Sijawahi kuona ‘ Poor Reporting Style ‘ na iliyopitwa na wakati kutoka katika Media za Tanzania kama hii ya leo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,920
Nimeangalia Vichwa vya Habari vya leo Jumapili tarehe 23, Septemba 2018 na mpaka sasa hivi nimebaki na ‘ mshangao ‘ mkubwa sana ambao unasindikizwa na ‘ masikitiko ‘ makubwa hasa kwakuwa nashuhudia kwa mara nyingine tena jinsi Vyombo vya Habari vya Tanzania vinavyofanya ‘ reporting ‘ zao za matukio muhimu katika hali ya ‘ Ushamba / Umbwigira ‘ kabisa halafu wenyewe wanadhani wanapatia na ni Weledi.

Hivi inawezekana vipi ‘ Headlines ‘ za karibia 90% ya Magazeti ya Kila siku yawe ni ya aina moja tu? Hivi inaingia ‘ akilini ‘ kweli katika dunia ya sasa ambayo ina Watu wengi wenye uelewa mkubwa wa mambo huku wakiwa tayari wana taarifa za kutosha halafu na Wewe tena kama Gazeti Kesho yake unakuja na Kichwa cha Habari ambacho hakileti sana ‘ Tija ‘ sana sana kinaonyesha tu ‘ udhaifu ‘ mkubwa katika Tasnia nzima ya Habari nchini Tanzania.

Nyie Waandishi wa Habari na Magazeti yenu ni nani amewaambieni kuwa Watanzania tunataka kuona ‘ Headline ‘ kama hii ambayo leo ndiyo ‘ imetawala ‘ katika Magazeti yenu isemayo… “ Mhandisi Alphonce Cherehani akutwa hai “…

Sisemi kwamba taarifa hiyo ni mbaya au haifai ila hoja yangu hapa ya msingi ni kwamba katika ‘ Modern Journalism / Modern Media Reporting ‘ hii ‘ Headline ‘ haikutakiwa isipokuwa hili tukio lingeelezewa tu moja kwa moja katika ‘ mtiririko ‘ wa Habari nzima lakini siyo kufanywa kama ndiyo ‘ Story Angle ‘ kama ambavyo Media nyingi zimefanya.

Katika ‘ Ancient Journalism /Ancient Reporting ‘ Kichwa cha Habari hiki kingefaa kama siyo kingependeza sana ila kama ‘ Wanataaluma ‘ tusisahau ya kwamba kuna ‘ Maendeleo ‘ mapya hasa katika ‘ Tasnia ‘ nzima ya Uandishi wa Habari duniani ambapo katika ‘ Modern Reporting ‘ mkazo unawekwa sana katika Kitu Kiitwacho ‘ Interpretative Journalism / Interpretative Reporting ‘ ambapo Mwandishi hapashwi tena kutueleza kilichotokea ambacho kinajulikana na badala yake sasa anatakiwa ‘ Kutafsiri ‘ ama katika mlengo wa Hasi au Chanya juu ya tukio zima ili kuweza kuwapa Wasomaji / Walaji wako uwanda mpana wa Kimaarifa na Elimu zaidi.

Kwa mfano baada sasa ya tukio zima la ‘ Mkasa ‘ uliotokea wa MV Nyerere kama Tanzania tungekuwa na ‘ Professional Journalists ‘ kabisa kama ambao wanapatikana sana katika Magazeti tu ya MWANANCHI na THE CITIZEN basi leo hii Vichwa vya Habari vya Magazeti ya Tanzania vingekuwa na ‘ Headlines ‘ ambazo sasa hazituachi tena pale tulipo na badala yake zinatupa ‘ mtazamo ‘ mpana ambao pia utasaidia kuweza Kuokoa au Kuzuia hali hii isitokee tena huko mbele lakini siyo Magazeti yote kuja na Kichwa cha Habari ‘ mfanano ‘ kisemacho “ Mhandisi wa MV Nyerere Alphonce Charahani akutwa hai na Waokoaji “ kidogo inaonyesha bado tuna tatizo la Kudumu katika ‘ Media ‘ zetu.

