa mwanamke ni shughuli pevu, fuata ushauri wa snowhite ametirirka vizuri shemeji yangu huyu wa kunyumba..............
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom