Habibu B. Anga
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 6,557
- 25,716
SIIONI "VITA" DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA.. NASIKIA KELELE TU.!
Binafsi sio mchangiaji sana wa mijadala ya kisiasa, kwa sababu kuna muda huwa nahisi ukifuatilia mienendo ya wanasiasa katika nchi zetu hizi masikini unaweza kujikuta unakata tamaa ya maisha.
Ni Bahati mbaya sana, tunapata viongozi wenye vyeo pasipo kuwa na sifa za uongozi na wakati huo huo tuna watu wenye sifa za uongozi ambao hawana vyeo vya kuwawezesha kupata fursa kutumia vipawa hivyo kwa manufaa ya jamii zetu.
Matokeo yake ni kwamba wenye vyeo (bila kuwa na sifa za uongozi) wataendelea kuvurunda utawala wa jamii zetu huku wale wenye sifa za uongozi (lakini hawana vyeo) "wakigara gara" mitaani pasipo jamii yetu kunufaika na talanta yao.
Nimeanza kwa kuyasema hayo kwa kufungua mjadala huu nilioguswa niandike nami japokuwa kiduchu tu kuhusu kinachoendelea nchini.
Kwenye siku za karibuni kumekuwa na vugu vugu linalotafsiriwa ati ni "vita dhidi madawa ya kulevya", vita ambayo kwa usahihi wake kabisa naiona ni kelele zile zile za kisiasa tulizozioea.
Kwanza kabisa;
Kama kijana, na zaidi nikiwa kama mtanzania niseme kwamba naunga mkono dhamira iliyoonyeshwa na RC Makonda kwa kutaka kutokomeza biashara ya madawa ya kulevya ambayo imeshamiri miaka ya karibuni na kuota mizizi.
Viongozi wengi wamejitokeza huko nyuma kujiapiza kupambana na wauza madawa ya kulevya, lakini viapo vyao vimeishia kuwa viapo hewa bila utekelezaji wowote kwa matendo!
Kwa kiasi fulani inatia moyo kuona hatimaye ametokea kiongozi ambaye sio tu kwamba amejiapiza kupambana na wauza madawa ya kulevya, bali pia anaoneka kuchukua hatua kutuhakikishia kiapo chake hicho… hii inatia moyo. Kwahiyo dhamira hii ya RC Makonda ni ya kutia moyo.
Lakini,
Yawezekana RC Makonda akawa na dhamira safi kabisa kuanzisha vugu vugu hili, lakini kutokana na namna anavyoendesha zoezi hili kinachoonekana ni kushindwa (au kuogopa) kwa vyombo vya Usalama kumshauri kuhusu namna ya kuendesha vugu vugu hili (au wanamshauri lakini hasikii).
Kwa wenye kufuatilia haya masuala kwa muda mrefu, unaweza kupata hisia kuwa kinachoendelea kinaharibu ushahidi dhidi ya wahusika halisi wa biashara hii, kwa kujua au kwa kutokujua.
Nasema "wahusika halisi" kwasababu tukiacha hizi 'sinema' za vikao na waandishi wa habari, Wahusika wa madawa ya kulevya wanajulikana. Hawa nawaongelea wale 'Kingpins'.
Wanajulikana, na vyombo vya usalama wanawajua.
RC Makonda kuwaambia wananchi waandike majina Kuwataja wafanya biashara ya mihadarati, hii inaketa picha kwamba.. Labda serikali haiwajui.. Na kama serikali haiwajui hii ni aibu kubwa kwa Idara yetu ya Usalama wa Taifa na Polisi. Hii kiasi Fulani inatukumbusha mbwembwe za Mrema mwanzoni mwa miaka ya tisini ambapo alipotaka kukomesha ujambazi badala ya kuimarisha Jeshi la Polisi na Idara zake, akaanza kuwalazimisha wananchi kulala nje wakiumwa na mbu, kufanya ulinzi wa jadi wa Sungu sungu.
Nasema hivi kwasababu, kama hawawajui mapapa wa mihadarati inatufanya tujiulize uwezo wa kiutendaji wa TISS, Polisi na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya.
