Sijasoma Namba kwa sababu hizi

Sijasoma Namba kwa sababu hizi

Mi nawashangaa wanaolia ukata wa hela wanaolia maisha magumu, wanaolia lia kuhusu kukosa ajira na mambo mengine mi ntawakosoa kwa haya,

1. UKATA WA HELA
jaman pigen kazi ,unataka hela ije wakati hufanyi kazi itatoka wapi,? Vijana ardhi Yetu INA rutuba , pia kuna fursa nyingi dunian siyo mpaka rais au serikali ikushike mkono na kukuonesha fursa zilipo,

2. AJIRA
Mtu kahitimu Chuo kikuu au vyuo vya kawaida yupo kwa baba yake na mama yake anasubiri ajira, wakati hao mama zake na baba hawakuwahi kuajiriwa popote na maisha wameyaweza mpaka kumsomesha huyo kijana , ila yeye kakaa tu anasubiri ajira uo si ustaarabu lazima utasoma Namba kwa namna hii tena za kirumi,

Sikuwahi zunguka zunguka na bahasha kisa ajira , kwasababu nilikuwa na maono kabla sijamaliza chuo enzi hizo nshaset mipango, pia hata walipo tangaza kazi nikiweka mguu naitwa kulingana na passmark zangu, SASA KWANINI NISOME NAMBA?

3. ELIMU
Mama ndalichako hebu kaza kaza kaza hatutaki watu wanaopata elimu dhaifu na kuanza kutamba mtaani wakati hawajui kuitumia , degree dhaifuuu yaan alafu anasema hawezi Fanya kazi za chini kisa degree ya STEMUCO? TEKU? JOKUKO? KIUKO?

Hapa lazima tujisahihishe, tuliteleza na sasa mama huyu anajaribu kurudisha heshima ya elimu lakin makanjanja wanalalamika,
Mbona sisi tulipita kwenye vigezo hivyo vigumu vigumu,? Na tukazisoma degree kwa ufasaha na entry qualification bila division one huendi Chuo kikuu direct, sasa hawa wamerudia mitihan mpaka baas wameunga unga mpaka basi, alafu unataka mteremko?? Soma za kigiriki sasa namba

4.BIASHARA
sijawahi kukwepa kodi na sikutegemea hela za magumashi nilisimama imara hata kabla ya magufuli kuwa rais hivyo anachofanya ni Muhim, ngoja watu wajue kuwa lazima utaratibu ufuatwe, Sasa nina kibali, nalipa kodi ninafuata taratibu zote, ntasomaje Namba?

5. UHURU WA HABARI NA KUJIELEZA
huwa nafuata mafundisho na taratibu kureport na kuhabarisha masual mbalimbali, istoshe sina utapiamlo unaosababisha kuota ndoto kama za lema, sasa hapo ntasomaje Namba?

6. NINATEGEMEA NGUVU ZANGU KUJIKWAMUA sitegemei serikali au yeyote hivyo dhana hii imenifanya nijione sawa kila muda hata aje rais gani, aweke mazingira yapi sitasoma Namba, maana ninafuata utaratibu,

Vijana faulu vizuri, jitume, kuwa mbunifu,fuata sheria ,unone kama utasoma Namba,
Hakuna umuhimu wakuwa na wafanyakazi wa serikali na hamuna umuhimu wakuwa na wizara ya ajira na kazi kwasababu hatuhitaji vitu hivyo kwa mujibu wa andiko lako
 
Vijana wamekua wakulalamika tu, mie swala la kusoma namba nawashangaa tu maana enzi hizo wanasema za neema sikuwah kumiliki milioni, kaja Magu nimepata kazi nzuriiii, nalipa kodi (payee) nalipa kodi ya pango na nnaendesha gari sasa unasemaje Magu mbaya nikuelewe vijana pigen kazi magumash muda wake umeisha
 
Biashara zangu sasa hivi zinakuwa kwa kasi ya ajabu kutoka na kipindi cha nyumba nilikuwa ninashinda na wakwepa kodi...Asante Magufuli.
 
Back
Top Bottom