Hallow wana MMU, nahitaji msaada kwa hili linalonitokea kwa sasa.
Kuna binti niko nae kwenye mahusiano huu ni mwaka wa saba sasa, kwakweli nampenda sana na yeye analijua hilo, tatizo lililopo sasa ni kwamba kwa miaka ya hivi karibuni amekua akibadilikabadilika sana yaani simuelewi.
Mwaka jana ilianza kujitokeza hali hii ambapo alipunguza mawasiliano na mimi, ikawa kila nikimsihi tuonane ananipiga chenga. Siku moja alikuja kwangu na akaniomba msamaha akakiri kuwa alikuwa na mahusiano na mtu mwingine.
Nilihuzunika sana, lakini kwasababu nampenda, nikamsamehe.
Tokea mwezi wa nne mwaka huu, hatujaonana wala kukaa pamoja kuzungumza pamoja na jitihada zangu zote za kumsihi tuonane.
Naomba nieleweke, sio kwamba anakataa moja kwa moja, anakubali lakini siku ikifika hatokei na pengine simu asipokee.
Kwasababu nampenda najua kuwa atakuwa amechoka maana anafanya kazi mpaka jumamosi.
Siku moja nikakuta comment ya kajamaa kwenye picha moja aliyoipost Instagram ikanipa shaka kidogo ikanibidi nitake kumfahamu huyo mtu. Huko ndiko nikakutana na picha aliyopiga na mpenzi wangu na comments za kutosha as if ni wapenzi.
Nikamtumia hiyo Picha whatsapp alishtuka, akaanza kuniuliza hiyo picha nilikoitoa, baada ya muda akanipigia simu na kunielezea kuwa nisishtuke kwa hiyo Picha, walipiga tu na huyo mtu kwasababu wanafanya kazi pamoja lakini hamna chochote kinachoendelea kati yao, nikakubali nikamuomba tuonane weekend iliyofuata, hakutokea.
Na mimi nikaacha kumuomba kuonana nae tena. Alhamisi ya wiki iliyopita akanipigia simu akaniahidi angekuja kwangu jumamosi iliyopita, hakuja wala kunitaarifu.
Jana jumapili nikiwa kwenye mishe zangu akanipigia simu akataka aje lakini mimi nikamueleza kuwa sipo nyumbani ila baada ya saa moja hivi nitakuwa nimerudi tayari, akanikubalia.
Baada ya kurudi nikampigia simu hapokei, nikatuma na sms hajajibu mpaka Leo.
Ndugu zangu hivi huyu binti anadhamira ya kweli au kuna kamchezo hapa kanaendelea mimi sina habari, naombeni ushauri.