Sijawahi kula nyama tamu kama konokono

sizonjemadawa

JF-Expert Member
Feb 11, 2017
1,053
1,304
Habarini wakuu

Maisha ni safari,

Katika mihangaiko ya maisha nchi tofauti nimekula wanyama na wadudu ambao kwa jamii za Tanzania wengi hawali kama vile
Konokono
Chura wakubwa (ryumi)
Nyoka aina ya chatu
Chui
Kobe
Ngedere (tumbili)
Funza wakubwa (wanakaa kwenye miti) n.k
Hao ni baadhi tu na nilikula sikulazimishwa ila sikuwa na jinsi, katika nyama zote niwe mkweli konokono nimetokea kumpenda sana, ni nyama tamu haina hata mfupa ukipata yule mwenye mayai duh hutoacha kula nawaambia,

Ombi: Kama hapa DSM kuna sehemu wanauza konokono mnidirect tafadhali.. nataka ile iliyokaangwa

Kama na wewe ushawahi kula vyakula ambavyo watanzania wengi wanaona uchafu vitaje, tufahamiane


Tembea ujionee Dunia ina mengi, vingine havisimuliki.
 
Habarini wakuu

Maisha ni safari,

katika mihangaiko ya maisha nchi tofauti nimekula wanyama na wadudu ambao kwa jamii za tanzania wengi hawali kama vile
Konokono
Chura wakubwa (ryumi)
Nyoka aina ya chatu
Chui
Kobe
Ngedere (tumbili)
Funza wakubwa (wanakaa kwenye miti) n.k
Hao ni baadhi tu, na nilikula sikulazimishwa ila sikuwa na jinsi, katika nyama zote niwe mkweli konokono nimetokea kumpenda sana, ni nyama tamu haina hata mfupa ukipata yule mwenye mayai duh hutoacha kula nawaambia,

ombi: kama hapa dsm kuna sehem wanauza konokono mnidirect tafadhali.. nataka ile iliyokaangwa

kama na ww ushawai kula vyakula ambavyo watanzania wengi wanaona uchafu vitaje, tufahamiane


Tembea ujionee Dunia inamengi vingine havisimuliki
Uko sahihi mkuu, mimi pia niliwahi kula aisee. Ile nyama ya konokono ni ya kipekee tamu sana sema sijajua kwa hapa Dar wapi wanauza
 
Kuna mdada mmoja wa Kiitaliano aliwahi niambia kuwa wao kule konokono ni chakula maarufu sana. Ila wanatushangaa Watz kwa kula kumbikumbi. Btw, ngoja wakushangae na kukucheka.

Siku wakisikia kuwa kula konokono kunatibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume au siku wakina mama wakisikia ni dawa ya kumdhibiti mume asitoke nje ya ndoa na dozi yake ni lazima uwatafune mkubwa mmoja kwa siku saba utaona wanavyofuatilia na kuulizia wanapatikana wapi.
 
Nilipokuwa Abuja almanusura nile konokono nikidhania filigisi! Tayari nilishatia hadi pilipili na pembeni kuna vanilla Coke.... Kilichoniokoa ni kugundua kwamba kila chombo kilichokuwa na Chakula eneo lile kilikuwa na lebo ya aina ya Chakula kilichomo...niliposoma kilichoandikwa pale nilipotoa filigisi zangu....dah... Snails!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom