Sijawahi kuambiwa nakupenda na mwenza wangu

fkawogo

Senior Member
May 30, 2013
131
37
Nipo mbele yenu waungwana katika jukwaa letu. Nina jambo nataka kuomba ushauri kwenu. Nimeoa sasa huu mwaka wapili niko kwenye ndoa.
elimu yangu ni ya shahada pamoja na mke wangu pia ana shahada.

Kilichonileta kwenu nikwamba tangu namtongoza mke wangu mpaka namuoa sijawahi kusikia neno nakupenda akinitamkia lakini mimi nimemwambia neno hilo na majina mengi mazuri Mara elfu kidogo.

Kwa kweli naumia sana mpaka najilaumu kwann nilimuoa lakini pia najiuliza hivi huyu mwanamke ananipenda kweli au ni uongo? Ila mambo ya nyumbani yote anafanya siwezi mlaumu.Tunashirikiana pamoja shida yangu ni neno nakupenda kwanini huwa hawezi kutamka?

Naombeni ushauri wenu au nipige chini?
 
Hii inatokea mkuu.... baadhi ya watu upenda kimoyo-moyo ila hawezi kutamka, je anapenda kukufatilia endapo utachelewa rudi nyumbani au vinginevyo...... kama mienendo yake mizuri haina haja kuachana nae

Unaweza pata mwingine akakuambia nakupenda ila akawa anahana tabia nzuri hata kidogo
 
nipo mbele yenu waungwana katika jukwaa letu. Nina jambo nataka kuomba ushauri kwenu.
nimeoa sasa huu mwaka wapili Niko kwenye ndoa.
elimu yangu ni ya shahada pamoja na mke wangu pia ana shahada.
kilicho nileta kwenu nikwamba tangu namtongoza mke wangu mpk namuoa sijawahi kusikia Neno NAKUPENDA akinitamkia lkn Mimi nimemwambia Neno hilo na majina mengi mazuri Mara elfu kidogo.
kwakweli naumia sana mpk najilaumu kwann nilimuoa.
lkn pia najiuliza hivi huyu mwanamke ananipenda kweli au ni uongo?
ila mambo ya nyumbani yote anafanya siwezi mlaumu. tunashirikiana pamoja shida yangu ni Neno NAKUPENDA kwanini huwa hawezi kutamka? naombeni ushauri wenu au Nipige chini?
Kibblia, mwanamume anapaswa kumpenda mkeo. HHuo ni wajibu wako. Mke anapaswa kukutii na kukuheshimu. Sioni shida yoyote hapo Mimi. Kumbuka, action speaks louder than words, sio lazima maneno. Wanawake, ndio wanapaswa kuambia maneno mazuri, inapaswa kuishi nao kwa akili. Pia unaweza ukaongea nae tu, mweleze ukweli. Kifupi ni kwamba kama anakutii hili ndilo muhimu. Hakuna jambo nilisozungumzika.
 
Kama hasemi au hawez kukiri kwa kinywa kama anakupenda hapo kuna uwezekano wa haya kuweoo kati yenu
1.either kiukwel hakupendi
2.pili anaweza akawa ni type ya mwanamke ambae si muwaz wa hisia zake
3.alikubali kuolewa sababu ya maslahi
4.wewe huwek mazingira ya yeye kuwa na furaha moyoni mpaka akutamkie maneno hayo
Kinyume na hapo kuna vitu na wewe hujatuweka wazi
 
nipo mbele yenu waungwana katika jukwaa letu. Nina jambo nataka kuomba ushauri kwenu.
nimeoa sasa huu mwaka wapili Niko kwenye ndoa.
elimu yangu ni ya shahada pamoja na mke wangu pia ana shahada.
kilicho nileta kwenu nikwamba tangu namtongoza mke wangu mpk namuoa sijawahi kusikia Neno NAKUPENDA akinitamkia lkn Mimi nimemwambia Neno hilo na majina mengi mazuri Mara elfu kidogo.
kwakweli naumia sana mpk najilaumu kwann nilimuoa.
lkn pia najiuliza hivi huyu mwanamke ananipenda kweli au ni uongo?
ila mambo ya nyumbani yote anafanya siwezi mlaumu. tunashirikiana pamoja shida yangu ni Neno NAKUPENDA kwanini huwa hawezi kutamka? naombeni ushauri wenu au Nipige chini?
Neno hilo ni ziiito sana, haliotoki kinywani kirahis lazma kuna mambo sharti uyatimize kwake ndo alitoe ilo neno.
Ukiona halitoi kwako jua analitoa kwingneko uko... anzisha msako
 
Jaribu kuongea nae... muulize nn tatizo. chunguza matendo yake... hope utapata jib
 
Mfundishe tu taratibu taratibu na atakuelewa. Ndivyo inavyokuwaga hivyo kwa baadhi ya watu. Mila, Desturi, Tamaduni, Malezi, Makuzi na Mazingira aliyokulia vinaweza vikawa vimechangia.
Ndoa ni chuo cha maisha.
 
Back
Top Bottom