Sijapenda alichofanyiwa Kijana wangu na Jimama

je parle

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
1,881
3,619
Siku jamaa kajichanganya kaenda kwa jimama lake kamkuta mshikaji mwengine yupo sebuleni kakaa ila jamaa hakupanic. Jimama likamtengea chai sehemu yake na yule mchizi mwengine akatengewa chai sehemu nyingine safi.

Baada ya chai jimama likamtuma kijana akanunue mboga sokoni, jamaa kaenda sokon akarudi akatumwa tena hospital akachukue kitu gani sijui
Jamaa karudi hospital anapiga hodi ndani kimya, ikabidi aingie ndani anakuta viatu vya mchizi nje ya mlango kana kwamba wapo wote chumbani wanafanya yao.

Jamaa akaona hapo nimeachwa kiudhalilishaji sana na yote haya ni kwasababu Sina pesa. Basi jamaa kajiondokea kiunyonge mno.

Hii stories jamaa hakuniambia kwakuwa anaona noma, alienisimulia ni mtu ambae alitumiwa sms na yule jimama, alishawai niambia kuwa kijana wako anasema ugonjwa wake ni wanawake wakubwa wakubwa yeye ndio magoma yake


Note: Hili naona liwe funzo kwa vijana wanaopenda kulelewa na mi shangazi wakati hao mashangazi na wao Kuna watu wanawachuna.

Ule Uzi haukutakiwa kuwa kataa ndoa Bali uwe kataaa uzinifu maana unatia sonona na mawazo.
 
Kwanza napenda kudeclare interest kuwa mimi sio kijana WA hovyo kama vijana wengine wapenda mademu lakini wanakataa ndoa......

Ipo hivi Nina kijana wangu mtaani ambae Huwa anauza kwenye kibanda changu Cha chipsi ,huyu kiumri ananizidi kidogo lakini bado ni kijana kwangu kwakuwa ni kama chawa kwangu na yeye ananiita brother

Ipo hivi karibia na Banda langu la kiepe Kuna mshangazi unauza kuku WA kukaanga

Sasa sijui mahusiano Yao yalianza vipi mpaka wakafikia kuwa kijana anaenda kwa JIMAMA anakaa hata siku tatu kajifungia tu ndani wanakula maisha

Lakini kijana Kila siku kulalamika kuwa biashara ngumu na majukumu ya nyumbani kwahiyo biashara mara inakufa ,mara inarudi tena basi tafran

Siku viazi vikipanda sana Huwa hafungui na Mimi Huwa nikafika kipindi simwambiii alete hata shilingi kumi yake

Huwa nakula tu sahani Moja naaga naondoka ,najisemea ngoja jamaa ajipange kwanza mana anakaa tu kwa mtu ila nikaribu na familia yake mana yake

Sasa Kuna wiki kama Moja alikuwa hafungui kabisa na nikimuuliza anasema vitu bei juu na hauzi sana ,kwahiyo kama karogwa hivi

Lakin nilikuwa nishaanza kusmell something kuwa huyu bwana ni mtu WA mademu na Kuna demu alikuwa anamkubali nikamwambia kama unamtaka kweli sema nitakusimamia uweke chombo ndani uache kuruka ruka ,

Ila alifuatilia yule mwanamke akamtolea mbavuni ,so ishu ikaishia hapo.

Akajiamishia kwa yule JIMAMA wanakula Raha wenyewe,

Sasa ishu ilikuja ni kuwa yule JIMAMA akipata bwana mwengine nadhani alikuwa anahonga KULIKO huyu kijana wangu, ndio mambo yakaharibia hapo

JIMAMA likaanza kumpa masharti kijana kwamba Kila siku uwe unanipa 12,000
Yan asubuhi 2000
Mchana 5000
Usiki 5000..

Jamaa akaona mambo magumu ila akawa anapambana japo sio yote hivyo hivyo maisha yanasonga.

Mara siku nyingine kijana akipigiwa simu na JIMAMA hapatikani dizain kama anakimbia 12,000 kubwa kwake anaona kama hasara wakati yeye mwenyewe kwa siku anatumia kubwa ni 2000 alafu anaambiwa atoe elfu 12

Siku akapigiwa simu hapatikani JIMAMA likaanza kutuma sms kwa namba ya rafiki yake

Meseji mbali mbali naaanza na hii
Mwanaume gani unashindwa kuhudumia mwanamke ,

Tafuta kazi sio Kila siku kucheza pool table tu

Mwanaume unataka kulishwa na mwanamke

Basi zimeandikwa sms za kutosha.


Siku jamaa kajichanganya kaenda kwa JIMAMA lake kamkuta mshikaji mwengine yupo sebuleni kakaa ila jamaa hakupanic

JIMAMA likamtengea chai sehemu yake na yule mchizi mwengine akatengewa chai sehemu nyingine safi.

Baada ya chai JIMAMA likamtuma kijana akanunue mboga sokon ,jamaa kaenda sokon akarudi akatumwa tena hospital akachukue kitu gani sijui
Jamaa karudi hospital anapiga hodi ndani kimya ,ikabidi aingie ndani anakuta viatu vya mchizi nje ya mlango kana kwamba wapo wote chumbani wanafanya Yao

Jamaa akaona hapo nimeachwa kiudhalilishaji sana na yote haya ni kwasababu Sina pesa.
Basi jamaa kajiondokea kiunyonge mno

Hii stories jamaa hakuniambia kwakuwa anaona noma ,alienisimulia ni mtu ambae alitumiwa sms na yule JIMAMA

Mana alishawai niambia kuwa kijana wako anasema ugonjwa wake ni wanawake wakubwa wakubwa yeye ndio magoma yake


Note.

Hili naona liwe funzo kwa vijana wanaopenda kulelewa na mi shangazi wakati hao mashangazi na wao Kuna watu wanawachuna

Ule Uzi haukutakiwa kuwa kataa ndoa Bali uwe kataaa uzinifu maana unatia sonono na mawazo
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Hivi kwann vijana wasimuige asake wa tandale daaa

Na log out I'm mr 💰🤣
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom