Tatizo lenu mnataka wanawake kama wa US ila ninyi hamtaki kuwa kama wanaume wa US so hata hao hamtawaweza, hivi unafahamu kwamba kule kila kitu ni 50/50 siyo kutafuta hela tu hata kazi za nyumbani kupika, kuosha vyombo, kufua, kusafisha nyumbani, kulea watoto nk nazo ni 50/50, kule hakuna cha eti sijui haya ni majukumu ya mwanaume au haya ni ya mwanamke
Wote mnatoka kwenda kazini kutafuta pesa na mnasaidiana kulipia bills na pia kazi za nyumbani mkirudi mnasaidiana kwa pamoja, na kulea watoto ikiwemo kuwalisha na kuwaogesha mnafanya wote au mnaajiri nannies na hutasikia wanaume wao wakilalamika, sasa huku wanaume wanataka wanawake wawasaidie kutafuta pesa na kulipa bills ila wao hawataki kuwasaidia kazi za nyumbani
Na wakiajiri housegirls utasikia wanaume wanaanza kulalamika mara "oo wake zetu wamejisahau sana kila kitu wanawaachia housegirls" matokeo yake wanaanza kutembea na hao housegirls, sasa mke anayetoka kwenda kufanya kazi au biashara na kukusaidia majukumu yako atawezaje kujigawa kufanya na majukumu yake ya nyumbani, yani mnarudi wote toka kazini mmechoka ila mkifika mke tena ahangaike na kazi za nyumbani ila mume anaweka miguu juu eti anapumzika