Navipongeza sana Vyombo vya Habari vya Tanzania kwa juhudi zake za Kuhabarisha, Kuelimisha na Kuburudisha ila kama GENTAMYCINE ningeambiwa nitoe alama ( Marks ) kwa ‘ Utendaji ‘ wa ‘ Media ‘ zetu wala nisingechelewa kuwapa alama 30% na kama ningewapendelea sana basi ningewapa alama 35% ila bado wana safari ndefu mno ya kuweza Kuzifikia ‘ Media ‘ kwa mfano za Kenya, Uganda, South Afrika, Algeria, Zimbabwe na Ghana. Badilikeni tafadhali kwani bado hamjachelewa na acheni ‘ mazoea ‘ katika ‘ reportings ‘ zenu.

Najua hapa JamiiForums kuna ‘ Manguli ‘ kabisa wa Habari, Utangazaji na Mawasiliano hivyo nami pia nitafurahi kama wakija hapa na Wao wakitoa mchango na uzoefu Wao juu ya hili nililoligusia na nitapenda pia ‘ wanikosoe ‘ kwa Hoja kabisa pale ambapo wameona sipo sahihi yote kwa yote ikiwa ni katika hali tu ya kuwekana sawa na kuzidi Kuelemishina. Hata Mimi GENTAMYCINE nitafurahi kama ‘ nikijuzwa ‘ zaidi ya pale ambapo naelewa kwakuwa napenda mno kuwa na ‘ Maarifa ‘ mapya kila Siku / Uchao.

Nawasilisha.
 
Sasa umeongea tuu bila ww kutoa heading ambayo unaona ingefaa umezunguka zunguka tu toa maoni yako au solution wangeandikaje mtu amekutwa hai kaokolewa ulitaka kichwa cha habari iweje hata BBC,CNN wakirepotigi matukio ya uokoaji akikutwa mtu hai pasipo kutegemea hua ni breaking news
 
Hawana uhakika waandike nini maana hawana uhakika kama habari hizo zitamfurahisha au kumkasirisha mtu. Hivyo wanaandika ili mradi tu, ila kiuhalisia ni kama vile wanasubiri msemaji wa serikali awapatie headlines na habari za kuandika ili waandike.
 
Wachovu wa kutafuta habari. Umesahau kipindi fulani hivi wakati wa Mzee Mwinyi (Mzee ruksa), watu walifanya mambo ya ajabu, kuna gazeti liliripoti "naye Mwinyi yumo", tena kwa habari nzito, kwenda kusoma habari yenyewe kumbe mwinyi mwingine kabisa!
 
Mkuu utayaoga matusi sasa hivi,mkuu poppma huwa hakosei
GENTAMYCINE aka Popoma ni noma. Ila huwa mapenda story zake, nyingi zinakua na balanced diet.
Ila nyingine baadhi akikosea huwa anakosea kweli, unakuwa ni full machakani.
😆😆Akija kunitukana tutagaqana mitusi, nusu ya mitusi utachukua wewe na nusu nyingine nitamrudishia yeye😆😆😆
 
Nimeangalia Vichwa vya Habari vya leo Jumapili tarehe 23, Septemba 2018 na mpaka sasa hivi nimebaki na ‘ mshangao ‘ mkubwa sana ambao unasindikizwa na ‘ masikitiko ‘ makubwa hasa kwakuwa nashuhudia kwa mara nyingine tena jinsi Vyombo vya Habari vya Tanzania vinavyofanya ‘ reporting ‘ zao za matukio muhimu katika hali ya ‘ Ushamba / Umbwigira ‘ kabisa halafu wenyewe wanadhani wanapatia na ni Weledi.

Hivi inawezekana vipi ‘ Headlines ‘ za karibia 90% ya Magazeti ya Kila siku yawe ni ya aina moja tu? Hivi inaingia ‘ akilini ‘ kweli katika dunia ya sasa ambayo ina Watu wengi wenye uelewa mkubwa wa mambo huku wakiwa tayari wana taarifa za kutosha halafu na Wewe tena kama Gazeti Kesho yake unakuja na Kichwa cha Habari ambacho hakileti sana ‘ Tija ‘ sana sana kinaonyesha tu ‘ udhaifu ‘ mkubwa katika Tasnia nzima ya Habari nchini Tanzania.