Kwa maslahi mapana na kuepusha mushkeli au kuwakwaza watu, niseme tu kuwa utendaji wa Idara ya Usalama wa Taifa ni wa kuridhisha na wanataarifa za kutosha tu juu ya wahusika wa biashara hii.
Swali, kama wanafahamika kwanini hawachukuliwi hatua??
Ili kuwashitaki hawa mapapa wa mihadarati unahitajika ushahidi wa kutosha ili kuwatia hatiani.. Kwahiyo kwa muda mrefu vyombo vya Usalama Vinahangaika kukusanya ushahidi ili kujenga kesi yenye mashiko dhidi yao.
Hapa ndio sababu kwanini nasema hiki kinachoendekea kinaharibu ushahidi dhidi ya "wahusika halisi" maana wanaanza kufanya shughuli zao kwa tahadhari kubwa zaidi kwa kujua kuwa wanafuatiliwa.
Kwa hiyo badala ya kupoteza muda mwingi kuitisha mikutano na waandishi wa habari, ningemshauri RC Makonda atumie nguvu yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama kuwapush Polish, TISS na Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya kukusanya ushahidi haraka na kuondoa kwenye 'system' maafisa wanaoshiriki kupoteza ushahidi au kuwalinda mapapa wa mihadarati.
.
Kwa kadiri ninavyofahamu, inawezekana katika baadhi ya hawa waliotajwa wamo wahusika halisi, lakini kwa namna suala hili linavyoendeshwa inasababisha muhusika huyo (au wahusika hao) kupata sympath kwenye jamii na hii inasababisha ugumu zaidi kujenga kesi ya kisheria dhidi yao.
Pia RC ni lazima afahamu (na najua anafahamu) kuwa vita hii ni nzito na kamwe haiwezi kuipigana peke yake yeye kama yeye.
Ni lazima tuone uungwaji mkono na Waziri wa Mambo ya Ndani.
Ni lazima tuone uungwaji mkono na Polisi.
Na lazima tuone uungwaji mkono na Mamlaka ya Kupambana na Madawa ya Kulevya.
Vita dhidi ya mapapa wa mihadarati sio rahisi kiasi kwamba unaweza kuishinda kwa "press conference."
Ni vita ambayo ili kuishinda unahitaji mkakati makini, tena sio mkakati wa vikao vya kisiasa.. Bali mkakati wa kijeshi/polisi.
Kwahiyo RC anahitaji 'kumobilise' support kutoka kila kada na jamii.. Ili hata hawa mapapa wakienda kuhonga vyombo vya habari ili wasafishwe kusiwe na mwanya wowote wa kuutumia ili kuwarubuni wananchi.
Tofauti na sasa ambapo namna zoezi linavyoendeshwa imekuwa rahisi mno kwa mapapa hao kucheza na media na kuhadaa wananchi ili wapate sympath.
Kwahiyo, ni muhimu kuzingatia kwamba.. Licha ya dhamira njema RC aliyo nayo, ni lazima tumkumbushe kuwa mtu mwenye kufaa na 'kutosha' katika cheo ni yule mwenye uwezo wa kuunganisha mamlaka ya cheo alicho nacho vikaungana na uwezo wa uongozi na busara.
Nimalize kwa kusema kuwa, hii ndio athari ya kutokuwa na mijadala ya kitaifa ili kutafakari na kujua changamoto na vipaumbele vyetu.
Hatuna utamaduni wa kujadili vipaumbele na changamoto zetu kama taifa! matokeo yake ni kwamba kila anayepata fursa ya kuwa kiongozi anajikuta anajipa jukumu la kutuamulia nini tujadili na nini ni changamoto yetu na kipaumbele chetu, mwishowe tunajikuta kwamba kuendeshwa kwa matukio ndio kama mfumo uliokubalika wa nchi yetu.
Hii vita ni kubwa, na kila mwenye kuonyesha dhamira ya kuipigana anapaswa kuungwa mkono, lakini pia ni lazima tumshauri mtu huyo na kumkumbusha kuwa nchi (na serikali) inaendeshwa kwa Sheria sio akili ya mtu binafsi. Kwamba unaweza ukalala na kuamka na kufanya utakalo.
The Bold