Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
Taarifa kutoka mkoani Kilimanjaro zinaeleza kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Siha Oscar Themi amenusurika kipigo katika Baraza la Madiwani jana baada ya kuibua mvutano wa kisiasa katika baraza hilo.
Awali Mwenyekiti huyo alikaribishwa na kupewa nafasi ya kusalimia lakini akaitumia nafasi hiyo kueleza sera za chama chake. Hali hiyo iliwakera madiwani wa CHADEMA na kumtaka aache kutumia kikao hicho vibaya, lakini akaonekana kukaidi. Ndipo wakamnyang'anya microphone kabla hajatimua na kupanda gari yake na kuondoka huku akiwaachia mzozo madiwani wa CCM na Chadema ndani ya kikao hicho.