Nyie Waandishi wa Habari na Magazeti yenu ni nani amewaambieni kuwa Watanzania tunataka kuona ‘ Headline ‘ kama hii ambayo leo ndiyo ‘ imetawala ‘ katika Magazeti yenu isemayo… “ Mhandisi Alphonce Cherehani akutwa hai “…

Sisemi kwamba taarifa hiyo ni mbaya au haifai ila hoja yangu hapa ya msingi ni kwamba katika ‘ Modern Journalism / Modern Media Reporting ‘ hii ‘ Headline ‘ haikutakiwa isipokuwa hili tukio lingeelezewa tu moja kwa moja katika ‘ mtiririko ‘ wa Habari nzima lakini siyo kufanywa kama ndiyo ‘ Story Angle ‘ kama ambavyo Media nyingi zimefanya.

Katika ‘ Ancient Journalism /Ancient Reporting ‘ Kichwa cha Habari hiki kingefaa kama siyo kingependeza sana ila kama ‘ Wanataaluma ‘ tusisahau ya kwamba kuna ‘ Maendeleo ‘ mapya hasa katika ‘ Tasnia ‘ nzima ya Uandishi wa Habari duniani ambapo katika ‘ Modern Reporting ‘ mkazo unawekwa sana katika Kitu Kiitwacho ‘ Interpretative Journalism / Interpretative Reporting ‘ ambapo Mwandishi hapashwi tena kutueleza kilichotokea ambacho kinajulikana na badala yake sasa anatakiwa ‘ Kutafsiri ‘ ama katika mlengo wa Hasi au Chanya juu ya tukio zima ili kuweza kuwapa Wasomaji / Walaji wako uwanda mpana wa Kimaarifa na Elimu zaidi.

Kwa mfano baada sasa ya tukio zima la ‘ Mkasa ‘ uliotokea wa MV Nyerere kama Tanzania tungekuwa na ‘ Professional Journalists ‘ kabisa kama ambao wanapatikana sana katika Magazeti tu ya MWANANCHI na THE CITIZEN basi leo hii Vichwa vya Habari vya Magazeti ya Tanzania vingekuwa na ‘ Headlines ‘ ambazo sasa hazituachi tena pale tulipo na badala yake zinatupa ‘ mtazamo ‘ mpana ambao pia utasaidia kuweza Kuokoa au Kuzuia hali hii isitokee tena huko mbele lakini siyo Magazeti yote kuja na Kichwa cha Habari ‘ mfanano ‘ kisemacho “ Mhandisi wa MV Nyerere Alphonce Charahani akutwa hai na Waokoaji “ kidogo inaonyesha bado tuna tatizo la Kudumu katika ‘ Media ‘ zetu.

Navipongeza sana Vyombo vya Habari vya Tanzania kwa juhudi zake za Kuhabarisha, Kuelimisha na Kuburudisha ila kama GENTAMYCINE ningeambiwa nitoe alama ( Marks ) kwa ‘ Utendaji ‘ wa ‘ Media ‘ zetu wala nisingechelewa kuwapa alama 30% na kama ningewapendelea sana basi ningewapa alama 35% ila bado wana safari ndefu mno ya kuweza Kuzifikia ‘ Media ‘ kwa mfano za Kenya, Uganda, South Afrika, Algeria, Zimbabwe na Ghana. Badilikeni tafadhali kwani bado hamjachelewa na acheni ‘ mazoea ‘ katika ‘ reportings ‘ zenu.

Najua hapa JamiiForums kuna ‘ Manguli ‘ kabisa wa Habari, Utangazaji na Mawasiliano hivyo nami pia nitafurahi kama wakija hapa na Wao wakitoa mchango na uzoefu Wao juu ya hili nililoligusia na nitapenda pia ‘ wanikosoe ‘ kwa Hoja kabisa pale ambapo wameona sipo sahihi yote kwa yote ikiwa ni katika hali tu ya kuwekana sawa na kuzidi Kuelemishina. Hata Mimi GENTAMYCINE nitafurahi kama ‘ nikijuzwa ‘ zaidi ya pale ambapo naelewa kwakuwa napenda mno kuwa na ‘ Maarifa ‘ mapya kila Siku / Uchao.

