Mara nyingi sababu huwa ni sisi wenyewe wanaume. Vuta picha kwa hisia za ndani kbs - unakumbuka wakati mkeo ana mimba ya mtoto wenu wa 1 ? unaonaje ukilinganisha na hivi sasa ? ule upendo, ukaribu, mapenzi, mahaba, ukarimu, heshima na kumjali vinafanana?( bila shaka jibu la moja kwa moja lenye kweli ndani yake ni HAPANA). Kama ndivyo basi ujue kuna pahala hapako sawa. Nafahamu wanaume tulio wengi huwa tunawapenda na kuwajali sana wake zetu hasa wanapokuwa na mimba ya mtoto/ watoto wa kwanza na sababu yake inajulikana i wazi kbs ni ile hamu ya kuwa na mtoto ambaye una uhakika ni wako i.e wewe unakuwa baba na yy mama X hivyo tension huwa kubwa kiasi cha kumpa mke matunzo adimu, maalumu bila kujali kwamba akilini unatambua ama kutotambua.
Shida inakuja kwa mimba ya pili hali ile hupungua na ya tatu ndio kabisaaaa na kuendelea. Inakuwa ni jambo la kawaida sasa mkeo kushika mimba akazaa- kumbuka nae pia mindset yake hujitune hivo hivo kadiri unavompa ile attention kwake. Matokeo ya hii ni hayo unayoyaeleza hapo. Kama tungelizingatia mambo haya bila kujali idadi ya watoto nina hakika tusingekutana na mapungufu haya isipokuwa kwa nadra sana