Nawasilisha.
@Gentamycine ulitaka kichwa cha habari cha aina gani?
Mimi kwa uelewa wangu mdogo kwenye ile habari ya mhandisi cherehani, ni habari muendelezo:
Mosi, ni habari mvunjiko, ambayo vyanzo vya habari ni watu waliomuokoa, mazingira waliomkuta, jinsi walivyomkuta hadi hospitali waliompeleka, matabibu walivyompokea, huduma waliompa na matarajio ya matabibu kwa mgonjwa.

Pili, kuhoji ndugu marafiki na watu anaofanya nao kazi mhandisi kujua ni mtu wa kariba gani.
Hii habari kwa awali ingeitajika ata kidogo basi mlaji wa taarifa apate taarifa hizi.

Mhandisi akitoka hospitali atakuja kutueleza aliweza kuishi vipi ndani ya boti, chini ya maji kwa siku tatu, atakuja kutueleza alikuwa kwenye hali ya namna gani kule.

Lakini baadae lazima tupate mwandishi ambaye atakuja kutupa historia ya kivuko chenyewe, kilinunuliwa wapi, kimetengenezwa kwa teknolojia gani, kina uwezo gani, Na tokea kimeletwa kimekumbana na changamoto gani kabla ya hii ajali???

Mwandishi lazima aweke mizani sawa kwa kuhoji wataalam mbalimbali kujua tatizo lile kitaalam linaitwaje? na makosa ni ya nani? Na nini kifanyike ajali kama hizi zisitokee maana hii ni ajali kama sijakosea ni ya tatu, kuna ile ya kule Zanzibar, mv bukoba na hii.

KWA HIYO SINA SHAKA NA KICHWA CHA HABARI "TATIZO HABARI YENYEWE IPO KI UWELEDI? "
 
@Gentamycine ulitaka kichwa cha habari cha aina gani?
Mimi kwa uelewa wangu mdogo kwenye ile habari ya mhandisi cherehani, ni habari muendelezo:
Mosi, ni habari mvunjiko, ambayo vyanzo vya habari ni watu waliomuokoa, mazingira waliomkuta, jinsi walivyomkuta hadi hospitali waliompeleka, matabibu walivyompokea, huduma waliompa na matarajio ya matabibu kwa mgonjwa.

Pili, kuhoji ndugu marafiki na watu anafanya nao kazi, mhandisi kujua ni mtu wa kariba gani.
Hii habari kwa awali ingeitajika ata kidogo basi mlaji wa taarifa apate taarifa hizi.

Mhandisi akitoka hospitali atakuja kutueleza aliweza kuishi vipi ndani ya boti, chini ya maji kwa siku tatu, atakuja kutueleza alikuwa kwenye hali ya namna gani kule.

Lakini baadae lazima tupate mwandishi ambaye atakuja kutupa historia ya kivuko chenyewe, kilinunuliwa wapi, kimetengenezwa kwa teknolojia gani, kina uwezo gani, Nampa tokea kimeletwa kimekumbana na changamoto gani kabla ya hii ajali???

Mwandishi lazima aweke mizani sawa kwa kuhoji wataalam mbalimbali kujua tatizo lile kitaalam linaitwaje? na makosa ni ya nani? Na nini kifanyike ajali kama hizi zisitokee maana hii ni ajali kama sijakosea ni ya tatu, kuna ile ya kule Zanzibar, mv bukoba baby hii.

KWA HIYO SINA SHAKA NA KICHWA CHA HABARI "TATIZO HABARI YENYEWE IPO KI UWELEDI? "

Akhsante kwa Elimu Mkuu kwani hata Mimi bado najifunza pia na hapa umenizidishia ' madini ' hasa Kimaarifa.
 
Back
Top Bottom